Huyu ndio Che Guevara wa Tanzania

Huyu ndio Che Guevara wa Tanzania

Kwanza napenda kuwapa salam ndugu, jamaa na marafiki wote mliopo humu. Ndugu zangu kabla ya kuanza na mada yangu ningependa kwanza nirejelee ule msemo aliowahi kuusema mzee wetu, baba yetu, babu yetu, au raisi wetu mstaafu mh Ally .H. Mwinyi kuwa "kila zama huja na kitabu chake" akiwa na maana kuwa kila raisi au serikali mpya inapoingia madarakani huja na mikakati yake ya uongozi.

Tumeweza kuona kuwa kila uongozi au kiongozi kama tulivyo binadam wengine, huwa na mazuri na mabaya yake. Kwahiyo hapa ningependa kuzungumzia yale mabaya yaliyofanywa na viongozi mbali mbali dhidi ya wapinzani wao.

Tukianza na utawala wa hayati Mkapa ambao ulikutana na upinzani mkali kutoka kwa aliekuwa mwenyekiti wa NCCR na baadae TLP mh Augustine.L. Mrema tuliona jinsi serikali ilivyopambana nae kwa njia na mbinu mbali mbali mpk kufikia hatua ya kumdhibiti na kumpoteza kabisa katika ulimwengu wa siasa bila kuleta madhara makubwa kwa nchi.

Baada ya Mrema kudhibitiwa akaibuka mpinzani mungine mh prof Lipumba, ambae kutokana na elimu yake watu wengi walihisi kuwa angeweza kuitumia elimu yake kumsumbua kweli kweli Rais Mkapa na pengine kushinda uchaguzi wa mwaka 2000 au 2005 na kuchukua dola, prof huyu akishirikiana na mzoefu wa mapambano ya kisiasa hayati Maalim Seifu, waliweza kui challenge serikali kwa kufanya maandamano mbali mbali na kuikosoa Serikali kwa namna mbali mbali, lkn mwisho wa siku sisi wote tuliona jinsi prof huyu alivyoangukia pua dakika za mwisho za utawala wa raisi Mkapa na mpk leo hana mbele wala nyuma, kifupi anazurula tu kule buguruni.

Baada ya Mkapa kumaliza uongozi wake, akaingia kiongozi mungine ambae alikuwa na aina tofauti ya uongozi. Huyu alikuwa ni zaidi ya Mkapa kwani aliweza kutumia mbinu za kisiasa na kisayansi kuwadhibiti wapinzani wake.

Ndipo hapo alipoibuka mpambanaji hatari, jasiri, mwenye ushawishi na maarifa ya mapambano. Huyu si mungine ni mh Dr Slaa au unaweza kumwita Che guevara wa Tanzania. Jamaa alipambana katika awamu zote mbili za raisi Kikwete na kukumbana na upinzani mkubwa kutoka kwenye serikali. Inasemekana jamaa alikuwa na moyo wa chuma kwani alikuwa tayari kupambana katika mazingira yoyote bila kujali kuwa anaweza kuumia, kufungwa au kupoteza maisha.

Jamaa aliweza kuongoza maandamano na mapambano mbali mbali tena yeye mwenyew akiwa front line huku mwenyekiti wake na viongozi wengine wakijificha majumbani mwao kuhofia usalama wao, na wale wachache waliojitokeza kumuunga mkono waliishia kujificha nyuma ya mgongo wake ili hali ikiwa mbaya wawe wa kwanza kuingia mitini.

Jamaa hakuwa na tabia ya kupanga maandamano halafu yeye ajifiche ndan kwakwe kama ilivyo kwa viongozi wengine, na hii ndo ilipelekea watu kujitokeza kwa wingi kila anapotangaza maandamano. Inasemekana baada ya raisi Kikwete kuona misimamo ya huyu mzee ni hatari kwa mustakabali wa uhai wa chama chake, ndio akaja na mbinu iliyosaidia chama hicho kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 na kuendelea kushika dola mpk leo.

Maana Rais aligundua kwamba endapo che guevara angegombea na kumletea unyonge kama ule waliouleta mwaka 2015 na 2020 basi kungechimbika kweli kweli. Sasa akapangwa waziri mkuu mstaafu fulani ili akatibue mipango na kuisambaratisha ngome. Na kweli ngome imesambaratika, waliojifanya kuvaa viatu vyake ndani ya chama wamejikuta haviwatoshi hata kidogo.

Ni muda sasa wa chama kuangalia namna ya kufanya negotiation na Che guevara ili aje arudishe amsha amsha ndan ya chama na nchi nzima kwa ujumla.
Zote hizi ni "reference" tu. Zilipendwa hizo.
 
Ww huna ndugu aliyeoza?????

Mwenyewe utaoza kwa hiyo tutakufa wote kifo s furaha wote tutafuata
Ajui ushawishi wa magufuli ni level ya mitume watu serikalini wanaangaika ili kuondoa legacy ya magufuli ila wapi wapinzani pia wanaangaika kuondoa wapi ndiyo maana nikasema
USHAWISHI WA MAGUFULI ULIKUWA LEVEL YA MITUME HATA WAKIFA KILE WALICHO KISIMAMISHA HAKIFI
Kwa miaka mitano tu cheki LEGACY ALIYO ACHA NYOYONI MWA WATANZANIA HADI MAFISADI WANA SHANGAA WANASEMA MAGU KAFA SASA HIKI NI NINI TENA au mzimu wa magufuli!!!!!!!!
 
Mbona kakimbia mapambano mapema sana!!!
Kahamisha uwanja wa mapambano tu. Anatema cheche kama kazi. Dola inahangaika kufuatilia mitandao na kumjibu.

Huyo unayemuita Che Guevara, siku hizi anaimba mapambio ya sifa na utukufu kwa mahasimu wake waliomlaza chini. Che hakuwa hivyo; alizipiga hadi kifo.
 
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Kama jamaa alikubali kupigishwa deki barabara na fisadi kuu kwa sababu ya masilahi ya tumbo lake, unategemea anaweza kuwa na mbinu gani za kuwadhibiti waliomtuma fisadi aje ampigishe deki barabarani?
 
Vya kale ni dhahabu... Che Guevara wa Tanzania alionesha njia ambayo wengine ili wafanikiwe wanatakiwa waifuate
Che Guavara uchwara....huyu ni mchaga tu kama wengine ...wengi wao walafi na tamaa zimewajaa....yaani sipati picha umpe nchi mchaga nafikiri watauza mpaka bahari,ziwa victoria ,SGR,bwawa la Nyerere nk
 
Hayo mawazo umeyakuta watu wanaongea maishani.Ukiambiwa utoe ushahidi uso mawaa huwa mnaanza kuwa wakali.
 
Che Guavara uchwara....huyu ni mchaga tu kama wengine ...wengi wao walafi na tamaa zimewajaa....yaani sipati picha umpe nchi mchaga nafikiri watauza mpaka bahari,ziwa victoria ,SGR,bwawa la Nyerere nk
Mkuu haya uliyoandika hapa hayana ukweli wowote, ni propaganda tu za watu. Nafikiri ifike kipindi tuwe tunawahukumu watu kutokana na tabia zao na sio makabila yao. Hata hivyo nashukuru kwa kuchangia mada.
 
Ni muda sasa wa chama kuangalia namna ya kufanya negotiation na Che guevara ili aje arudishe amsha amsha ndan ya chama na nchi nzima kwa ujumla.
Mkuu Mr Dudumizi , kwanza asante sana na hongera sana kwa mada hii fikirishi. Pili ni kweli mtajwa hapo mwanzo alikuwa kama Chee, tofauti ni moja tuu, Chee hakuwahi kufika bei, mtajwa alifika bei.

Mwanzo alikuwa CCM, alipohamia Upinzani, hakurudisha kadi ya CCM !.

Na ule mkutano wake wa Serena kutangaza kujitoa na kudai anashindia mihogo, unajua uligharmiwa na nani?.

Na kama ulivyosema kila zama na zama zake, huyu Che wako, hata asinge fika bei sasa ni Mzee, kajizeekea hivyo hawezi tena. Mwache ajistaafie kwa amani, ajilie pensheni yake taratibu.

P.
 
Asante mkuu Pascal Mayalla kwa mchango wako. Lkn pamoja na yote uliyoandika hapa, mimi nafikiri wapinzani bado wana mengi ya kujifunza kupitia kwake, hapa nazungumzia yale mazuri ambayo yalisaidia kwa namna moja au nyingine kukijenga chama nk.
 
Back
Top Bottom