Huyu ndiye atakayeshinda Urais 2015

Onesmo Kyauke

Verified Member
Feb 9, 2015
67
70
Wanajamvi,
Kwa watu wanaotoa maoni huru bila ushabiki uchaguzi wa mwaka huu ndio uchaguzi mgumu zaidi katika historia ya Taifa letu. Ni kweli kwamba Chama cha Mapinduzi kimeshinda katika chaguzi zote za vyama vingi lakini mwaka 1995 na 2010 kilipata kura za urais wa asilimia 60. Hii ina maanisha kwamba iliwazidi wapinzani kwa asilimia 10 tu. Safari hii wapinzani wameimarika kwa sababu zifuatazo:-

(i) Vijana wengi na wasomi ambao ndio wanaunga zaidi mkono wapinzani wamejiandikisha na wana hamasa ya kupiga kura.
(ii) Upinzani ambao uligawanyika sana katika chaguzi zilizopita sasa umeungana
(iii) Upinzani umeonyesha uwezo wa rasilimali kwa ajili ya kupiga kampeni na hivyo kwa mara ya kwanza wapinzani wameweza kukabana koo na ccm katika kupiga kampeni.

Zipo sababu nyingi kuonyesha kuwa upinzani wa mwaka huu ni mkubwa zaidi kupita kipindi kingine chochote. Kwa tathmini yangu, yeyote katika wagombea wawili yaani Mh Dr Magufuli na Mh Lowassa anaweza kushinda. Kitakachomsaidia mmoja wao ashinde ni jinsi gani chama chake kitaweza kuhamasisha watu watoke kwenda kupiga kura. Kila mmoja ana wafuasi wa kutosha kumpa kura milioni 9 au 10 ambazo zitatosha kumpa ushindi. Swali ni je, wafuasi wao watajitokeza kupiga kura? Je, ni wafuasi wa upande gani wana hamasa zaidi?

Tusubiri tuone. Lakini nashauri kwa mfuasi yeyote wa upande mmoja wao lazima ahakikishe anawashawishi wale watakaopigia kura upande wake wajitokeze kwa wingi. Nawatakia uchaguzi mwema.,
 
Nkobhe

JF-Expert Member
Jan 26, 2015
452
225
endelea kujidanganya Rais alishachaguliwa nyie mnaenda kutimiza masharti tuu ya kuingia ikulu
 
MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,122
2,000
Maelezo yako hayajakamilika bila kumalizia " na kuzilinda kwa umbali wa mita 100 tu bila kuchoka wala kurubuniwa"

Wanajamvi,
.............

Zipo sababu nyingi kuonyesha kuwa upinzani wa mwaka huu ni mkubwa zaidi kupita kipindi kingine chochote. Kwa tathmini yangu, yeyote katika wagombea wawili yaani Mh Dr Magufuli na Mh Lowassa anaweza kushinda. Kitakachomsaidia mmoja wao ashinde ni jinsi gani chama chake kitaweza kuhamasisha watu watoke kwenda kupiga kura. Kila mmoja ana wafuasi wa kutosha kumpa kura milioni 9 au 10 ambazo zitatosha kumpa ushindi. Swali ni je, wafuasi wao watajitokeza kupiga kura? Je, ni wafuasi wa upande gani wana hamasa zaidi?

............
 
Mantown

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
265
195
Wanajamvi,
Kwa watu wanaotoa maoni huru bila ushabiki uchaguzi wa mwaka huu ndio uchaguzi mgumu zaidi katika historia ya Taifa letu. Ni kweli kwamba Chama cha Mapinduzi kimeshinda katika chaguzi zote za vyama vingi lakini mwaka 1995 na 2010 kilipata kura za urais wa asilimia 60. Hii ina maanisha kwamba iliwazidi wapinzani kwa asilimia 10 tu. Safari hii wapinzani wameimarika kwa sababu zifuatazo:-

(i) Vijana wengi na wasomi ambao ndio wanaunga zaidi mkono wapinzani wamejiandikisha na wana hamasa ya kupiga kura.
(ii) Upinzani ambao uligawanyika sana katika chaguzi zilizopita sasa umeungana
(iii) Upinzani umeonyesha uwezo wa rasilimali kwa ajili ya kupiga kampeni na hivyo kwa mara ya kwanza wapinzani wameweza kukabana koo na ccm katika kupiga kampeni.

Zipo sababu nyingi kuonyesha kuwa upinzani wa mwaka huu ni mkubwa zaidi kupita kipindi kingine chochote. Kwa tathmini yangu, yeyote katika wagombea wawili yaani Mh Dr Magufuli na Mh Lowassa anaweza kushinda. Kitakachomsaidia mmoja wao ashinde ni jinsi gani chama chake kitaweza kuhamasisha watu watoke kwenda kupiga kura. Kila mmoja ana wafuasi wa kutosha kumpa kura milioni 9 au 10 ambazo zitatosha kumpa ushindi. Swali ni je, wafuasi wao watajitokeza kupiga kura? Je, ni wafuasi wa upande gani wana hamasa zaidi?

Tusubiri tuone. Lakini nashauri kwa mfuasi yeyote wa upande mmoja wao lazima ahakikishe anawashawishi wale watakaopigia kura upande wake wajitokeze kwa wingi. Nawatakia uchaguzi mwema.,
Umekurupuka au ulilala mchana?
 
Top Bottom