Huyu ndio Kikwete bwana!

simba songea

JF-Expert Member
Feb 8, 2016
1,498
1,214
Asallaam alleykum na tumsifu Yesu kristo, kama kinavyojieleza kichwa cha habari hapo juu;

watu wengi wamekuwa wakimponda rais mstaafu jakaya mrisho kikwete wakisema eti amepiga pesa nyingi na wengine wakisema alikuwa mzee wa madili.

Watu tunamsifu Rais magufuli na kumsahau kikwete, ndiye aliyempigania huyu tingatinga kuingia ikulu. Kipindi magufuli akiwa waziri wa miundombinu tujiulize alikuwa anatoa pesa wapi za kujenga barabara kama sio kwa kikwete.

Kikwete ndo aliyepigana kutafuta pesa za kumpa waziri wake li ajenge barabara. Alisababisha hata idadi ya ikulu iwe ndogo aliangaika nchi za ughaibuni hata kukopa ili ampe waziri wa ujenzi wakati huo magufuri ili akajenge barabara. Hii ilipelekea kikwete kusimangwa na watu kwamba anazurura ovyo hatulii chini kwake. lakin tujiulize asingeangaika hizo pesa angepata wapi? hizo barabara zingetoka wapi? pengine hata magufuli asingeshinda urais maana angekuwa hamna alichofanya kipindi cha uwaziri wake.

tukumbuke kikwete ndio aliyempigania huyu rais wa sasa magufuli, mzee kikwete alikuwa halali usiku kucha akifanya mipango ya magufuli ashinde, maana uchaguzi uliopita ulikuwa na ushindani mkubwa na ikapelekea hata baadhi ya viongozi wa chama wa ccm kuhama wakiwemo mawaziri wastaafu hata wabunge pia walihama.

Rais mstaafu akuogopa wala kutishwa kwa kuhama hao viongozi yeye alisimamia msimamo wake wa chama kwanza mengine baadae yaani magufuli ashinde kwanza afu mengine baadae. Watu walianza kumsanifu kikwete wakisema chama sasa kinamfia mikononi mwake maanahaiwezekani mawaziri wakuu wastaafu na wabunge wakihame chama.
 
Fala kweli wewe,huyu asiyezurula pesa anatoa wapi???laiti ingelikuwa kuzurula kwa jk ndo kunailetea nchi hela nafikiri tanzania ilitakiwa kusiwe na shida yoyote maana hyo mkwele kazurula kuliko maelezo
 
Umeandika kama una wasifu mpya wa kikwete ambao labda wana jukwaa walikuwa hawana taarifa!
Ahsante kwa kuelezea hali ilivyo kuwa kabla na wakati wa uchaguzi 2015!
kukumbushana sio mbaya, mara moja moja
 
kikwete ni jembe.... asante sana jakaya kikwete popote ulipo...

watanzania tunakupenda sana... wewe ni rais bora kuliko wote tuliowahi kupata ukiondoa nyerere...

bila wewe magufuli asingepata nafasi hiyo...
 
kikwete ni jembe.... asante sana jakaya kikwete popote ulipo...

watanzania tunakupenda sana... wewe ni rais bora kuliko wote tuliowahi kupata ukiondoa nyerere...

bila wewe magufuli asingepata nafasi hiyo...
kweli kabisa
 
Back
Top Bottom