Huyu Mende sijawahi kumuona tangu nizaliwe! Anapaa kama popo umbali mrefu

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,577
15,337
Kuna mende mmoja simuelewi usiku huu maana tofauti na mende wa kawaida yeye anapaa kama popo.

Anauwezo wa kupaa umbali mrefu bila kutua au kuzunguka muda mrefe bila kutua tofauti na mende wa kawaida.

Napata mashaka sana maana tabia za mende huyu sizisomi kabisa.

Je ni mende kweli wa kibaiolojia ?
Je ni Jini anataka kunitoa kwenye mstari?
Je ni mchawi anasoma ramani zangu?
Je ni drone ?
Je ni shetani ananmendea maana alimmendea hawa katika umbo la nyoka?

wataalam wa mambo ya kishirikina, kibaiolojia na kitamaduni mtoe ushirikiano tafadhari.
 
Acha uoga,yaani kuruka ruka chumbani hapo unasema umbali mrefu bwana?
 
Wewe sasa una vituko. Mara nge sasa mende! Kuna mende wakubwa ambao huwa wanaruka kama wadudu wengine wote. Wewe umezoea wale watoto wa mende wa kwenye makabati. Fungua sceptic tank kwako uone mijimende na inavyoruka. Ukianza ushirikina utakufa maskini tena muda mfupi tu.
 
Yaani tuseme baba zima hauelewi "haiba" ya viumbe wanaokuzunguka?

Tangu uzaliwe hauelewi kwamba mende wanajikoboa mbawa na kujivua gamba kama afanyavyo nyoka na anauwezo wa kuruka na kupaa umbali mrefu hadi akafika mawinguni?

Ama ni mende gani hasa unayemuongelea wewe?

Maana ulivyoiandika hii thread ni kama mafumbo yaliyolenga kufumbia wajinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
appetizer imeharibika/chacha bila picha hii ni chai ya saa 8👎👎👎👎
sio chai mkuu, labda sijawahi kuonana na hii spishi ya mdudu mende.
sasa ulitaka video au maana anafanana na mende mzalendo wa kawaida kwa sura ila vitendo vyake ndio sio vya kawaida.
 
Huyo katoka gym hivyo anatest kile alichokuwa anakifanya

Alafu mkuu jaribu kubadilisha geto maana geto lako lipo karibu sana na choo
 
Wewe sasa una vituko. Mara nge sasa mende! Kuna mende wakubwa ambao huwa wanaruka kama wadudu wengine wote. Wewe umezoea wale watoto wa mende wa kwenye makabati. Fungua sceptic tank kwako uone mijimende na inavyoruka. Ukianza ushirikina utakufa maskini tena muda mfupi tu.
kwa sababu ushirikina ni kosa kisheria sio mbaya nikiufikirai mkuu, wenda nikapata ushahidi wa kumshughulikia anayetaka kuleta fyokofyoko nyumbani kwangu.
Ila ni Kweli lile jimende kubwa linapaa dakika kadhaa bila kutua tena umbali mrefu sijawahi kuona ndio maana imenilazimu kumuangalia kwa jicho la nyuzi 360. Kama wapo hapo sawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom