Huyu ndie Rais watanzania tunaemuhitaji

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,998
144,329
Si mwingine bali ni yule atakaefanya haya:-
1.Atakaetupa katiba mpya
2.Atakaerudisha Bunge live
3.Atakaerudisha fao la kujito
4.Atakaefuta makato ya asimia 15 kwa ajili ya Bodi ya Mikopo
5.Atakaeshusha PAYE
6.Atakaefuta vigezo vya utoaji wa mikopo kwa kuangalia aina ya kozi,ufaulu au familia anayotoka muombaji
7.Atakaetunga sheria ya kuongeza mishahara ya watumishi kila mwaka wa fedha mbali na hii annual increment kwa kuweka walau minimum percentage ya nyongeza kwa kima chini cha mshahara.
8.Atakaetoa kipaumbele kwenye kilimo
9.Atakaekuja na sera ya kuanzisha kilimo cha umwagiliaji.
10.Ataekuja na mpango wa kutoa kifuta machozi kwa watumishi waliofukuzwa kwa kuwa na vyeti feki maana wana mchango wa kwa Taifa hili.
11.Atakaekuja na mpango wa kutoa kifuta machozi kwa waathirika wa bomoabomoa waliovunjiwa nyumba zao kimakosa
12.Atakaekuja na mpango maalumu wa kibajeti wa kuondoa shule za nyasi na tope maeneo yote ya vijijjini.
13.Atakaeanzisha mfuko wa maji vijijjini.
14.Atakaesitisha ununuzi wa mashangingi kwa ajili ya viongozi
15.Atakaeiondoa serikali kwenye uendeshaji na umiliki wa ATCL
16.Atakaetengeza fursa za ajira serikalini.
17.Atakekuwa na sera rafiki kwa ustawi wa sekta binafsi.
18.Atakaerudisha utaratibu wa serikali kuendeshwa kwa uwazi na kuufanya kuwa ni wa kisheria.
19.Atakaebadili sheria kuiwezesha TAKUKURU kushitaki bila kusubiri kibali cha DPP na kumfanya mkurugenzi wa TAKUKURU asiwe mteule wa Raisi.
20.Atakaebadili sheria na kumuwezeshaa CAG kumshitaki mahakamani CEO wa taasisi yoyote ya serikal atakaebainika kutumia vibaya fedha za umma.
21.Atakaekuja na sheria itakayoiwezesha ofisi ya CAG kuwa na vyanzo vyake mahususi vya mapato bila kutegemea bajeti ya serikali kama ilvyo EWURA, TCAA,n.k ili aweza kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
22.Atakaebadili sheria ya Jeshi la Polisi lisitambulike kama Jeshi bali kiwe ni chombo cha kutoa service kwa wananchi.
23.Raisi atakaekuja na sheria au mpango wa kufuta sitting allowance za wabunge.
24.Raisi atakaekuja na sheria inayotaka mikataba yote ipate ridhaa ya Bunge.
25.Raisi atakaekuja na sheria inayozuia serikali kukopa bila kushirkisha Bunge unless kumetokea dharura kama Taifa kuingia vitani,n.k
26.Raisi atakaeshirikisha wadau wa ellimu nchi nzima ambao watatunga sera ya elimu na serikali nayo kutengeneza sheria itakayozuia kila kiongozi kuja na sera yake ya elimu.

Kiongozi wa aina hii ndio atakaeweza kuibadili Tanzania na maisha ya watanzania kwa ujumla iwapo atapata wasaidi wazuri na yeye mwenyewe akawa commited.

Hakuna hata moja lililo gumu hapo zaidi ya uzalendo,nia na utayari wa kiongozi muhusika tu..
 
Kuna kijana alikuwa anachelewa kuoa Kwa kuwa alikuwa anatafuta Mke Mwenye Sifa zifuatazo

1) Mrefu
2) Mweupe
3) Mwenye figure nzuri
4) Mwenye sura nzuri
5) Mwenye ngozi nzuri
5) Mwenye Elimu angalau ya Chuo kikuu
6) Mwenye kazi nzuri
7) Mwenye heshma Kwa Mumewe
8) Mwenye kuheshimu Ndugu wa Mumewe
9) Mkarimu Na Mcheshi
10) asie Na tamaa

Mie kimoyo Moyo nikawa najisemea Mke Mwenye Sifa hizo atampata Yaumul qiyaama hapa Duniani ajiandae kufa Bachelor ( Mseja)
 
Naongezea Mkuu..
Atakaye Ongoza Nchi Kwa Kufuata Katiba aliyo Apa na Sheria tulizojiwekea Kama Nchi.
 
19B64A99-3BD7-462B-A130-0494675AB6F8.jpeg
Mbona unazunguka zunguka ,sema tu MTU wa design hiyo ni mbowe
 
Salary Slip unaota,hata chadema wakishika dola hawatatunga sheria ya kupandisha mshahara kila mwaka
 
1 Bunge live tuone vituko vya wabunge Tz itakua wwe ya bure
.


mkuu kwa sifa unazozitaka inaonekana umetumbuliwa jipu mahala..
umeamua kuwa mkereketwa tu
 
Back
Top Bottom