Huyu ndio Che Guevara wa Tanzania

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Kwanza napenda kuwapa salam ndugu, jamaa na marafiki wote mliopo humu. Ndugu zangu kabla ya kuanza na mada yangu ningependa kwanza nirejelee ule msemo aliowahi kuusema mzee wetu, baba yetu, babu yetu, au raisi wetu mstaafu mh Ally .H. Mwinyi kuwa "kila zama huja na kitabu chake" akiwa na maana kuwa kila raisi au serikali mpya inapoingia madarakani huja na mikakati yake ya uongozi.

Tumeweza kuona kuwa kila uongozi au kiongozi kama tulivyo binadam wengine, huwa na mazuri na mabaya yake. Kwahiyo hapa ningependa kuzungumzia yale mabaya yaliyofanywa na viongozi mbali mbali dhidi ya wapinzani wao.

Tukianza na utawala wa hayati Mkapa ambao ulikutana na upinzani mkali kutoka kwa aliekuwa mwenyekiti wa NCCR na baadae TLP mh Augustine.L. Mrema tuliona jinsi serikali ilivyopambana nae kwa njia na mbinu mbali mbali mpk kufikia hatua ya kumdhibiti na kumpoteza kabisa katika ulimwengu wa siasa bila kuleta madhara makubwa kwa nchi.

Baada ya Mrema kudhibitiwa akaibuka mpinzani mungine mh prof Lipumba, ambae kutokana na elimu yake watu wengi walihisi kuwa angeweza kuitumia elimu yake kumsumbua kweli kweli Rais Mkapa na pengine kushinda uchaguzi wa mwaka 2000 au 2005 na kuchukua dola, prof huyu akishirikiana na mzoefu wa mapambano ya kisiasa hayati Maalim Seifu, waliweza kui challenge serikali kwa kufanya maandamano mbali mbali na kuikosoa Serikali kwa namna mbali mbali, lkn mwisho wa siku sisi wote tuliona jinsi prof huyu alivyoangukia pua dakika za mwisho za utawala wa raisi Mkapa na mpk leo hana mbele wala nyuma, kifupi anazurula tu kule buguruni.

Baada ya Mkapa kumaliza uongozi wake, akaingia kiongozi mungine ambae alikuwa na aina tofauti ya uongozi. Huyu alikuwa ni zaidi ya Mkapa kwani aliweza kutumia mbinu za kisiasa na kisayansi kuwadhibiti wapinzani wake.

Ndipo hapo alipoibuka mpambanaji hatari, jasiri, mwenye ushawishi na maarifa ya mapambano. Huyu si mungine ni mh Dr Slaa au unaweza kumwita Che guevara wa Tanzania. Jamaa alipambana katika awamu zote mbili za raisi Kikwete na kukumbana na upinzani mkubwa kutoka kwenye serikali. Inasemekana jamaa alikuwa na moyo wa chuma kwani alikuwa tayari kupambana katika mazingira yoyote bila kujali kuwa anaweza kuumia, kufungwa au kupoteza maisha.

Jamaa aliweza kuongoza maandamano na mapambano mbali mbali tena yeye mwenyew akiwa front line huku mwenyekiti wake na viongozi wengine wakijificha majumbani mwao kuhofia usalama wao, na wale wachache waliojitokeza kumuunga mkono waliishia kujificha nyuma ya mgongo wake ili hali ikiwa mbaya wawe wa kwanza kuingia mitini.

Jamaa hakuwa na tabia ya kupanga maandamano halafu yeye ajifiche ndan kwakwe kama ilivyo kwa viongozi wengine, na hii ndo ilipelekea watu kujitokeza kwa wingi kila anapotangaza maandamano. Inasemekana baada ya raisi Kikwete kuona misimamo ya huyu mzee ni hatari kwa mustakabali wa uhai wa chama chake, ndio akaja na mbinu iliyosaidia chama hicho kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 na kuendelea kushika dola mpk leo.

Maana Rais aligundua kwamba endapo che guevara angegombea na kumletea unyonge kama ule waliouleta mwaka 2015 na 2020 basi kungechimbika kweli kweli. Sasa akapangwa waziri mkuu mstaafu fulani ili akatibue mipango na kuisambaratisha ngome. Na kweli ngome imesambaratika, waliojifanya kuvaa viatu vyake ndani ya chama wamejikuta haviwatoshi hata kidogo.

Ni muda sasa wa chama kuangalia namna ya kufanya negotiation na Che guevara ili aje arudishe amsha amsha ndan ya chama na nchi nzima kwa ujumla.
 
Nilitarajia ungemalizia kwa jinsi alivyopambana na alivyomalizia mapambano yake. Ni kama anaendelea!
 
Ww huna ndugu aliyeoza?

Mwenyewe utaoza kwa hiyo tutakufa wote kifo s furaha wote tutafuata
Huyo baba tu sina kwanini nifurahie madhila ya mtu?ila hiko chuma kilikuwa chenyewe kinayafurahia matatizo ya watu (refer tukio la Lissu kupigwa risasi), hata humu mpo watu mnashangilia kinachomkuta Mbowe.

Kwenye haki ya wengi kama wewe ukaonekana kikwazo na ukapata tatizo hata kama hilo tatizo litakuja kwa kila mmoja wetu kwa wakati wake mimi nitafurahi.
 
Huyo baba tu sina kwanini nifurahie madhila ya mtu?ila hiko chuma kilikuwa chenyewe kinayafurahia matatizo ya watu (refer tukio la Lissu kupigwa risasi),hata humu mpo watu mnashangilia kinachomkuta Mbowe...
Wewe kenge acha kujikuta Mungu Mt ww hujawahi furahishwa na chochote ambacho ni kibaya kwa wengine?
 
Wewe kenge acha kujikuta Mungu Mt ww hujawahi furahishwa na chochote ambacho ni kibaya kwa wengine??

Ume-panic kidogo tu matusi yanakutoka!

CCM ndo mnajikuta miungu watu,sasa unataka vipi mimi nifurahishwe na kitu kibaya kwenu (dai la katiba mpya) hali ya kuwa hamtaki kufurahia kizuri ninachokitaka mimi?

Mpaka hapo nani ni Mungu mtu?
 
Nilitarajia ungemalizia kwa jinsi alivyopambana na alivyomalizia mapambano yake. Ni kama anaendelea!
Ameacha mapambano mwaka 2015 baada ya kusalitiwa na aliokuwa akiwapambania wakiongozwa na mwenyekiti wao.
 
Mr Dudumizi shukrani kwa kutupa historia.

Natupia clip inayoonesha maisha ya 'Che' Freeman Mbowe ikionesha kwa kifupi mapambano yake ya kudai demokrasia na uhuru wa waTanzania ndani ya katiba mpya ya vyama vingi vya siasa.

 
Back
Top Bottom