Huyu Mdada Anateseka!...Kuna Namna Ya Kumsaidia... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Mdada Anateseka!...Kuna Namna Ya Kumsaidia...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Boflo, May 28, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]Habari zenu?[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kila napoangalia wanawake wengine wanapendwa na waume zao roho huwa inaniuma sana ,sio kwasababu naona wivu ila kwasababu nawaza kwanini isiwe mimi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Nimeolewa mwaka wa kumi na moja huu sasa tuna watoto watatu .mume wangu ana kimada nje ambae amezaa nae na ndio anaemthamini zaidi yangu na wanawe.kuna wakati hawalipii watoto ada ya shule hadi wanarudishwa nyumbani, mwaka jana mtoto wetu wa mwisho ndio alizaliwa pale katika hospitali ya tmj,mikocheni.nilijifungua kwa operesheni na nilikaa hospitali siki 3 bila mume wangu kufika hospitali na nikawa nashindwa kurudi nyumbani kwasababu sikuwa na pesa ya kulipia kila akipigiwa simu hapokei,mpaka siku ya tano ndio alinifata na kunipeleka nyumbani.[/FONT]
  [FONT=&quot]Ni visa vingi na mateso mengi nimeyapata kwa huyu baba.huwa anatuacha nyumbani hata wiki nne bila pesa ya chakula inabidi niende kuomba chakula kwa majirani,akirudi nikimuuliza ananipiga sana mpaka kuna siku alinivunja taya.sijui nifanye nini,sina pa kwenda,sina pa kuwapeleka wanangu.nifanye nini?je kuna sehemu yoyote nayoweza kwenda nikapata msaada
  [/FONT]
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  oooh jamani hii habari imeniumiza sana moyoni..machozi yamenitoka
  kwanini mnakuwa hivi jamani? Mbona hamtuhurumii ?
  Tunajua mnayafanya huko nje ..naona huyu kavuka mipaka natamani nimfate nikamtafune mzima kwani huyu dada hana ndugu jamaa na marafiki wanaoweza kumpa msaada wa karibu haya ni mateso .
  siku yangu imevurugika kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.naomba mungu unisaidie usinipokonye kipato changu hiki kidogo kinachonisaidia kujikimu maisha ....
  oooh eeeh kumbe ni hivi???????
   
 3. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Dada, uyo mmeo ametekwa tu na shetani, siku akija kufumbuka macho, atasikitika sana juu ya anachokifanya, na atakuheshimu kwa uvumilivu uliompa....wakati mwingine wanakuwa wamelishwa dawa tu na hao nyumba ndogo hivyo hajielewi pengine, mwonee huruma tu..usishindane na mtu asiyeelewa utakuwa unamwonea. Nakushauri mwombe Mungu, atakusaidia, Mungu anaweza kuzibua hata kama alilishwa libwata, atarudi kwako na atakuheshimu. ila ukichukua uamzi mbaya, yeye atakaporudi kujitambua na kuona wewe ambaye ulikuwa unaelewa haukumsaidia kwa maombi na uvumilivu, huta pata heshima ile ambayo ungepata kama ungemwomba Mungu na kumsubiria....hii ni ngumu sana kuifanya ktk ulimwengu huu wa usawa ktk jinsia etc. wengi hapa watakushauri mengine...

  nenda kanisani kwa watu waliookoka, shirikiana na wachungaji kumwomba Mungu, Mungu atambana kwenye kona yeye mwenyewe atajileta akitembelea magoti. tumeona watu waliokuwa wamebebwa na machangu wanalia kama watoto wadogo kuomba msamaha kwa wake zao baada ya maombi...wakati mwingine mchungaji wangu alishawai kumwombea mtu fulani, aisee, varangati lililotokea huko kwa nyumba ndogo, hamu yote ya nyumba ndogo iliisha siku hiyo hiyo na akarudi moja kwa moja kwa Mke wake. Mungu anao uwezo wa kuwagombanisha hao mahawara za mmeo naye, akarudi home akaona hamna faida kabisa kuitelekeza familia. SO PLEASE, SOLVE IT IN THAT WAY, usi sovu kwa namna ingine, kwani ukisolve kwa namna ingine inaweza kuongeza madhara badala ya kupunguza.
   
 4. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Hata la kushauri sina, imenikumbusha mateso mengi sana. Ni mateso makubwa ya kutisha, na wala wanaume hao hawajali. Moyo.... Msaada gani maskini? kama anayetakiwa kuwajibika anaishi hajafa na unageuka ombaomba, watoto........ usiku hulali mchana mawazo tele...... Sina la kusema. :angry:
   
 5. vkeisy2006

  vkeisy2006 JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 230
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  daaaah mi nahuzunika sana kwa nini jamni inakua hivi wababa kwa nini hamna huruma....jana nusu jirani yetu afekule mtaani mume wake ameoa anapitisha miezi haji home mama wa watu anauza mkaa apate hela ya kula na wanae sita yule baba amewaacha akija hapo home ni matusi kwenda mbele mtu mbaba mzima miaka 60 halafu BOSI WA DOWUTA BANDARI....Inatia kinyaa..hela mpaka akatwe kwenye mshahara kutoka oFisini ndo ipelekwe home daaah wanaume mnatutisha sisi ambao bado hatujaolewa jamani itakueje...huyu jirani yetu jan apresha nusu afe.....dada pole sana mungu akusaidie NENDA TAMWA WAMKOMESHE HUYO MBABA ASO HAYA....yani na hasira kama ntukane...lakini naheshimu kijiwe....ila kina baba mmezidi jamani....MBONA ZAFANANA TU KWANINI HAMTULIII.....
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa nini usikae chini na wote wawili muwe na discussion nzuri? Wote wawili watoe yaliyomo moyoni alafu muangalie kitakachofuata! SIkubaliani na kuteseka kwa mwanamke yeyote katika ndoa. Ni nafuu afungushe virago vyake na kwenda kuishi mwenyewe!
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duhh kuna mianaume mingine mikatili kweli sijui kalishwa libwata!!
   
 8. c

  christer Senior Member

  #8
  May 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole sana my dear,msaada unaohitaji sasa ni kujengewa uwezo wa kutunza familia hasa shule kwa watoto
  kwani hao ndo watakusaidia baadae.huyo bwana mkabdthi kwa mungu, ipo siku atakukumbuka na kukuona wa maana.la muhimu usizae nae tena kwa kipindi hiki ambacho haeleweki.la sivyo utakuwa mchezo wa kukuzalisha.
  nanyie wanaume mbona hivi jamani?mtatukosesha peponi bure kwa matendo yenu maovu.
   
 9. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  uslilie F.L utakuja kuliza jukwaa zima hapa...hata mimi hapa machozi yananitoka...
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pole na safari ya Mombasa kumbe tayari jijini!
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  kuzaa watoto wengi napo ni tatizo maisha yanakuwa magumu unawaza huna msaada ukiangalia watoto wanakuliza ..wajibu wako kuwatunza lakini leo hii wanakushinda ..kwa nini nisitoe chozi mie
   
 12. ngonzi zomukama

  ngonzi zomukama Senior Member

  #12
  May 28, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani huyu baba sio akili yake ni pepo yuko akilini maana hata watoto wa kuwazaa jamani wamekosa nini hawa malaika wa mungu? kuna haja amlazimishe aende kanisani atolewe mapepo na afunguliwe akili yake me najua amefungwa eidha kwa kupewa LIMBWATA au SHUNTAMA imenitia simanzi sana sitamani kuolewa tena kama mambo yenyewe ndo haya.
   
 13. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wanaume mbona hamchangii jamani hii topic!! Mkimaliza kusoma tu..mnakula kona..kwa nini???
   
 14. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ni kwasababu huyo mwanaume anatuaibisha sisi wanaume wenzie, huwezi kutupa watoto na mke wako first love namna hiyo..mke ni mke jamani ana raha yake, nyumba ndogo hata ikijifariji, kuna siku masikitiko yatawajia tu hao nyumba ndogo, kwasababu huyo bado ni mumeo. this is too bad.
   
 15. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Boflo sio hivyo topic hizi tumezidiscuss sana kwa style tofauti.

  kwa kuchangia tu ni kwamba huyu dada muulize alijuana na huyo mume wake kwa muda gani kabla ya kuoana? aliomba Mungu ammpe Mume au mchumba? kwani naamini mume/mke bora hutoka kwa Mungu
   
 16. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jamani nimeumia mm, hv kwann wanawake wanateseka hivi!
  huyu dada anatakiwa amwombe Mungu sana na atafute kipato ili asishindwe kuwalisha na kuwasomesha watoto. hata kama hana elimu ajishughulishe na kazi ndogondogo angalau asimtegemee huyo mwanaume kwa kila kitu.
  Wanaume hawa!
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mhh Fidel!
  Kulishwa limbwata siyo hoja..kwani alishikwa pua afungue mdomo alishwe kwa nguvu?
  Huu ni ulimbukeni haswa ... Iweje wewe mwanaume mwenye akili timamu... unajua una familia ukaamua kuwa na mpenzi wa pembeni ujisahau namna hii? Kwani jamani mkiwa na hao wapenzi wenu wa nje akili inahama? Si bado mnakuwa na akili zenu? Ingekuwa akili zinahama basi mngekuwa mnasahau hata kuvaa nguo na hapo tungejua kweli kuwa love can make u go crazy.Ni wazi kwamba akili bado zinakuwepo.Kwanini ushindwe kutanabahi kuwa hilo penzi la nje ni kitu cha muda cha kupita kama ulivyomzuzukia mkeo hadi ukamuoa, hata huyu kimada wako utakuja kumuona wa kawaida tu.Kabla hujajiingiza kwa nyumba ndogo jipige interview wewe na roho yako ujue kama una ubavu wa kubakiza akili zako intact.

  Kwa mdada unayewakiliswha na boflo, elewa kuwa waume wengi wana roho ndogo sana ya kushinda majaribu.The good thing is wengi hata kama wana vimada, hustahi na kuheshimu familia zao kwa kuzijali kwa kila hali ikiwa ni pamoja na mahitaji - shule, chakula, mavazi, ugonjwa nk.Huyu wa kwako inaelekea alikuwa mbaya tangia akikuchumbia na ulidhani utambadili uingiapo ndani ya nyumba ya ndoa.Hilo lilikuwa kosa. Maadam ulishakosea toka mwanzo, ujue hilo ni zigo lako utalibeba na kuhangaika nalo labda ulitue. Sasa ni wewe tu uamue unataka kulitua lini na kwa style gani.
  Pole sana mpenzi!
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Libwata siku hizi dili mama,
  Mtu anamlisha mwanaume kwa matakwa yake binafsi na akili za mwanaume zinahamia kwa huyo kimada.
  Nina jamaa zangu kadhaa walilishwa hii kitu ikabidi tufanye kazi ya ziada kwenda kwenye kamati za ufundi sasa hivi wanafrahia maisha yao.
   
 19. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nishawachukia wanaume wote long time ago ni kama vile baba yao mmoja
  samahani mashemeji kama nitawakwanza ila hii ni kutoka moyoni.
   
 20. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Manaume mengine bana, kama hayawezi kuendesha ndoa zao kwanini yanaoa.......nimekasirika kweli!...wengine tunahaha kupata wake, mijitu mingine inatesa wake zao....aaaaaaaaaaarrrrrrrrrrgggggggg
   
Loading...