Huyu Mende sijawahi kumuona tangu nizaliwe! Anapaa kama popo umbali mrefu

nachekaga na huyu kaka jaman ana ucomed muda wote😂😂😁 eti jini anakutoa kwenye mstari
hahaha
kweli mkuu wewe mende muda wote yuko Juujuu anashuka saa ngapi ili ale.
Mende anaonekana usiku tu, hasa nikiwa peke yangu,
Ukitaka Kumuua unahangaishana nae utadhani unawinda sungura.
Ikiona yuko hatarini anapaa juu zaidi ambapo huwezi kumfikia, hata ukipuliza rungu haimfikii, ni jengo lenye paa refu kidogo.
Ila nimegundua ni mende wa kawaida asiyepaa kama mende wenzake ambao nimewahi kuwaona tangu nizaliwe.
 
Kapige pesa kwenye maonesho sasa, unasubiri nini??

Sent using Jamii Forums mobile app
1548744135643.png

Kuna drone mende mkuu

Mkuu dunia imebadilika, sio enzi zile za wakina zwangedaba na mwanamutapa ambao kila kitu kilikua natural. siku hizi kuna hadi drone zenye saizi ya kiroboto na anachukua picha safi utadhani Camera ya Iphone 100 ambayo itatoka 2050 .
 
Amka toka chukua rungu au Hit pulisha y akutosha chumbani subiri dk 20 hapa seblen then rudi lala
 
Na huwezi kumuona huyo kuku,utamuonea wapi,au na wewe utakuwa unapaa?

Kawaida tu mkuu wala usijali.
mkuu makadilio tu.
Kama umesimama kwenye Flaiova ya Ubungo (Underconstruction) kuku ukaona anavuka hosteli za magufuli na kupotelea juu ya anga za mcity kwa hesabu za projectile lazima ujue atatua kuanzia kwa Mtumishi Kakobe hadi Kawe baharini.
Hiyo ajabu
 
Yaani tuseme baba zima hauelewi "haiba" ya viumbe wanaokuzunguka?

Tangu uzaliwe hauelewi kwamba mende wanajikoboa mbawa na kujivua gamba kama afanyavyo nyoka na anauwezo wa kuruka na kupaa umbali mrefu hadi akafika mawinguni?

Ama ni mende gani hasa unayemuongelea wewe?

Maana ulivyoiandika hii thread ni kama mafumbo yaliyolenga kufumbia wajinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu mimi ''sinaga'' mafumbo kama wale wakina paskali na gwanamasino.
ni mende kweli, haya uliyosema nilikuwa sijui maana nimeishi kijijini nimewaona mende wakivua gamba lkn kwa kupaa kule kulinishtua kidogo, Labda mende wa dar wamebuni mbinu mpya ya kupambana na hali zao, Maana siku hizi hata majalalani hakuna makombo, wanahofu ya kuliwa labda.
 
Mwangalie vizuri isije ikawa umeingiziwa drone, inakuremodi tu humo.

Sent using Jamii Forums mobile app
labda iletwe na mabeberu, bongo naona bado tuko analojia sana mambo mengi. Lile ni mende la kawaida ila kupaa kule ndio kulinitisha na kunifanya niliangalia katika nyanja zote kibaiolojia, kishirikina na kijasusi.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Ki kawaida mende WOTE wanapaa, si wanayo mabawa sasa washangaa nini?
mkuu hata mbuni anamabawa mkuu ila ukimkuta angani lazima ushangae. avarage ya muda aliopaa na umbali ndio nimeona kama umevuka uzoefu wa mende wa kawaida ikabidi nijiongeze. lkn wadau wanasema yako mamende mengine yanaviwango hivyo.
 
Kwa hiyo unamendewa mkuu?
hahaha hapana nilikuwa namtafiti tu huyu kiumbe.
mimi sina lolote la kumendewa labda na walozi wa mitaani tu maana ukinunua hata kuku wananuna, wanaweza kukutumia drone za asili wakutengue hata kiuno ushindwe kwenda kibaruani uwe kama wao.
 
kwa sababu ushirikina ni kosa kisheria sio mbaya nikiufikirai mkuu, wenda nikapata ushahidi wa kumshughulikia anayetaka kuleta fyokofyoko nyumbani kwangu.
Ila ni Kweli lile jimende kubwa linapaa dakika kadhaa bila kutua tena umbali mrefu sijawahi kuona ndio maana imenilazimu kumuangalia kwa jicho la nyuzi 360. Kama wapo hapo sawa.
Yaani wewe kama Comedian unachekesha saana. Zima taa atatua mende anapenda giza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom