Huyu ndo Mbowe, kaja na plan B na daima hatabiriki!

Huyu ndo Mbowe, kaja na plan B na daima hatabiriki!

Najua ukweli utawauma tu twende mbele turudi nyuma lini wafuasi wa chadema wakamsifu lipumba???ni lini wafuasi wa chadema watakubali wafanye kampeni kwa Liiipumba??? Si mlisemaga hawa Cuf ni Ccm b?? Nyie mmekuwa Ccm C??? Siasa za bongo raha sana hasa linapokuja suala la mgombea hapo ndioo mashati na kelele zinapoanzia washabiki woote watasema ni heri wampe lowasa

Siasa hazina misimamo ya kudumu kama dini. Pale mnapokuwa pamoja katika msimamo wa aina fulani mnashirikiana na pale mnapokwenda tofauti mnaachana. Suala la katiba limewaweka pamoja Chadema,CUF na NCCR Kkwa hoja zao kufanana hivyo usione ajabu kushirikiana. Hilo la kukampeniana kuwa haiwezekani ni hoja mfu kwani iko kwenye kufikiri tuu na si uhalisia.
Tabia za kuhisihisi ni za CCM ndio maana hawataki hata mabadiliko kwani wanahisi hayawezekani.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Next ukawa na watanzania wote na vyama ungana tutavaa t-shert za tanganyika na kofia zake na kila mkeleketwa wa chama atakuwa na bendera ya chama chake.kama wewe ni cuf utakuwa na t shirt ya tanganyika na kofia na bendera ya cuf na wengine hivyo hivyo kama chadema hivyo hivyo
 
Binafsi niwapongeze ukawa kwa malengo yao matukufu na Mungu azidi kuonekana kupitia ukawa
 
Next ukawa na watanzania wote na vyama ungana tutavaa t-shert za tanganyika na kofia zake na kila mkeleketwa wa chama atakuwa na bendera ya chama chake.kama wewe ni cuf utakuwa na t shirt ya tanganyika na kofia na bendera ya cuf na wengine hivyo hivyo kama chadema hivyo hivyo

We ndo umeongea. Kuunganisha nguvu siyo kuua vyama. Hapa siyo Kenya ambapo vyama vikiungana inamaanisha kuua vyama na kusimama kwenye uchaguzi kama muungano.
 
swali langu ni je, muungano huu utadumu? usije kuwa tu ni muungano wa kupinga muungano!
 
Mbowe ni mjanja sana, anawalaghai waingie kingi af apige mihela, chezea mjasiriamali wa kisiasa weye
 
Katika kikao kimoja tulichofanyia Mwanza mwaka jana mwishoni Mbowe aliwakuna wajumbe alipotupa siri kwamba alikataa kuwa mwenye kiti wa Chadema mpaka kamati kuu walipokubali mashariti yake. Baadhi ya mashariti ilikuwa kumuomba na kamati kuu ikubali Dr Slaa awe Katibu mkuu badala ya makamu mwenyekiti, kuruhusu kufungua milango ili aingize watu toka vyama vingine na kubadilisha rangi za bendera ya chama. Alitwambia jisi alivyopata shida kuwashawishi wazee wa chama kukubali kombati kuwa vazi la chama na kadhalika. Ilikuwa story ya kuvutia sana!

Leo wakati Ccm wakidhani tuna tofauti kubwa sana na vyama vingine hasa Cuf, na walijitahidi sana kupanda chuki kati yetu. Na zaidi walijitahidi kuivuruga Chadema kwa kutumia mamluki, kumbe Kamanda wa anga anafkiria kitu kikubwa zaidi. Ametoka na plan B amabayo inawafanya Ccm warudi kwenye drawing board kupanga upya mbinu tofauti na hii ya mamluki. Kwa vyovyote sasa mbinu ni kuchonganisha huu muungano maana hauwezi kuwaacha salama.

Mchambuzi yoyote wa siasa anajua kwamba tukiingia kwenye uchaguzi kwa muungano huu Ccm watatoka jasho kweli kweli. Muungano huu utasambaratisha kabisa propaganda ya udini na ukabila, utasambaratisha propaganda ya uchu wa madaraka. Lakini italigawa taifa katika kanda ambazo ni rahisi kupiga kampeini kulingana na sehemu vyama vinavyokubalika. Itapunguza mzigo wa gharama maana utashughulikia eneo dogo kwa ufanisi.

Long live Kamanda Mbowe!


Kwani hoja iliyosababisha kuungana ni Uongozi au Katiba? Naapa na naamini Hakuna muungano hapa. Chama kinachoongozwa ka matukio hakiwezi kuchukua dola hata siku moja. Yaani bila katiba Mpya SIJUI CHEDMA wangekuwa na hoja gani. Short living CHADEMA
 
"Leo wakati Ccm wakidhani tuna tofauti kubwa sana na vyama vingine hasa Cuf, na walijitahidi sana kupanda chuki kati yetu. Na zaidi walijitahidi kuivuruga Chadema kwa kutumia mamluki, kumbe Kamanda wa anga anafkiria kitu kikubwa zaidi. Ametoka na plan B amabayo inawafanya Ccm warudi kwenye drawing board kupanga upya mbinu tofauti na hii ya mamluki. Kwa vyovyote sasa mbinu ni kuchonganisha huu muungano maana hauwezi kuwaacha salama."

Haya sasa mahaba niue huyu jamaa kasahau kabisa abla kadabla za humu JF na anawasingizia CCM tena wakati wao walikuwa hawataki kusikia kuhusu CUF na kuwaita wameolewa nao na balaa lao lilizidi alipoteuliwa Mbatia viti maalum. Huyu dogo mgeni humu JF au ndio mahaba niue. Walipoteua mawaziri kivuli na kutupa nje CUF wote, mbona mnasahau mapema sana.
 
zito ungana na wenzio omba msamaha watanzania tutakusamehe,uongeze nguvu kwenye jeshi la wokovu wa nchi yetu.tulikomboe taifa letu
ZITTO hafai tena ni muasisi na master mind wa ACT. CHADEMA msilogwe kumrejesha jamaa Huyu. Think tank wa ACT ni Kitila na jamaa mmoja wa CWT mkiti wa chama cha walimu
 
Kwani hoja iliyosababisha kuungana ni Uongozi au Katiba? Naapa na naamini Hakuna muungano hapa. Chama kinachoongozwa ka matukio hakiwezi kuchukua dola hata siku moja. Yaani bila katiba Mpya SIJUI CHEDMA wangekuwa na hoja gani. Short living CHADEMA

...uhai wa chama ni ktk matukio ndo maana kila tukio chadema watakalofanya,ccm wataiga,kwaiyo ccm ni maiti inaburuzwa tu na cdm. Tumeimarisha chadema diaspora,angalia kilasiku mnasafiri kupambana na cdm..,
 
Sasa nimekubali maneno ya mh.Mbowe kwamba,hata kama ccm watatupiga kwa kutumia polisi!basi iko sk polisi haohao watatulinda!ushauri wangu ni kwamba,viongozi wa UKAWA jamani msikubali kuhadaiwa!najua ccm wanajipanga kuwavuruga!pamoja sana viongozi wangu
 
Mkuu huchi huo ulikuwa upeo wao huwezi kulazimisha kuwa ndo agenda ya chama kama utakumbuka Mnyika suala La Mtei alilitolea ufafanuzi.
Alitakiwa Mzee Mtei mwenyewe mwenye Chadema yake aliyesema tume ya katiba imejaa waisalamu ndiye angelitolea ufafanuzi siyo Mnyika. Kumbuka "anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo" na Mzee Mtei ndiye Nyerere wa Chadema, kwa mtazamo ule wa udini Mtei hawezi kukubali huo umoja wenu mgombea awe muislamu
 
Back
Top Bottom