Huyu ndie Rais watanzania tunaemuhitaji

Huyu ndie Rais watanzania tunaemuhitaji

Kuna kijana alikuwa anachelewa kuoa Kwa kuwa alikuwa anatafuta Mke Mwenye Sifa zifuatazo

1) Mrefu
2) Mweupe
3) Mwenye figure nzuri
4) Mwenye sura nzuri
5) Mwenye ngozi nzuri
5) Mwenye Elimu angalau ya Chuo kikuu
6) Mwenye kazi nzuri
7) Mwenye heshma Kwa Mumewe
8) Mwenye kuheshimu Ndugu wa Mumewe
9) Mkarimu Na Mcheshi
10) asie Na tamaa

Mie kimoyo Moyo nikawa najisemea Mke Mwenye Sifa hizo atampata Yaumul qiyaama hapa Duniani ajiandae kufa Bachelor ( Mseja)
Kuzikataa fikra za mtu ambaye hakupunguzii kimo chako ni ujinga.Haya, sasa ulimshauri nini? Au uliishia kukariri vijistari vya vitabu na kuleta hapa?
 
Mithali 28:16 Mtawala asiye na akili ni mdhalimu ,mkatili....sifa za Juma Pombe Maharage na Bashite...jumapili njema
 
Si mwingine bali ni yule atakaefanya haya:-
1.Atakaetupa katiba mpya
2.Atakaerudisha Bunge live
3.Atakaerudisha fao la kujito
4.Atakaefuta makato ya asimia 15 kwa ajili ya Bodi ya Mikopo
5.Atakaeshusha PAYE
6.Atakaefuta vigezo vya utoaji wa mikopo kwa kuangalia aina ya kozi,ufaulu au familia anayotoka muombaji
7.Atakaetunga sheria ya kuongeza mishahara ya watumishi kila mwaka wa fedha mbali na hii annual increment kwa kuweka walau minimum ya percent ya kuongeza kwa kima chini cha mshahara.
8.Atakaetoa kipaumbele kwenye kilimo
9.Atakaekuja na sera ya kuanzisha kilimo cha umwagiliaji.
10.Ataekuja na mpango wa kutoa kifuta machozi kwa watumishi waliofukuzwa kwa kuwa na vyeti feki maana wana mchango wa kwa Taifa hili.
11.Atakaekuja na mpango wa kutoa kifuta machozi kwa waathirika wa bomoabomoa waliovunjiwa nyumba zao kimakosa
12.Atakaekuja na mpango maalumu wa kibajeti wa kuondoa shule za nyasi na tope maeneo yote ya vijijjini.
13.Atakaeanzisha mfuko wa maji vijijjini.
14.Atakaesitisha ununuzi wa mashangingi kwa ajili ya viongozi
15.Atakaeiondoa serikali kwenye uendeshaji na umiliki wa ATCL
16.Atakaetengeza fursa za ajira serikalini.
17.Atakekuwa na sera rafiki kwa ustawi wa sekta binafsi.
18.Atakaerudisha utaratibu wa serikali kuendeshwa kwa uwazi na kuufanya kuwa ni wa kisheria.
19.Atakaebadili sheria kuiwezesha TAKUKURU kushitaki bila kusubiri kibali cha DPP na kumfanya mkurugenzi wa TAKUKURU asiwe mteule wa Raisi.
20.Atakaebadili sheria na kumuwezeshaa CAG kumshitaki mahakamani CE wa taasisi yoyote ya serikal atakaebainika kutumia vibaya fedha za umma.
21.Atakaekuja na sheria itakayoiwezesha ofisi ya CAG kuwa na vyanzo vyake mahususi vya mapato bila kutegemea bajeti ya serikali kama ilvyo EWURA, TCAA,n.k ili aweza kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
22.Atakaebadili sheria ya Jeshi la Polisi lisitambulike kama Jeshi bali kiwe ni chombo cha kutoa service kwa wananchi.
23.Raisi atakaekuja na sheria au mpango wa kufuta sitting allowance za wabunge.
24.Raisi atakaekuja na sheria inayotaka mikataba yote ipate ridhaa ya Bunge.
25.Raisi atakaekuja na sheria inayozuia serikali kukopa bila kushirkisha Bunge unless kumetokea dharura kama Taifa kuingia vitani,n.k
26.Raisi atakaeshirikisha wadau wa ellimu nchi nzima ambao watatunga sera ya elimu na serikali nayo kutengeneza sheria itakayozuia kila kiongozi kuja na sera yake ya elimu.

Kiongozi wa aina hii ndio atakaeweza kuibadili Tanzania na maisha ya watanzania kwa ujumla iwapo atapata wasaidi wazuri na yeye mwenyewe akawa commited.

Hakuna hata moja lililo gumu hapo zaidi ya uzalendo,nia na utayari wa kiongozi muhusika tu..
Wewe ndiye, wakati ukifika liamshe dude
 
Raisi hatungi sheria
Sheria ikiwa nzuri au mbaya nani huwa analaumiwa?Miswaada huandaliwa serikalini na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kwa baraka za Raisi na cabinet yake kisha hupelekwa Bungeni kujadiliwa na miswaada mingi hupita Bungeni kama ilivyo.

Najua nachokiongea hapa.
 
Kuna msemo wetu maarufu "mwenye shibe hamjui mwenye njaa" ambapo mambo mengi yaliyoorodheshwa hayamgusi kiongozi wa juu kabisa. Ni vizuri kujua utungaji wa sheria unatumia vigezo gani au inputs kutoka wapi.
Bado nasema taifa linahitaji kuwa na ajenda kadhaa ambazo hazitategemea ni nani ndiye anayeongoza.
 
Back
Top Bottom