Huyu mwanaume kanichosha kabisa sijui tu nifanyeje ni mpenzi tumeahidiana kuoana anavyodai by DEC tuanze process za kutambulishana nyumbani japo ndugu zake au wazazi wake naongea nao kwenye simu so wanafahamu mtoto wao ana mchumba japo hawajaniona.
Kinachonikera kwa mchumba wangu huyu hana akili ya kujiongeza, mimi nina duka lina mtaji kama mil 2 au 1.5 hivi so kwa mwezi naweza pata faida kama ya lak 4. Mwenzangu anafanya kazi katika kampun flani ana mshahara mzuri tu kuanzia million hivi.
Tatizo la mtu wangu hajui mwanamke anahitaji hiki wala hiki mimi sina tabia ya kumuomba hela huwa nampa Uhuru tu anipe yeye atakayoona kama mwanamke nahitaji matumiz gani.
Ajabu hawezi jiongeza kabisa anaweza akaja kwangu akala akalala akaondoka asubuhi haachi hata hela ya matumizi au akaja akashinda akala akalala akaondoka bila hata kujali chochote.
Yaani nakuta najigharamia kila kitu kuanzia, kodi, bills zote, mafuta ya kupaka, saloon, nguo kula yaani kila kitu kuna kipindi nilijaribu kuongea nae akasema OK sorry akawa akija kulala asubuh anacha elf 5 ya matumiz ilienda kama siku 3 hivi akaacha. Napata uchungu Mimi nina mtoto nilizaa na mwanaume mwingine huwa anatoa hela ya matumizi ya mtoto, unakuta mzazi mwenzangu akinitumia hela nanunua vyakula naweka ndani tunatumia na huyu mchumba wangu moyo wangu unauma nashindwa niamue nini naogopa kumpoteza maana umri umeenda, Nina 30yrs.
Napata uchungu kuona nahangaika kutafuta maisha, nakaa Dukani kuanzia asubuhi mpaka SAA NNE sina msaada wowote, yeye akija niku sex tu asubuhi akaondoka na anaweza akafululiza hata siku 4 kila siku anakuja kulala na hanisaidii chochote.
Sasa Jana kaniombia anashida nimtafutie elf 40 mshahara ukitoka atanirudishia, nimemwambia sina akadai tafuta tunza kila siku elf 10 katika biashara yako Jumapili unipe mshahara ukitoka nitakurudishia bado nawaza hata hanionei huruma???
Naomben ushauri ndugu zangu