Huyu mlemavu ana matusi balaa

BatteryLow

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
446
Reaction score
149
Hapa mtaani kuna mlemavu ana mguu m1 anatumia magongo, basi aliniomba pesa siku ya kwanza nikawa sina akapita siku nyingine akaniomba nikamwambia sina, mungu wangu, aliporomosha matusi balaa, alianza kwa kusema 'hivi ww unanionaje? leo ni mara ya pili nakuomba msaada unasema huna?...' Siku 1 nikamweleza jamaa yangu akaniambia yule alikuwa jambazi akapigwa akavunjwa mguu, eti watu kama hao mungu anawapunguza kasi ya kuwafanyia watu maovu kwa kuwapa kilema. Nikaamini kwa jinsi yule kilema alivyo na matusi, je angekuwa mzima si shida?
 
Pole sana kaka!!! Kuna mmoja yupo Tazara pale mataa!!! Siku moja akiwa na mwenzake naye mlemavu,aliniomba hela,sasa kwakuwa walikuwa wawili nkatoa 5000 nkawaambia wakagawane!! Mungu wangu lilikuwa ni kosa,jamaa aliniporomoshea matusi balaaa akisema kwanini niwape wakagawane? Toka siku ile nkasema sitatoa hela tena kwa jamii hii
 
tena kuna wengine wanaigiza utafkiri ana mguu ngama kumbe mmoja anaficha, na matusi juu anakupa!!
 

Usije ukawahurumia watu kama hao, wanatumikia adhabu ya muumba.
 
Ningemshushia kisago hadi akiniona anisalimie.

Huwezi kunitukana from nowhere
 


 

Na mie ningemtukana na angerudisha Pesa yangu na makofi juu ..huwa wanatumia ulemavu wao vibaya huruma sometimes haiapply sehemu zote.
 
kuna mmoja Arusha ni babu yeye ni kiwete hatembei siku moja kaniomba hela nikampa mia mbili yaani alinitukana matusi ya ajabu makubwa.Mwisho akamalizia kwa kusema pumbavu wewe unadhani mimi napigwa na jua hapa kwa ajili ya mia mbili kisha akairusha barabarani
 
Msimsahau yule anayehudhuria midahalo ya nkrumah hall UDSM anadai anatokea mkoa wa Mara eti aliahidiwa na rais 2010 hadi leo hajatimiziwa.
Kila mdahalo ukifanyika nkrumah yupo na madai yake ni hayo hayo. Anafanya shughuli zake saa ngapi?
 
Na mie ningemtukana na angerudisha Pesa yangu na makofi juu ..huwa wanatumia ulemavu wao vibaya huruma sometimes haiapply sehemu zote.

unaweza ukasema ukomae uchukue pesa yako elfu5 wakakuitia mwizi, noma sana
 
Kuna mwingine mzee hivi yupo makutano ya bibi titi/morogoro road kona ya dit ni noma anaita babaa ukimwangalia ukapotezea bila kumtoa sikilizia shit itayokufuata!

Yule mzee si mlemavu.....miguu yake anaikunja.Anaita kama mtu wa heshima ila usipompa anajifanya anakutolea laana
 
Aisee kuna moja alikuwa anajifanya ombaomba kumbe jambazi kakamatwa na polisi akiwa na bunduki na milioni za pesa
 
Kuna mwingine anatembelea maeneo ya sinza yeye anagonga mlango ukifungua tu kabla ya salam anakutolea uume wake na kusema kaambukizwa maradhi ya ngono sasa asipopata pesa utakatwa inabidi umpe maana hata kuangalia ameathirika vipi huwezi na huwa anawatolea wanawake tu maana anajua mwanamume mwenzie atauangalia, usipompa pesa anakulilia yeye hatukani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…