Huyu ndio Pablo Escobar: Muuza madawa ya kulevya ambaye hajapata kutokea duniani mpaka leo

MT255

JF-Expert Member
May 3, 2012
3,381
4,648
Anaitwa Pablo Escobar a.k.a El Doctor, El Patrón,Don Pablo,El Señor, El Magico.

Kila $1 aliyokua anaweka katika biashara yake alikua anapata profit OR return ya $200.

Alikuwa anakusanya pesa haweki bank, anatunza ndani chini ya ardhi, juu ya dari or ukutani. Adui pekee wa hela zake walikuwa ni Panya wenye njaa kali. Kila mwaka inasemekana alikua anapoteza 10% ya faida ambayo kwa haraka haraka ni $b1, Panya walizokuwa wanakula.

Marekani na Serikali ya Colombia ilitaka Pablo akamatwe na afungwe. Akakubali but Gereza akajenga yeye. Ndani ya gereza kulikuwa ni kama 5star hôtel. Alijiwekea kila kitu, Jacuzi, Bar, Pub, TV,na vitu kibao vya thamani. Pia wanawake wakawa wanaingia na akiwa jela alikuwa ana uwezo wa kutoka na kurudi kisirisiri, coz walinzi wa gereza alikuwa anawahonga vizuri sana.

Baadae, Pablo alichoka maisha ya Jela la Hôtel, anataka kurudi kitaa, akatoroka. Wakati anatoroka akachukua familia yake na walinzi wake wakakimbilia Maporini. Wakati wapo huko vichakani, mtoto akaugua ghafla na kukawa na baridi sana, ukahitajika moto unajua Pablo alochofanya?

Aliwasha moto wa kutoa baridi la ugonjwa wa kwa mwanae kwa kutumia noti zaidi ya 2million dollars, ziliwasha moto mtoto aote moto kupata joto, na kupika kwa note za $2,000,000, za kibongo ni b3 na m240.

Alikuwa ananunua na kutumia Rubber band za $2,500 = tsh 4,050,000 za kibongo kufungia hela zake kila mwezi, so kwa mwaka alikuwa ananunua rubber band za $30,000 = 48,600,000 kufunga tu mihela yake (hata BOT hawatumii rubber band za $2,500 kwa mwezi na haijawahi kutokea kwa mtu wala taasisi)

Alinunua ndege kwa ajili ya kusafirishia hela zake tu, kila trip ndege ilikuwa inabeba $10m. Mwaka 1989, Forbes ilimtaja kama tajiri wa 7 duniani, anakadiriwa kuwa na utajiri wa $25-30b, watu wake wa karibu wanasema alikuwa anazidi hata hapo coz kwa siku alikuwa anatengeneza sio chini ya $60m, coz kwa mwezi alikuwa anasafirisha zaidi ya 80-100t USA.

Na ubabe wake wote, Pablo alikuwa anaogopa sana kufa. Baada ya kutoroka Jela, serikali na jeshi la Colombia wakawa wanamtafuta Pablo, akawa-offer serikali iachane nae na atailipia serikali deni ililokuwa inadaiwa $b10 zaidi ya tirioni 18 za kibongo, ili serikali imalize deni inalodaiwa, lakini serikali ilikataa, msako wa Pablo wakakabidhiwa wamarekani na kumuua December 2/1993.

Mpaka leo hongo/rushwa kubwa duniani kuwahi kutokea ni hiyo ya $10b ya Pablo kutaka kulipa deni la taifa la Colombia, 10b usd = trilioni 18.


Shukuru Mungu hukuzaliwa Colombia wakati huyu jamaa yupo. Anaaminika kuwa mtu katili kabisa tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu. Haijawahi tokea. Kuua kwake ni kama anatafuta appetite ya kitu.

Huyu alikuwa ni muuza madawa ya kulevya. Sio drug dealer ni drug lord kabisa. Ukiambiwa vita vya madawa ya kulevya vinaweza vikaitikisa nchi kubali. Na wote tunakubaliana na taharuki iliyotokea kipindi cha nyuma. Vitu vingi sana viliibuliwa.

Sasa basi huyu mtu ambaye alikuwa ni notorious aliaminika kuwa na mtandao mkubwa sana ndani ya nchi ya colombia. Licha ya kuwa ni muuwaji ila aliwajali wananchi. Ndio mana ilichukua muda wa yeye kuangamizwa. Aliwahi kumteka hata makamu wa raisi wa colombia. Hakuna kwake kitu kilichoshindikana

Alihakikisha kuwa ananunua maaskari wote, majaji na wanasheria na viongozi wa serikali. Mtu yeyote yule aliyekuwa anajitokeza kuanzisha mipango ya kumkamata alikuwa hamalizi hata siku. Operation nyingi za kijeshi zilifeli dhidi yake kutokana pia na wanajeshi kuogopa kuwa kwenye commanding force ya kumuondoa kabisa. Hakuna aliyepona.

Hakuna aliyesalimika alipokuwa akifanya operation zake. Aliua watu mia kwa ajili ya kumtarget mtu mmoja. Ilikuwa ni kawaida yake. Alishawahi kulipua ndege ya abiria kwa ajili ya kumpata mtu mmoja aliyekuwamo humo.

Raisi wa colombia enzi hizo alikubali na bunge lilikubaliana pablo asikilizwe. Nchi haikutawalika na hakuna kitu kilitawalika. Alikuwa na pesa nyingi sana hadi nyingine zilikuwa zinaliwa na panya kwa sababu zilipokuwa zinawekwa zilikuwa haziguswi kwasababu zilikuwa ni nyingi. Aliwahi kupigwa na baridi yeye na familia yake ambapo alichoma zaidi ya mabilioni ya hela ili mradi ajikinge na baridi.

Aliwapa maafisa masharti kuwa ajitengenezee jela yake ambapo kila kitu kiwemo na pia walinzi watakaolinda jela hiyo wawe ni wa kwake. Serikali ilikubali na baadae kweli alijisalimisha yeye mwenyewe na kwenda kukaa hiyo jela. Baadae jeshi la nchi hiyo lilimfanyia mashambulizi ya kushtukiza. Pablo aliua askari wote na akafanikiwa kutoroka jela hiyo na kukimbilia msituni.. itaendelea

ICYMI-Ben R.Mtobwa ametangulia mbele ya haki ,Mwenyezi Mungu alimpa karama ya utunzi ,ubunifu na umakini wa uandishi wa vitabu katika kiwango cha hali ya juu.

Ukimsoma Ben Mtobwa unakuwa mtumwa wa vitabu vyake kwa maneno matamu na lishe bora ya nafsi na ubongo kwa maandiko .Mtobwa hayupo duniani ila kazi zake bado zipo hai kwa vizazi vyote vijavyo.Dance with the Angels GhostWritter Ben R.Mtobwa.

Kitabu chake cha ‘’Pesa zako zinanuka’’ kilinipa funzo kubwa sana kiasi ambacho kila nisomapo na kumtizama, Pablo Emilio Escobar Gaviria a.k.a Don Pablo (Sir Pablo) a.k.a El Padrino (The Godfather) a.k.a El Patrón (The Boss) a.k.aEl Señor (The Lord) a.k.a El Mágico (The Magician) a.k.a El Pablito (Little Pablo) nasema Pablo Emilio Escobar Gaviria Pesa Zako Zinanuka.

Mzee , Abel de Jesús Dari Escobar ,ambaye alikuwa mkulima na mkewe Hermilda Gaviria ambaye alikuwa mwalimu wa shule za awali tarehe ,1 December 1949 wanabahatika kupata mtoto wao watatu na kumpa jina la ,Pablo Emilio Escobar Gaviria .

Pablo alisoma chuo cha Universidad Autónoma Latinoamericana, lakini hakuweza kumaliza degree yake sababu alikuwa anapenda sana pesa kuliko shule .

Kwa hiyo akaacha chuo na kuingia mtaani kuitafuta pesa kwa kutumia machozi jasho na damu badala ya kutumia akili.Mtaani kuna elimu bora na darasa la maisha ,Pablo akaamua kuingia mtaani na kuacha vyeti vyuoni.

Miaka ya 1970 ,Pablo alikuwa anauza sigara pamoja na tiketi bandia za michezo ya bahati nasibu.,kisha akajiingiza kwenye uwizi wa kuiba magari na mchezo mchafu wa kuteka watu kisha kuhitaji pesa kwa ndugu na jamaa wa mtu aliyemteka .

Kwa kifupi Pablo alikuwa na shida ya pesa ,aliipenda sana pesa na akawa mtumwa wa pesa na ndio maana alikuwa anatumia njia mbaya kuipata pesa na kuimiliki pesa.Alipokuwa na umri wa miaka 22 alikuwa anamiliki kiasi cha $1 million,alipofikisha umri wa miaka 26 alikuwa na US $3 million.

1975 alianza kuuza unga wa madawa ya kulevya [powder cocaine] nchini Marekani.Biashara yake ilikuwa ni kubwa na yenye wateja wengi sana nchini Marekani, kiasi ambacho uhitaji wa soko ulikuwa mkubwa sana kumfanya Pablo kuongeza idadi ya usafirishaji wake wa madawa ya kulevya kuwa 70 to 80 tons kwa mwezi kulingana na uhitaji mkubwa wa soko lake kwa wateja wake.

Pesa huleta jina kiburi na maringo na siku zote pesa inapozungumza ukweli huwa unajificha na uongo unatamalaki.Pablo alitengeneza eneo muhimu kwa ajiri ya usafirishaji wa madawa yake ya kulevya katika kisiwa cha Bahama 220 miles sawa na km 350 kusini mwa mji wa Florida ili kuweza kumrahisishia kusambaza bidhaa yake kwa ubora na urahisi .

Pablo alisambaza madawa ya kulevya katika nchi za: Marekani, Mexico, Puerto Rico, Dominican Republic, Venezuela, na Spain kiasi ambacho biashara hii ilimuingizia kiasi cha US $70 million kwa siku moja, na kumfanya kuzalisha kiasi cha $26 billion kwa mwaka pekee.

Kwa week moja pekee , Pablo Emilio Escobar Gaviria alitumia kiasi cha US $1000 kununua rubber band za kufungia pesa zake.,wakati mwenyezi Mungu anasema tumtolee dhaka na dhabihu kuwa kumpa 10% ya kipato chetu cha haki na halali ila (10%) ya pesa za Pablo zilikuwa zinaliwa na panya sababu alihifadhi kwenye ghala na sio Benki sababu zilikuwa ni pesa chafu.

Pablo alinunua ndege, helicopters ,magari makubwa ya kubebea cocaine na akaongeza submarines mbili za kubebea cocaine kusambaza katika nchi zote zenye wateja wa madawa ha kulevya.

Pablo alitengeneza mrija wa pesa kiasi ambacho pesa zilimzidia na akaanza kuchimba makaburi na kufukia pesa huku zikiwa zinalindwa na watu . Pesa inavyozidi ongezeka ndio njaa ya kuitafuta inavyozidi kuwa kubwa,

Pablo aliathirika na pesa na sio kuathirika na madawa ya kulevya aliwahonga viongozi wote wa serikali waliojaribu kumfuatilia juu ya biashara yake ,aliwahonga wafanyakazi wenye uwezo mkubwa kwenye maswala ya Bank kiasi ambacho alipata wazo la kutakatisha pesa zake na kuepukana na[ AML-Anti Money lunadry ]....Itaendeleaaaa kesho.[HASHTAG]#UtuBusaraUjingaHasara[/HASHTAG]

cef6b85a08cb2294523ca25ce774842f.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • 1422652131639.jpg
    1422652131639.jpg
    145.3 KB · Views: 5,305
  • 1422652145759.jpg
    1422652145759.jpg
    104.8 KB · Views: 5,102
miaka ya 90s mtunzi na mchoraji maarufu John Kaduma aliwahi kuandika stori kuhusu madawa ya kulevya iliyokwenda kwa jina la Pablo zungu kupitia jarida la kiu kwa walioisoma stori watakubaliana nami kuwa ilikuwa stori nzuri sana japo haikufika mwisho
hivyo nikisikia au kusoma Pablo nakumbuka mbaali
 
Mleta mada tupe source hili bandiko lako. Ingawaje ni kweli kwamba huyu bwana alikuwa drug lord mashuhuri, mengine kwenye hiyo story yako umechapia. Kwa mfano Pablo hakuuawa na wamarekani, aliuawa na askari wa nchi yake, wacolumbia wenyewe. Serikali ilijaribu mara nyingi kumkamata lakini ilikuwa inashindwa kwa kuwa wengi wa maafisa usalama walikuwa kwenye payroll yake, hivyo walikuwa wanaunguza picha na yeye kupata nafasi ya kutoroka. Lile gereza alimowekwa hakulijenga yeye, lilijengwa na serikali kwa makubaliano na sharti la yeye kujitokeza ili wamkamate. Wajenzi walipenyeza vyombo vya mawasiliano kwa siri kwenye hilo gereza na hivyo pamoja na kwamba alikuwa amefungwa, aliendelea kusimamia biashara zake za madawa ya kulevya akiwa kifungoni.

Serikali ya marekani ililalamikia hali hiyo na kuishinikiza serikali ya columbia kumuhamishia Escobar kwenye gereza la kawaida. Kama kawaida, Escobar alipata taarifa za huo mpango na kuamua kutoroka kwenye hilo gereza siku moja kabla ya siku waliyokuwa wamepanga kumuhamisha.

Serikali ilianza jitihada za kumtafuta. Kwa msaada wa technologia ya wamarekani ya kunasa mazungumzo ya simu na kufuatilia eneo simu ilikopigwa, waliweza kujua alikokuwa amejificha. Alikuwa amejificha kwenye nyumba iliyoko eneo moja la walalahoi. Alipojua kwamba nyumba imezingirwa na askari alijaribu kutoroka kupitia kwenye paa ya hiyo nyumba, lakini jamaa wakamuwahi kwa risasi na huo ukawa ndio mwisho wake.

Ukweli huyu jamaa aliitikisa dunia kwa biashara zake za kusafirisha madawa ya kulevya.

Tiba
 
Je ana u ndugu na NAS ESCOBAR?
kuna yule pacha wa kumuziki wa Dogo Ditto anaitwa KOBA, vp ni ndugu ama?
 
kuna mengi sana kuhusu huyu mtu ila mwenye data za upande wa ukatili wake alete tafadhali.
 
Wakuu katikati ya hii mada Kuhusu Pablo namimi Naomba kuuliza........ Hivi tunavyosikia Unga unalipa sana kiasi cha hawa Jamaa kuwa jeuri hata kwa serikali, mfano hapa Tanzania,hizo hela zinatokana na kuwauzia hawa Wapiga debe (mateja) Unga Au kuna kazi nyingine unafanyia tofauti na matumizi haya ya ndugu zangu wanaojidunga?
 
Back
Top Bottom