Huyu Mama noma sana

Tuwaseme

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
645
1,188
Mama mmoja aliamua kumtembelea mtoto wake wa kiume anayesoma chuo kikuu katika HOSTEL aliyopanga ili wale chakula cha jioni pamoja..
Alipofika hapo chumbani kwa mtoto wake alimkuta mwanaye anaishi na msichana mrembo sana pia kuna vitanda viwili, yule msichana akaanda chakula wakala pamoja,,,
Lakini Mama akawa anamuangalia sana yule binti, mtoto wake akavunja ukimya na kusema:
(NAJUA UNACHOFIKIRIA MAMA, USIWE NA WASIWASI HUYO NI MWANACHUO MWENZANGU TUU WALA SIO MPENZI WANGU)
Mama akatabasamu tuu lakini hakujibu kitu
Harafu akawaaga na kuondoka zake‍♀
Baada ya siku tatu, yule msichana akamwambia yule jamaa kuwa tangu mama yake aje kula chakula siku ile kuna sahani moja ya SILVER imepotea pale chumbani

Jamaa akaamua amuandikie BARUA mama yake isemayo:

(SHIKAMOO MAMA YANGU KIPENZI, NI MATUMAINI YANGU KUWA UMZINMA WA AFYA NA MIMI PIA NI MZIMA, MAMA KUNA SAHANI YA SILVER ILIPOTEA HAPA CHUMBANI KWANGU TANGU BAADA YA WEWE KUONDOKA SIKU ILE ULIPOKUJA KULA CHAKULA,,,, SIO KWAMBA NASEMA UMEICHUKUA WALA SISEMI KWAMBA HUJAICHUA ILA KIUKWELI SAHANI HIYO ILIPOTEA TANGU SIKU ILE ULIPOONDOKA HUKU✍
Wako mwanao kipenzi)

Mama baada ya kupokea ile barua akaamua kujibu namna hii:

✍ MARHABA MWANANGU, SISI SOTE NI WAZIMA,, SIO KWAMBA NASEMA HUYO MSICHANA HUWA UNALALA NAYE KITANDA KIMOJA WALA SISEMI KUWA HUWA HULALI NAYE KITANDA KIMOJA, ila ukweli ni kwamba kama huwa analala kwenye kitanda chake basi angeiona hiyo SAHANI YA SILVER chini ya mto wa kitanda chake...
wako mama kipenzi.
 
hahaha mama anafahamu ase,huenda kwa kuwaangalia machoni pao tu alifahamu kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao.akina mama wana busara sana aseeeee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom