Huyu ndio Godwin Aswile (Scania)

Godwin Aswile Scania alisifika sana Kwa Mapafu ya Kurusha Mpira,
Anawwza Kurusha Mpira Toka Katikati ya Uwanja Hadi Golini Kwa Timu Pinzani na Mpira Ukiwa juu juu !
 
Godwin Aswile na Thomas Kipese walichezea Simba msimu wa 1993 baada kutimuliwa Yanga kwa tuhuma za rushwa.

Hata hivyo, wakiwa Simba mwaka huo walichezea mechi za kimataifa pekee.

Maana wakati wanatua Simba tayari dirisha la usajiri kwa ligi ya ndani lilishafungwa.

Aswile na Kipese walitoa mchango mkubwa kwa mafanikio ya Simba kimataifa mwaka huo.

Mwaka 1993 ndiyo mwaka ambao Simba ilifika fainali Kombe la CAF ikiwa na kikosi kilichojaa vipaji akiwemo Godwin Aswile Mlimba.
 
View attachment 2010227

Godwin Aswile Mulimba
Beki wa kati aliyepata sifa kubwa kutokana na uchezaji wake wa kutumia nguvu na akili kwa pamoja huku akiziba vizuri makosa ya mabeki wake wapembeni pindi inapotokea wamepitwa katika kipindi chake cha uchezaji aliweza kuisaidia Yanga ubingwa wa Tanzania mwaka 1993

ZAMA ZAKE AKICHEZEA YANGA SC​

BEKI wa Yanga SC, Godwin Aswile Mulimba ‘Scania’ (kushoto) akiingiza mguu kuondosha mpira kwenye himaya ya mchezaji wa Kurugenzi Dodoma katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi Kuu) Tanzania Bara mwaka 1988 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-1.

Tumewamiss sana mabeki makatili kama hawa!!mabeki wetu siku hizi nyoronyoro sana!!Godwin Aswile Scaniaa
 
Godwin Aswile na Thomas Kipese walichezea Simba msimu wa 1993 baada kutimuliwa Yanga kwa tuhuma za rushwa.

Hata hivyo, wakiwa Simba mwaka huo walichezea mechi za kimataifa pekee.

Maana wakati wanatua Simba tayari dirisha la usajiri kwa ligi ya ndani lilishafungwa.

Aswile na Kipese walitoa mchango mkubwa kwa mafanikio ya Simba kimataifa mwaka huo.

Mwaka 1993 ndiyo mwaka ambao Simba ilifika fainali Kombe la CAF ikiwa na kikosi kilichojaa vipaji akiwemo Godwin Aswile Mlimba.
Halafu kulikuwa na beki wa kushoto wa Simba anaitwa Michael Kidilu kutoka Igoma (Dar es Salaam Ndogo) kwa walima viazi chips alikuwa wamoto ni balaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom