Huyu ndiye Rais Samia ndani ya siku 69 za uongozi wake

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
HUYU NDIYE RAIS SAMIA NDANI YA SIKU 69 ZA UONGOZI WAKE.

Na Elius Ndabila (MHITIMU LLB-MZUMBE)

Mara nyingi duniani kote kiongozi wa nchi huanza kupimwa utumishi wake kwa kipindindi Cha siku mia moja. Lakini si sheria wala kanuni ni utaratibu tu ambao watu wanadhani unaweza kusaidia kujua uwezo wa kiongozi.

Katika kuelekea siku mia moja za Mama Samia, Rais wa Tanzania, leo ninataka nigusie kidogo juu ya utawala wake wa siku 69 tangu alipoapishwa tr. 19/3/2021 baada ya kifo cha mtangulizi wake Hayati Dkt John Magufuli.

Kukuza na kuendeleza Diplomasia na nchi zingine. Rais Samia kwa kipindi hiki kifupi ameendelea kujenga mahusiano ya kikanda na Kimataifa kwa kuwa anaamini kuwa maendeleo ya nchi ni ya kutegemeana. Pamoja na kutembelewa na wageni mbalimbali toka nje lakini hata yeye kwa kipindi hiki kifupi ameshafika Uganda na Kenya. Ikumbukwe kuwa ilizuka Vita ya maneno kati ya Kenya na Tanzania ambayo ilisababisha hata mdororo wa biashara wa nchi hizi mbili. Mhe Samia na Rais wa Kenya walikaa na kulitatua na kujenga mazingira mazuri ya Diplomasia ya kiuchumi. Tukumbuke kuwa uchumi wa sasa unajengwa zaidi na diplomasia ya uchumi. Nchi zote ambazo uchumi wake unakua na kuimalika basi ujue kuwa mahusiano yake na mataifa uko vizuri. Dunia ya sasa mahusiano ni Uchumi, hakuna mahusiano ya stori.

Mhe Samia awali alizungumza kuwa Tanzania haiwezi kujifungia. Tuna miradi mikubwa, lazima wenzetu watusaidie. Na kwa kulifanya hilo alimteua mwanadipolomasia nguli Mama Mlamula kuhakikisha zile tofauti ndogo ndogo zilizokuwa zinapandkizwa juu ya Tanzania zinamalizwa.

Vita dhidi ya Corona. Mhe Samia kwa siku zake 69 ameonyesha kuwa Corona ipo na nilazima Tanzania nayo ianze kupambana nayo Kama mataifa mengine. Mhe Rais alisema kuwa Tanzania si kisiwa, na aliunda tume ambayo alisema itaishauri serikali. Ikumbukwe kuwa ugomvi mkubwa wa Tanzania na baadhi ya mataifa ilikuwa ni namna Tanzania inavyolichukulia suala la covid 19. Lakini Rais Samia amesistiza kuchukua hatua zote ambazo wenzetu wanazichukua hususani uvaiji wa Barakoa. Mapambano hayo yameiweka Tanzania katika sura mpya katika medani za Kimataifa kwani mwanzo Tanzania ilitafsiriwa kama wakaidi.

Kupiga Vita uonevu hasa kwa Wafanyabiashara. Ikumbukwe kuwa kulipa kodi ni takwa la kisheria na kila mfanya biashara anapaswa kulipa kodi. Lakini kukusana kodi kwa kutumia nguvu na vyombo vingine vya dola ni kuhatarisha usalama wa biashara. Mama Samia baada ya kuapishwa tu alisema kazi ya kwanza ni kuhakikisha TRA na vyombo vingine vinavyokusanya kodi kukusanya kwa mjibu wa sheria. Alikataza mamlaka kufungu akaunti za Wafanyabiashara kibabe na zaidi aliwaasa wote waliokuwa wamefanyiwa hivyo kufunguliwa akaunti zao. Alienda mbali kwa kuitaka Wizara inayohusika na uwekezaji kutokuwa kikwazo. Kwa siku hizi 69 tumeshuhudia Wawekezaji wengi wakianza kurudi baada ya kuhakishiwa usalama wa biashara zao na mitaji yao. Wafanyabiashara waliokuwa wamekimbilia nchi za jirani kwa unyanyasaji wa sheria za TRA wameanza kurejea.

Uhuru wa vyombo vya habari, baada ya kuapishwa tu Mhe Rais aliagiza online tv zote ambazo zilikuwa zimefungiwa kufunguliwa. Mhe Rais kwa mkutadha wa kawaida ni muumini wa haki, lakini aliwataka wanahabari hao kuzingatia weredi wao. Hadi leo Mhe Samia anafikisha siku 69, online tv zote zipo hewani zaidi ya 440 zilizosajiliwa. Hivyo siku 69 za Mhe Rais zimeongeza wigo wa habari.

Suala la Uhuru wa kufanya shughuli za kisiasa, Mhe Samia baada ya kuapishwa amefungua milango kwa wanasiasa kufanya kazi zao za kisiasa na pia ameruhusu majadiliano Kama kuna mahali kuna mikanganyiko. Na bado amesema atakutana na viongozi wa vyama vyote ili kuboresha demokrasia.

Pamoja na hivyo, kwa siku 69 ambazo amekuwa kiongozi kauli zake nyingi zinaleta tabasamu kwa Watanzania. Mhe Samia anabeba dhima nzima ya mwanamke anayetaka kuona familia yake inafuraha muda wote. Ninaamini wale Watafiti ambao Mhe Prof Lipumba alikuwa akiwatumia kwenye kampeni kuwa Watanzania hawana furaha kwa kipindi hiki Cha Mama Samia Watanzania wengi wameongeza furaha, inawezekana ni malezi thabiti ya Mama.

Ameongeza kasi, ubunifu na maarifa katika uwajibikaji. Mhe Samia amejipambanua ktk kuhakikisha sheria haiwi kikwazo Cha watu kulijenga Taifa. Na amekuwa anasistiza Kama sheria ni kikwazo basi zifanyiwe marekebisho. Katika siku 69 za uongozi wake amefanya mabadiliko makubwa kwenye sekta mbalimbali katika kuongeza kasi ya kuchapa kazi.

Kuendelea kusimamia miradi ya kimkakati ambayo ilianzishwa na mtangulizi wake. Mhe Samia alisema ataendelea kuijenga miradi yote ya kimkakati ambayo ilisimamiwa na mtangulizi wake na ameendelea kuisimamia kwa vitendo.

Yapo Mambo mengi ambayo Mhe Samia ameonyesha umahiri wa kuyashughulikia kwa kipindi hiki Cha "KAZI IENDELEE". Nitaendelea kuwapa mafanikio yake hadi atimize siku 100 ambazo ndizo kipimo kwa viongozi wengi.

Wajibu wetu Watanzania ni kuendelea kumuombea Mhe Rais ili yale aliyokusudia aweze kuyafanya, lakini wale waliopewa nafasi ya kumsaidia basi wamsaidie kwa dhati ili asikwamishwe wala kucheleweshwa. Mhe Rais na WASAIDIZI wake Wana kazi kubwa kuhakikisha Uchumi ulioshuka kutoka zaidi ya asilimia sita hadi asilimia nne na zaidi unakuzwa.

0768239284
 
Kule wizarani ni mwendo wa kujilipa posho tuuuu kwa kisingizio cha ^Kazi Maalumu^ Bi Mkubwa atajutia sana ukurupukaji na ulimbukeni wake kuliko hata Mstaafu wa Msoga
 
Back
Top Bottom