Habari wana jf?
Nadhani niliwaletea mkasa wa mimi kugombana na boyfriend wangu kiufupi nilitambulishwa na nilifahamiana na mama mkwe na ndugu wote wa ex boyfriend wangu pamoja na wao kuwafahamu ndugu zetu na kuna muda wanakuja hadi nyumbani kusalimia.
Inapotokea ugomvi na mwenzangu, wao wanakua chachu na kuchochea sisi kuachana.
Tofauti na mategemeo ya kuona wao wakiwa mstari wa kwanza kutusuluhisha lakini wao wanakua wa kwanza kunipa ushauri wa kuachana na mwenzangu kua sitomuweza nk nk.
Swali kubwa nililokua najiuliza, sijawahi ona mama akikataa mkwe mzuri mpole na mwenye future hata kama mwanae ni kibaka. Ila akipata mkwe ambaye anajielewa anakua chachu ya mapenzi yao.
Wenzangu nimekutana na hizo kasumba na je ni dalili za kua sitakiwi kama mkwe? kwa nini wasimwambie mwenyewe kua huyu dada achana nae?