Huyu ndiye Traffic anayehitajika D'Salaam

Hii kiboko kwa dar huyu hafai aisee maana atasababisha foleni sana watu watakuwa hawatembezi magari watakuwa wanataka kuona tu hii burudani ya trafiki na kucheka hahahaha, amenichekesha sana ila anaonekana anafanya sana mazoezi duh, ila hawa wa kwetu na vitambi vyao wataweza kweli hii kitu?
 
Wabongo afanye vitimbi hivyo rushwa ataomba saa ngapi? Wa bongo huwa wanajificha kusubiri kosa litokee ili wapate rushwa!
 
Mhh, huu nao ni ubunifu wa aina yake, ila kwa Dar magari yatagongana kwa kushangaa. Very nice, comedy hadi kazini? kweli wenzetu wako juu
 
Unajuwa kazi yoyote ukiwa unaichukia, basi tafuta sababu ya kuipenda (Funny side ya hiyo kazi).
 
Teeeh teeeh teeeh! Ila Mayenu nae alikuwa kiboko, sijui hata yuko wapi siku sizi inga pale Salender bridge na Morocco napo kuna Samwel nae chizi chizi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom