Huyu mzee ananitakia mema kweli?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
21,033
64,844
Hivi jamani huyu baba mkwe mtarajiwa unampelekea Mahari anakataa anasema binti yake hauzwi, wewe andaa harusi tu.
Huyu Mchagga ananitakia mema Mimi na binti take kweli?

Hivi kwanini ukatae Mahari?
Mhhh huyu mzee kweli ana nia njema?
Au binti yake ni matatizo hadi akatae mahari?
Siku huyu binti si anaweza anasema kwanza wewe hukunitolea Mahari niache niende kwetu?

Kuna maswali ukiyafikiria mweeeeh!
Jamani wadada hivi wewe ulipotolewa Mahari ulijisikiaje?

Tena Mahari ilipokuwa kubwa au ndogo moyoni ilikuwaje?

Tusaidiane tu maana hakuna namna!!!!!
 
Ulipeleka mahari bila kutajiwa?
Unajua taratibu za ndoa?unaanza kuposa halafu unatajiwa mahari.
 
Hivi jamani huyu baba mkwe mtarajiwa unampelekea Mali anakataa anasema binti yake hauzwi, wewe andaa harusi tu.
Huyu Mchagga ananitakia mema Mimi na binti take kweli?

Hivi kwanini ukatae Mali?
Mhhh huyu mzee kweli ana nia njema?
Au binti yake ni matatizo hadi akatae mali?
Siku huyu binti si anaweza anasema kwanza wewe hukunitolea Mali niache niende kwetu?

Kuna maswali ukiyafikiria mweeeeh!
Jamani wadada hivi wewe ulipotolewa Mali ulijisikiaje?

Tena Mali ilipokuwa kubwa au ndogo moyoni ilikuwaje?

Tusaidiane tu maana hakuna namna!!!!!

Mali ndio nini ndugu??..inawezekana hamkuelewana lugha maana kuandika tu ndio hivi je kuongea unaongeaje??.. umerudia kuandika MALI mara kadhaa hii inaonyesha hata ukitakacho hukijui..jipange
 
mpelekee mali kwa mtindo wa zawadi, angalia anapenda nn then mpelekee, ukubwa wa zawadi uendane na thamani ya hela uliyotaka kumpa kama mahali, wakati mwingine kama family ina kiuwezo wanaweza kupotezea tu hiyo mambo japo kiutaratibu wa nyumbani ni kama mzee amezingua, hebu jaribu pia kuongea na mama mkwe huenda ye anatamani taratibu zote zifatwe
 
Mahali si unatoa baada ya kutajiwa kiasi gani au utoe kitu gani sasa wewe kwanini ulipeka bila kuambiwa upeleke nin
Makubaliano na wajomba, mzee anasema hiyo hela nimepanga itumiwe kwenye harusi. Sasa hapo ndipo sielewi kwa nini hiyo Mali asipokee tu?
Kwani kuna ugumu gani?
 
Mali ndio nini ndugu??..inawezekana hamkuelewana lugha maana kuandika tu ndio hivi je kuongea unaongeaje??.. umerudia kuandika MALI mara kadhaa hii inaonyesha hata ukitakacho hukijui..jipange
Wewe hii simu ina edit keyboard sasa inaandika mali baada ya mahari sorry typing error
 
Mali??? Or mahari??? Jiamini tuu braza kama unayosema sio chai.....

Hivi utaratibu wa kutoa mahari ndio hivi!!! unajibebea tu unapeleka kabla hata ya posa alafu ikikubaliwa ndio unapangiwa mahari! au mimi ndio sijui.
 
Mali??? Or mahari??? Jiamini tuu braza kama unayosema sio chai.....

Ulipeleka mahari bila kutajiwa?
Unajua taratibu za ndoa?unaanza kuposa halafu unatajiwa mahari.
Bwana wewe mjomba kapanga mahari au siyo?
Sasa tunampa anasema itumike kwenye mambo ya harusi.
Wewe unaona pana nini hapa kama siyo hitirafu ya kifundi?
 
Hivi utaratibu wa kutoa mahari ndio hivi!!! unajibebea tu unapeleka kabla hata ya posa alafu ikikubaliwa ndio unapangiwa mahari! au mimi ndio sijui.
Jamani utaratibu wote tayari,
Sasa tunapeleka hicho kiasi ambacho kimepangwa anasema kitumike tu kwenye harusi.
Wewe unaona hii ni kawaida kweli?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom