Huyu ndo Mbowe, kaja na plan B na daima hatabiriki!

Huyu ndo Mbowe, kaja na plan B na daima hatabiriki!

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Katika kikao kimoja tulichofanyia Mwanza mwaka jana mwishoni Mbowe aliwakuna wajumbe alipotupa siri kwamba alikataa kuwa mwenye kiti wa Chadema mpaka kamati kuu walipokubali mashariti yake. Baadhi ya mashariti ilikuwa kumuomba na kamati kuu ikubali Dr Slaa awe Katibu mkuu badala ya makamu mwenyekiti, kuruhusu kufungua milango ili aingize watu toka vyama vingine na kubadilisha rangi za bendera ya chama. Alitwambia jisi alivyopata shida kuwashawishi wazee wa chama kukubali kombati kuwa vazi la chama na kadhalika. Ilikuwa story ya kuvutia sana!

Leo wakati Ccm wakidhani tuna tofauti kubwa sana na vyama vingine hasa Cuf, na walijitahidi sana kupanda chuki kati yetu. Na zaidi walijitahidi kuivuruga Chadema kwa kutumia mamluki, kumbe Kamanda wa anga anafkiria kitu kikubwa zaidi. Ametoka na plan B amabayo inawafanya Ccm warudi kwenye drawing board kupanga upya mbinu tofauti na hii ya mamluki. Kwa vyovyote sasa mbinu ni kuchonganisha huu muungano maana hauwezi kuwaacha salama.

Mchambuzi yoyote wa siasa anajua kwamba tukiingia kwenye uchaguzi kwa muungano huu Ccm watatoka jasho kweli kweli. Muungano huu utasambaratisha kabisa propaganda ya udini na ukabila, utasambaratisha propaganda ya uchu wa madaraka. Lakini italigawa taifa katika kanda ambazo ni rahisi kupiga kampeini kulingana na sehemu vyama vinavyokubalika. Itapunguza mzigo wa gharama maana utashughulikia eneo dogo kwa ufanisi.

Long live Kamanda Mbowe!
 
Namtakia mafanikio mema... tuko pamoja na kila mwenye malengo ya kuwaondoa genge la mafisadi na wapora rasilimali za nchi ili kushibisha matumbo yao na kuneemesha familia zao ...
 
  • Thanks
Reactions: mpk
Kweli tupu.
Katika vitunilivyokuwa nikiomba vitokee kwa haraka sana ni muungano wa vyama vya upinzani ili wasimamishe mgombea mmoja wa urais nikiona hili limetimia kwakweli niraweka sherehe nikiamini tayari dubu hatari kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania limeondoka

Nitaomba usiku na mchana Mungu azidi kumlinda yule aliekuja na wazo mujarabu la kuwaunganisha wapinzani kuwa kitu kimoja.
Bado naomba hilo litokee.

BACK TANGANYIKA
 
Kama wataweza kukubaliana katika kuungana, basi zile sababu za ukatoliki, ukaskazini nk. zitakuwa hazina nguvu tena. Sasa sijui itatafutwa slogan ipi nyingine ya kuwachafua. Ni vyema watawala wetu waachane na propaganda, wafanye mambo yao kwa uadilifu, na wapambane na changamoto kwa uhalisia wa mambo.
 
Kweli tupu.
Katika vitunilivyokuwa nikiomba vitokee kwa haraka sana ni muungano wa vyama vya upinzani ili wasimamishe mgombea mmoja wa urais nikiona hili limetimia kwakweli niraweka sherehe nikiamini tayari dubu hatari kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania limeondoka

Nitaomba usiku na mchana Mungu azidi kumlinda yule aliekuja na wazo mujarabu la kuwaunganisha wapinzani kuwa kitu kimoja.
Bado naomba hilo litokee.

BACK TANGANYIKA
 
Hongera UKAWA tengenezeni hadidu za rejea mapema maana muda wa kujiandaa unayoyoma. Tunachotaka kuona na kusikia ni kuwaambia watanzania ukweli na mara wakishawapa kura muonyesha hiyo ya ukweli sio yajirudie yale yale ya CCM. Inawezekana tusonge mbele!
 
Tunawaombea kila atakayekuwa anapambana na mtandao wa mafisadi Tanzania. CDM wanaonesha njia na sasa wameunda umoja mzuri amabao ndiyo mafanikio na tuko nyuma yao wasisikilize propaganda zozote wapige tu kazi kama wanavyofanya kila siku mungu awabariki hata zito kabwe mungu akubariki usipotee tena zito jirudi sasa tutakuombea msamaha
 
hao ndio watu wenye upeo. elimu si cheti bali mawzo, unaweza kuwa dr lakini hamna kitu.
 
zito ungana na wenzio omba msamaha watanzania tutakusamehe,uongeze nguvu kwenye jeshi la wokovu wa nchi yetu.tulikomboe taifa letu
 
Hatutakubali ZZK asiingie ktk historia ya ukombozi wa nchi hii labda yeye mwenyewe!
 
he is outstanding politician ever.....may living God help and support all his doings!!!!
 
Tangu lini mbowe akafanya kazi au jambo lenye mafanikio kwa chama au taifa.
 
Sasa ni mashambulizi tu
Kamanda wa anga freeman
Mkuu wa makombando ibrahim
Mkuu wa kikosi cha aridhi tindu
Mkuu wa kikosi cha maji wilbord
Mkuu wa kikosi cha mawasiliano james
Aisee ccm bye bye dadadeki full kikosi
 
Sasa ni mashambulizi tu
Kamanda wa anga freeman
Mkuu wa makombando ibrahim
Mkuu wa kikosi cha aridhi tindu
Mkuu wa kikosi cha maji wilbord
Mkuu wa kikosi cha mawasiliano james
Aisee ccm bye bye dadadeki full kikosi

Wenzako wa Lumumba unajua hali zao? uwe na huruma ndg!
 
Back
Top Bottom