Mpendwa mwajiri, serikali, familia na wengine wote mnaonihusu.
Kwa kutambua kuwa world cup ni ya dunia nzima basi tusaidiane kama ifuatavyo:
1. Boss ukiniona nasinzia ofisini tuamshane tu kwa upole
2. Nikichelewa kufika kazini boss mwezi huu tusameheane tu kwa upole
3. Muhongo umeme mwezi huu tafadhali tusikomoane
4. Mke wangu mwezi huu chukulia tu kama nimesafiri ili tusigombane
5. Chonde chonde boss safari zozote za kikazi zifanyike maeneo ya mjini na padiem boss iongezeke kidogo ili nkalale hotel zenye dstv
6. Strabag naomba barabara zote zifunguliwe ili hata nikichelewa kuamka niweze kuwahi kufika kazini
7. Boss mshahara wa mwezi huu nishikie kwanza maana ntamaliza kwa Ku bett
8. Wafanyakazi wenzangu nikija ofcn cjapiga mswaki tuvumiliane mjue nimekurupuka
9. Mchepuko wangu Tafadhali yale maneno matamu matamu cjui darling, baby ...nahisi huu sio muda wake ntakuudhi bure.
10. Police nikitukana mjue ni hasira tusameheane mwezi huu.
Mwezi huu usitufarakanishe tuvumiliane tuchukuliane ktk kila hali asanteni.