Huyu mwanaume tutawezana kweli?

Huyu mwanaume tutawezana kweli?

Kinachoniuma anakipato kikubwa lkn hata kidogo changu anataka akijue mapato mpaka matumiz wkt za kwake sijui!!!

Yani hapo ushauri ni mmoja tu, walk away!
No compromise, NO second thought walk away. A man who can not care for a family is not fit for marriage. Ama msubiri hadi awe matured enough ndo muoane. Please think about the children and the future.

Huyo jamaa hajapevuka in so many levels.
1) Anatakiwa kutenga hela ya familia, akiba na miradi kwa ajili ya familia (Na hii itoke kichwani kwake mwenyewe na atekeleze mwenyewe in preparation for marriage).

2) Atafutie familia yake (Kabla hajaipata) mahali pa kukaa (shelter) na plan nzuri za kuishi na kupata mahitaji kama mavazi, chakula, elimu na nyinginezo (Hii pia ni mipango yake mwenyewe na mkewe atakuja msaidia huko mbele).

3) Awe na aibu na heshima kwa jamii. Huwezi kopa hela kwa shemeji halafu unambwela kulipa kha!

I can go on and on but the point is, he is just not ready for marriage!
 
Ukiolewa nae huyo utateseka sana its not too late unaweza kufanya maamuz mapema
 
Naomba tu uende ukafanye kazi uko ulipopata,dukani mweke mtu,
 
Am out of words. Dada unatafuta nini hasa toka kwa huyo mwanaume? Mungu amekujalia unapata hela yako ya kula na mtoto wako anakula, huko unakoelekea watafuta kitu gani?

Mimi ni mwanamke kama wewe, na sio kwamba nakuonea wivu, ila trust me, huko ubakoelekea utalia kilio cha mbwa mdomo wazi. Achana na huyo mwanaume, hakufai kabisa.

Kama tu kipindi cha uchumba anakufanyia hivyo, prepare yourself for worse my dear.Cut off the wedding, hakuna mume hapo kipenzi.
 
Naomben mawazo yenu kidogo hapa
Ninamchumba ambae tumemaliza process zote bado ndoa tu ambapo tumepanga tufunge mwez wa 7
Mi nawaza nitaishije na huyu mtu?
Mimi ninakipharmacy kidogo mtaji wa 1m ..ammbapo faida naweza pata lak 270_mpaka 3 kulingana na hali ya kibiashara

Mchumba wangu anafanya kazi ambapo anaweza ingiza kuanzia mil 1.7 mpaka mil 2 kwa mwezi
Mimi na mchumba angu huyu tunaelewana vizuri tu tatizo ni mbinafsi sana
Yaana yeye anataka ajue mapato na matumiz yangu lkn yeye ya kwake hata anishirikishi...
Kibaya ananiambia nisevu hela ili nikiolewa namfata wilaya alipo so niweke mtaji kwa ajir ya kufungua kule duka jingine
Sasa jmn kwa kipato changu hicho kwa mwez napoishi nalipa 60 + 50 chumba cha biashara + bills zote maji umeme sehem 2..... Kula Mimi na mtoto
Maana ninamtoto ambae baba ake alishafariki
sasa kwa matumiz hayo naweza save hela kweli?
Maana yeye hanisaidii kwa chochote hata nikimuomba anisaidie kulipa kodi anadai kwao familia inamtegemea hivyo nisubir amalize majukum ya kwao
Nina mwaka nae lkn hajawai kuninunulia hata nguo...hata kiatu tu cha mtoto wangu hawez
Dec mwaka Jana nilipoteza cm akaniambia kopa sehem nitalipa nikamkoba kaka angu nikanunua cm lkn kila nikimwambia tulipe angalau 50 kila mwez anadai nisubir kwanza imebidi niilipe tu mwenyewe
Juz ananiambia tuanze kutunza hela kila mwez yeye aweke lak 2 Mimi laki 1 kwa ajir ya kununua kiwanja....
Nikamwambia nimepata kaz mkoa mwingine basi nikafanye dukan niweke mtu hataki mi kipato hiki hakinitoshi maana Tayar ninamtoto ambae ananitegemea Mimi hataki nikaajiliwe wkt anisaidii chochote
Yeye hela yake ikiingia robo 3 ya mshahara inaenda kwao na kwa ndugu jamaa na marafiki
Juz alipata bonus kazin kwao kama laki 7 hivi nikamuomba elf 30 tu nikanunue kitenge nishone akasema unavaa nini nguo unazo
Sijakaa sawa mjomba ake akaomba laki akatumiwa
Yeye leo ananiambia kanunua cm ya laki 5...

Kinachoniuma anakipato kikubwa lkn hata kidogo changu anataka akijue mapato mpaka matumiz wkt za kwake sijui!!!
Mpige chini
 
Mtu anakutumia kisawasawa kisa ndoa!? Kwanini uteseke kwasababu ya ndoa!?? Kama sasa hivi ni wakati wa uchumba, usitegemee kama atabadilika akikuoa, tena hali itakuwa mbaya zaidi huko mbeleni. Mweleze mapema tatizo unaloliona, na kwamba aoneshe mabadiliko sasa hivi kabla ya ndoa, kama hataki ujue, biashara ndio imekwisha hapo! Hata ukiingia tambua utajiingiza shimoni
 
Back
Top Bottom