"Huyu nae ni walewale tu"

"Huyu nae ni walewale tu"

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Inawezekana wakati huo,inaweza kuwa imepita hata miaka,wakati huyo mumeo alipokutamkia kwa mara ya kwanza neno nakupenda uliwaza hivyo
'
Lakini leo mkiwa kwenye ndoa au mahusiano imara au mkipanga kufunga ndoa huenda umesahau,lakini leo nakukumbusha siku hiyo,unajisikiaje?
'
Vipi ulipokua unamzungusha?Unajionaje?Hebu kumbuka vile ulivyokua unataka kupishana na bahati,unatamani hata ujiadhibu?
'
Uliongozwa na mazoea kuwa wanaume ni waongo,huyo jamaa amekukosoa au siyo?
'
WALIOTENDWA
'
Unaikumbukaje siku jamaa alipokutamkia nakupenda?Ulijipa moyo kuwa aah huyu anaweza kuwa tofautiee,matokeo yamekua kinyume
'
Unajilaumu?Pole,
'
Unaweza kuchukia neno hilo lakini ipo siku utakuwa kwenye kundi la kwanza
'
Usiseme "huyu nae ni walewale",toa nafasi!
 
::
Moyo uliojeruhiwa,
Una hadhari kubwa,
Unahitaji kutibiwa,
Si kwa maneno elewa,
Bali matendo atendayo .
=
 
hakuna haja ya kujilaumu coz tunajua ya sasa tu ila ya mbele hatuyajui!
 
::
Moyo uliojeruhiwa,
Una hadhari kubwa,
Unahitaji kutibiwa,
Si kwa maneno elewa,
Bali matendo atendayo .
=

Najua namna ulivyotendwa,ila nadhani mimi ni zaidi yako,wanaume hatupaswi kulialia,dawa yao ni kuwatafuna na kutupa kule!
 
Najua namna ulivyotendwa,ila nadhani mimi ni zaidi yako,wanaume hatupaswi kulialia,dawa yao ni kuwatafuna na kutupa kule!

::
Eiyer hapa sio kulia,
Kutendwa ni asilia,
Ni funzo la kujivunia,
Litakulinda shikilia,
Eiyer nakupa mia,
Na huyu kama yule pia,
Tofauti ni wakati na Matendo.
=
 
::
Eiyer hapa sio kulia,
Kutendwa ni asilia,
Ni funzo la kujivunia,
Litakulinda shikilia,
Eiyer nakupa mia,
Na huyu kama yule pia,
Tofauti ni wakati na Matendo.
=

Bingo!!!!!!!!!!!!!
 
Sa bro ndo nin sah kurudshana nyuma,wewee napiga m2 chn hapa ninaona dalil za kuchezea tena
 
Back
Top Bottom