Huyu jamaa kiboko

Syston

Senior Member
Nov 6, 2017
184
250
Jamaa mmoja alitembelewa na rafiki zake geto, kama unavyojua hii januari jamaa alikuwa juu ya mawe, anafunga mchana anafuturu usiku.

Sasa kama unavyojua wakija wageni hata kama unalala njaa inabidi uwaoneshe unakulaga, jamaa akawachemshia chai ila haikuwa na sukari, akaenda kununua mihogo kahela aliko bajeti kampush siku kadhaa.

Jamaa akawaandalia chai wageni wake ila kabla hawajaanza kunywa akawaambia kuna kikombe kimoja chai haina sukari hivyo atayekipata ajue atawanunulia wenzie lunch mchana.

Basi mpaka wanamaliza kunywa chai kila mmoja anamwambia jamaa sukari mbona kama ilizidi kidogo maana chai ilikuwa tamu kama asali. Hakupatikana aliyekosa sukari.

Jamaa akasolve ishu yake kiaina tu.
 
Top Bottom