Huyu mchumba ana tatizo gani?

Huyu mchumba ana tatizo gani?

Habari zenu wakuu?
Mimi ni msichana na nipo kwenye mahusiano na mtu ambaye naona simuelewi.
Kiukweli nampenda sana ingawa sijui kama yeye ananipenda ingawa kuna muda anadai ananipenda pasipo hata kumuuliza kama ananipenda.
Mwanaume huyu tumedumu nae kwa mwaka sasa.
Tatizo lililopo ni kama vile kuna muda anakua hajielewi au anakua comfused.
Tunaweza kupatana sana text, calls kukutana ni all the time. Kumissiana ndio usiseme. Ikitokea tatizo tunashirikiana sana kwa pamoja hadi linaisha.
But furaha yetu uwa haidumu. Tunaweza kukaa hivyo kwa miez mitatu ila baada ya muda tu anaweza kuanzisha ugomvi hata wa kipuuzi tu mfano mara nya mwisho alikasirika kwa nini nilimuuliza kua kwa nini hakupokea simu yangu.
Hapo hata nikijishusha itakua ni ugomvi kwa miezi hata miwili, atanuna kama mtu aliyepania ugomvi uwepo kwa makusudi fulani.
Kuna kipindi nikaona kheri kuondokana na maisha haya. Kweli nilimuacha na maisha yake lakini baada ya miezi miwili or less alinipigia simu usiku wa birthday yake na kuniomba msamaha sana na kua hatorudia tena mambo yake.
Kweli nilimsamehe na tukakaa chini kuongelea nini kinachomfanya muda mwingine awe anakurupuka namna hiyo. Akaomba msamaha na kudai hatorudia hilo.
Lakini wiki iliyopita mambo yaleyale yamejitokeza. Hiyo haikupita muda hata wa wiki, akapata habari nzuri juu ya mambo yake ya kazini, haraka alirudi kunishirikisha ambapo tukawa kama watu ambao hatujagombana.
Baada ya kunishirikisha jambo lake, kama mtu aliyetua mzigo, ugomvi umerudi tena.
Wakuu mimi siamini kwenye kila tatizo ni kulikimbia, nataka kurekebisha na tuishi kwa furaha tena kama ilivyokua mwanzo.
Sijui nini cha kufanya hivyo naombeni ushauri wa kujenga. I am confused.
Hajazaliwa mwezi wa nne (April) kweli Huyo? Hebu lete hapa tarehe yake ya kuzaliwa!
 
My brother ngoja nikuambie
Kuna wengine wana penda sana utata so pale akiona amani ipo tele anaona kama vile kuna tatizo so ugomvi kwake yeye ndo amani. So brother cha kufnya jua kumsoma
Ukishajua ameaanza kuwa mkali wewe kuwa normal kwan itafika mda atapoa na kutaka kuwa na amani au mda mwingine usijali. Si anapenda kugombana we kuwa kama haujali mwisho wa siku atakuja kushuka na pale anapokuwa anataka iwepo amani ndo na wewe anza kujali.
Cha muhimu uwe unajua kumsoma attitude yake
 
Back
Top Bottom