Huyu msichana kaniaibisha sana sikutegemea

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
5,741
Reaction score
8,527
Binafsi huwa sipendi kutongoza tongoza na hata nikivutiwa na msichana huwa sikurupuki kumtongoza hadi nione light flag kuwa nayeye anavutiwa na mimi lengo ni kuondoa kero na aibu za kutangazwa kwa watu

Sasa huyu msichana nimesoma nae o-level na kiukweli nilikuwa navutiwa nae ila sikuwahi kumwambia japo alikuwa anaonekana kuvutiwa nami pia. Hadi tunamaliza Form4 hatukuwahi kuongea inshu za mapenzi

Mimi nilifaulu kwenda form5 yeye hakufanikiwa kupass sasa juzi kati narudi kitaa akanifungukia kuwa angetamani kuwa namimi ila hakusema kinaga ubaga alisema kwa mafumbo mimi nikampa moyo usiwaze na kwakuwa tulikutana tu njiani kusalimiana kila mtu akajua Mambo yake

Basi nikamcheki kwa sms tukachati na kumuuliza kuhusu lile alosema akawa hakukubali wala hakukataa akabaki katikati. Sasa kilichonikera kesho yake naenda kwa mashkaji kupiga story mbili tatu nakuta kila mtu anayo habari kuwa eti nimemtongoza na namtaka aiseeh nimejisikia vibaya Sana

Yani nilikuwa nakaribia kumuelewa na kumpenda lakini ghafla nimemkinai sitaki hata kumuona sijui wasichana wakoje
 
Binafsi huwa sipendi kutongoza tongoza na hata nikivutiwa na msichana huwa sikurupuki kumtongoza hadi nione red flag kuwa nayeye anavutiwa na mimi lengo ni kuondoa kero na aibu za kutangazwa kwa watu

Sasa huyu msichana nimesoma nae o-level na kiukweli nilikuwa navutiwa nae ila sikuwahi kumwambia japo alikuwa anaonekana kuvutiwa nami pia. Hadi tunamaliza Form4 hatukuwahi kuongea inshu za mapenzi

Mimi nilifaulu kwenda form5 yeye hakufanikiwa kupass sasa juzi kati narudi kitaa akanifungukia kuwa angetamani kuwa namimi ila hakusema kinaga ubaga alisema kwa mafumbo mimi nikampa moyo usiwaze na kwakuwa tulikutana tu njiani kusalimiana kila mtu akajua Mambo yake

Basi nikamcheki kwa sms tukachati na kumuuliza kuhusu lile alosema akawa hakukubali wala hakukataa akabaki katikati. Sasa kilichonikera kesho yake naenda kwa mashkaji kupiga story mbili tatu nakuta kila mtu anayo habari kuwa eti nimemtongoza na namtaka aiseeh nimejisikia vibaya Sana

Yani nilikuwa nakaribia kumuelewa na kumpenda lakini ghafla nimemkinai sitaki hata kumuona sijui wasichana wakoje
Hapo mwenzio amekuelewa anaimarisha ulinzi wengine wasikuchukue. Kama unampenda maliza show. Kwa sisi tuliokula chumvi hayo ni kawaida. Tena bora huyo mwingine anakutangaza Mhuni ili wengine waogope halafu ajilie pweza gizani. Ipo siku utanielewa
 
Angefanya hivyo kwa wasichana wenzie ningemuelewa ila ananitangazia kwa mashkaji ili iweje huyu analake lingine
 
Duuh sawa ila nikimuona sijui namuonaje sitaki hata kumuona kwanza

Hutaki kumuona kwa sababu kasema jamaa mtaani umemtongoza? Halafu mkionana utamuuliza kwanini unasema nakutongoza? Unakoelekea kumdharirisha binti. Kama ulikuwa unataka kujiweka na unavutiwa naye kukubari kuwa kweli unamtongoza shida iko wapi? Labda kama umeona ana tabia za hovyo ulitaka kupiga na kuchapa mwendo. Kama ni malaya una haki ya kukasirika. Kama ni innocent mlinde
 
Hapo mwenzio amekuelewa anaimarisha ulinzi wengine wasikuchukue. Kama unampenda maliza show. Kwa sisi tuliokula chumvi hayo ni kawaida. Tena bora huyo mwingine anakutangaza Mhuni ili wengine waogope halafu ajilie pweza gizani. Ipo siku utanielewa
Kuna pisi nilichukua namba kwa ajili ya biashara, kesho yake nasikia mtaani kashatangaza nimemchezea na kumuacha, hayo maneno aliniambia dada mmoja tunaheshimiana sana, nikaambiwa tena na mtu mwingine. Na ako na sura pasono mweusi tiii chuma cha mjerumani.
 
Hutaki kumuona kwa sababu kasema jamaa mtaani umemtongoza? Halafu mkionana utamuuliza kwanini unasema nakutongoza? Unakoelekea kumdharirisha binti. Kama ulikuwa unataka kujiweka na unavutiwa naye kukubari kuwa kweli unamtongoza shida iko wapi? Labda kama umeona ana tabia za hovyo ulitaka kupiga na kuchapa mwendo. Kama ni malaya una haki ya kukasirika. Kama ni innocent mlinde
Mkuu sasa yeye ndio kaanza kunitongoza halafu anatangaza nimemtongoza tena kwa jamaa zangu tunaoaminiana sana na kuheshimiana hata kama nimemtongoza kweli ndio anitangaze mtaa mzima?
 
Back
Top Bottom