Huyu mdudu anaitwaje?

Huyo mdudu akikuuma kadri anavyo tembea ndivyo sumu inasambaa mwilini
Huo ni uongo stories za wahenga. Nimeshanga'twa zaidi ya Mara 3 na huyo mdudu. Mara moja alifanikiwa kukimbia baada ya kuning'ata.
 
huyo ni mende pori...no, ni tandu, mpuuzi tu kwetu akikuuma unajikata ulipoumwa, unamchoma jivu lake unajipa kesi imeisha
 
Sheikh Zanziberi kwema?

 
Hata jamaa yangu aliingiliwa na huyu mdudu kwenye suruali lakini bila ya kujua kama ni Tandu alivua suruali na kumtoa bila ya kuumwa,nadhani inapofikia kukuuma ni lazima utakuwa umembana au umemkanyaga,tofauti na Nge..
 
Huyo Ni tandu anauma na ana sumu Kali tu japo haiui. Akikuuma kama leo sa10 utabaki na maumivu makali mpaka kesho mda kama huo ndio unapata nafuu
 
Pole sana
 
Hata jamaa yangu aliingiliwa na huyu mdudu kwenye suruali lakini bila ya kujua kama ni Tandu alivua suruali na kumtoa bila ya kuumwa,nadhani inapofikia kukuuma ni lazima utakuwa umembana au umemkanyaga,tofauti na Nge..
Yah nahisi ni kweli, kama umekaa umetulia ivi hakuumi ata kama anatembea kwenye mwili hata kama utamuondosha kwa mkono na akawa bado yupo katika mwili haumi, huyu nahisi anauma pale unapombonyeza kwa nguvu kiasi cha kuhatarisha uhai wake ndio ana respond. Nilishukuru mana nlikuwa na waza sijui kama ningekufa siku hio πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Tandu Huyo, Kuna species nyingi sana, baadhi ya specie wana sumu Kali sana kiasi akikung'ata ukachelewa kupata matibabu Unaweza ku-paralyse mwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…