Huyu mwanaume tutawezana kweli?

Huyu mwanaume tutawezana kweli?

Dexaneo

New Member
Joined
Mar 8, 2018
Posts
4
Reaction score
15
Naomben mawazo yenu kidogo hapa
Ninamchumba ambae tumemaliza process zote bado ndoa tu ambapo tumepanga tufunge mwez wa 7
Mi nawaza nitaishije na huyu mtu?
Mimi ninakipharmacy kidogo mtaji wa 1m ..ammbapo faida naweza pata lak 270_mpaka 3 kulingana na hali ya kibiashara

Mchumba wangu anafanya kazi ambapo anaweza ingiza kuanzia mil 1.7 mpaka mil 2 kwa mwezi
Mimi na mchumba angu huyu tunaelewana vizuri tu tatizo ni mbinafsi sana
Yaana yeye anataka ajue mapato na matumiz yangu lkn yeye ya kwake hata anishirikishi...
Kibaya ananiambia nisevu hela ili nikiolewa namfata wilaya alipo so niweke mtaji kwa ajir ya kufungua kule duka jingine
Sasa jmn kwa kipato changu hicho kwa mwez napoishi nalipa 60 + 50 chumba cha biashara + bills zote maji umeme sehem 2..... Kula Mimi na mtoto
Maana ninamtoto ambae baba ake alishafariki
sasa kwa matumiz hayo naweza save hela kweli?
Maana yeye hanisaidii kwa chochote hata nikimuomba anisaidie kulipa kodi anadai kwao familia inamtegemea hivyo nisubir amalize majukum ya kwao
Nina mwaka nae lkn hajawai kuninunulia hata nguo...hata kiatu tu cha mtoto wangu hawez
Dec mwaka Jana nilipoteza cm akaniambia kopa sehem nitalipa nikamkoba kaka angu nikanunua cm lkn kila nikimwambia tulipe angalau 50 kila mwez anadai nisubir kwanza imebidi niilipe tu mwenyewe
Juz ananiambia tuanze kutunza hela kila mwez yeye aweke lak 2 Mimi laki 1 kwa ajir ya kununua kiwanja....
Nikamwambia nimepata kaz mkoa mwingine basi nikafanye dukan niweke mtu hataki mi kipato hiki hakinitoshi maana Tayar ninamtoto ambae ananitegemea Mimi hataki nikaajiliwe wkt anisaidii chochote
Yeye hela yake ikiingia robo 3 ya mshahara inaenda kwao na kwa ndugu jamaa na marafiki
Juz alipata bonus kazin kwao kama laki 7 hivi nikamuomba elf 30 tu nikanunue kitenge nishone akasema unavaa nini nguo unazo
Sijakaa sawa mjomba ake akaomba laki akatumiwa
Yeye leo ananiambia kanunua cm ya laki 5...

Kinachoniuma anakipato kikubwa lkn hata kidogo changu anataka akijue mapato mpaka matumiz wkt za kwake sijui!!!
 
Nachoweza kusema maisha ya ndoa yanahitaji kujitoa kwa wote wawili na sio ubinafsi wa mtu mmoja, huu ndio wakati wa ufanya maamuzi sahihi usije jutia baadae,

Ndoa ni taasisi nyengine, inahitaji uwe unekubaliana na vyote ndugu yangu kama unaona uhusiano hauko healthy hujachelewa kufanya maamuzi
 
Hapo bado ndoa nanga inapaa hivyo,akikuoa jee??shoga utachundaaa kama nakuona utakavyopalika uwiiii,kuna tabia za kurekebishika na pengine kuvumilika ila tabia ya uchoyo na umimi(ubinafsi)hapana jamanii hazivumiliki na hivi una mtoto tena sio wake ohooo ataumwa huyo atashindwa kumnunulia hata paracetamol,..

Kama unaweza vunja uchumba anza upya kama huwezi basi komaa umzidi kipato na uchumi wako uwe ngangari kwelikweli tena uhakikishe hata ukishuka bado hauwi chini yake.. La sivyo olewa ilaaaa jiandae kisaikolojia,kifizikia,kiakili,kimwili,kiRoho maana nahisi utapelekwa milembe bila kupenda.
 
Mhhh heri nusu shari kuliko shari nzima yaaani ni bora ukaushia njiani kabla hujajifunga. Ila wadada wakisikia kigezo cha kuolewa huchanganyikiwa sidhani kama utatusikiliza mawazo yetu haya. Mimi naona huyo atakutesaaaaaaà
 
Sasa wewe nawe
Ulikubalije mpaka mkafika mbali kiasi hiki na mtu wa aina hiyo?
Whats wrong with your head!

Call off the wedding kama unaona hauta wezana naye. Au kaa naye chini umueleze unategemea nn toka kwake kabla hamja oana, msikilze na yeye anasemaje ukiona haeleweki mwache move on.
 
Hapo bado ndoa nanga inapaa hivyo,akikuoa jee??shoga utachundaaa kama nakuona utakavyopalika uwiiii,kuna tabia za kurekebishika na pengine kuvumilika ila tabia ya uchoyo na umimi(ubinafsi)hapana jamanii hazivumiliki na hivi una mtoto tena sio wake ohooo ataumwa huyo atashindwa kumnunulia hata paracetamol,..

Kama unaweza vunja uchumba anza upya kama huwezi basi komaa umzidi kipato na uchumi wako uwe ngangari kwelikweli tena uhakikishe hata ukishuka bado hauwi chini yake.. La sivyo olewa ilaaaa jiandae kisaikolojia,kifizikia,kiakili,kimwili,kiRoho maana nahisi utapelekwa milembe bila kupenda.
Kafanya uzembe mwenyewe maana unafikaje mbali na mtu wajati unaona kuna tabia haziko sawa!
 
HAHAAA HUYO JAMAA NIMSUKULE AISEEEE HAPO UMEPATIKANA ""

BINAFSI MIMI NI MWANAUME LAKINI SIWEZI KUTETEA ROHO MBAYA YA HUYO MUMEO MTARAJIWA AISEEE ...huwa siwezi kumpa mwanamke Pesa hovyo kama akiwa ninfujaji wa hzo Pesa lakini siwezi kumnyima pia pindi anapohitaji kupata vitu vya muhimu ""

but nikiwa na budget ndogo ya Pesa kutoa kidogo nakuwaga mgumu kiasi chake huwa na angalia nashida yenyewe ya muhusika
 
Back
Top Bottom