Huyu ndio Magufuli

Huyu ndio Magufuli

Reuters

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
375
Reaction score
160
HUYU NDIO MAGUFULI:
"Uwajibikaji ndio suluhisho la wazembe, nitajenga utamaduni mpya wa uwajibikaji, kutakuwa hakuna kusameheana, kubebana wala kujuana. Nitaimarisha mfumo mzima wa utumishi wa umma ili kuiwezesha serikali kuwatumikia wananchi lakini pia kurahisisha utoaji adhabu kwa watakaozembea badala ya kulindana na kuunda tume na kamati zisizo na tija"
 
Hivi hakuwa na wasaa wa kumshauri rais???wizara yake nayo ina udhaifu,,rushwa mizani na ujenz wa barabara chini ya kiwango,wahusika aliwafanyaje???mfano ni ujenz wa barabara ya Kilwa ambao hauishi kwa sababu ya kujengwa below standards
 
Ccm ni ile ile hata kwenye wimbo wa kumnadi magufuli kila siku wanatuimbia. Sasa kama ccm ni ile ile hayo mabadiliko mnayosema yatapenya wapi?

Kilichobaki ni Lowasa! Mabadilikooooo. Mabadiliko! Lowasaaaaaaaaaa
 
sasa anatuelezea uzembe na udhaifu wa CCM wakati na yeye mwenyewe alikua katika system. binafsi namuona magufuli anaongea kama mpinzani na anaivua nguo serikali ya CCM
 
Tokea 1977 mpaka 2015 Inatosha. Ni vizuri tuwe na utaratibu wa kuruhusu vyama vyengine kuchukua madaraka kwa njia ya amani.

Katika nchi zinazoitwa za demokrasia( domokrasia) huwezi kupata chama cha siasa kukaa madarakani kwa miongo miwili mfululizo.

Tusilee usultani, ufalme wa vyama.
 
Baada ya miaka 54, hakuna nafasi nyingine ya kudanganya watu kwa maneno ya kutunga kama haya. CCM mlichoshindwa kukifanya kwa miaka 54, mtawezaje kukifanya kwa miaka mitano ijayo????? HATUDANGANYIKI TENA!!!!!! CCM OUT! Hakuna namna nyingine!!!!!!!
 
sasa anatuelezea uzembe na udhaifu wa CCM wakati na yeye mwenyewe alikua katika system. binafsi namuona magufuli anaongea kama mpinzani na anaivua nguo serikali ya CCM

Ahamie tu ukawa kama kashaona mabovu ya ccm
 
Watumishi tumesha tapeliwa sana na selekali ya ccm, tumepanda madaraja mishahara haibadiliki tunazidi kuhesabu miaka tangu tupewe barua za kupandishwa. Kwanini ccm ipewe nafasi tena?
 
HUYU NDIO MAGUFULI:
"Uwajibikaji ndio suluhisho la wazembe,nitajenga utamaduni mpya wa uwajibikaji,kutakuwa hakuna kusamehana,kubebana wala kujuana.Nitaimarisha mfumo mzima wa utumishi wa umma ili kuiwezesha serikali kuwatumikia wananchi lakini pia kurahisisha utoaji adhabu kwa watakaozembea badala ya kulindana na kuunda tume na kamati zisizo na tija"

Mfumo wa "kusameheana, kubebana na kujuana" ndio unaotumika na kuubadilisha maana yake ni kuachana na chama tawala na kujiunga na Ukawa. Kama marais waliopita hawakuweza kufanya hivyo, Magufuli hawezi peke yake kufanya miujiza maana atakuwa amezungukwa na watu waliokwisha faidika na mfumo anaotaka kuubadilisha, ambao pia na yeye amefaidika nao.
 
Anhaaa. Na hyo ndio sifa ya Raisi tunayemtaka. Asiyeonea haya madhaifu hata yake mwenyewe.
sasa anatuelezea uzembe na udhaifu wa CCM wakati na yeye mwenyewe alikua katika system. binafsi namuona magufuli anaongea kama mpinzani na anaivua nguo serikali ya CCM
 
Magufuli ndiye chaguo la wengi sana. Watanzania wanatambua uwezo wa Magufuli.
 
Lazima ccm ife kwanza ndio wananchi wapate mabadiliko wanayoyataka
 
Magufuli ni sawa na mtoto ambaye anataka awapangie sheria baba na mama waliomzaa ndani ya ccm ki2 ambacho hakiwezekani kwa kweli

Hakuna kisichowezekana, hata sisi wana ccm twataka mabadiliko tena yetu yanaanzia ndani ya chama chetu hadi utawala wa nchi . Change is uniform all over the world and it is not related to one party.
 
Magufuli sio mtu wa kufananishwa na mafisadi, historia yake inampatia heshima kubwa sana ndani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom