Hii imenikuta jana,
natoka zangu job jioni nikasema nipitie dukani nikanunue mahitaji mawili
matatu. Nimeshanunua nakaribia mlangoni simu inaita , naangalia naona
namba land line siijui.Nikapokea na mazungumzo yangu na Caller yakawa
hivi.
Caller: Hallooo (Sauti ya mwanamke wa makamu kiasi atleast 40 years of
age)
Maundumula: Halloo habari
Caller: Wewe ndio unaitwa Maundumula (sauti ya ukali)
Maundumula: (Anasita kidogo kwakuwa anayepiga simu hajajitambulisha na
tone yake inaonesha yupo impatient)
Caller: Au sio wewe mimi nikate simu
Maundumula: Ndio mimi , nazungumza na nani?
Caller: Mbona unanijibu kwa ukali, nitakata simu mimi, nakupigia kwa
faida yako mwenywe
Maundumula: (Confused, anabaki kimya)
Caller: Uliomba kazi ya ...... au hukuomba nikate simu?
Maundumula: Unapiga simu kutoka wapi?
Caller: Nina watu wengine wa kuwapigia na wewe unanipotezea muda, au
nikate simu??
Maundumula. Mama, mbona unakuwa mkali hivyo , au ndio unanipigia
ushahidi tu wakati mna watu wenu mmeshawaahidi kazi?
Caller: Huoo usemi ndio ufute kabisa yaani uufute kabisaaa huo wa kusema
tuna watu wetu tungekuwa na watu wetu tusingekupigia blah blah blah
(Amehamaki temper is at max, breathing heavily) , au unataka nikate simu
eeeeh
Maundumula: Bora ukate tu mama maana naona hatutaelewana
Caller: Tiii tiii (Hang up)
Ushauri wangu: Hizi kazi za mawasiliano ni vyema wawe wanapewa watu
ambao wamesomea na communication skills japo kidogo. Huwezi kupiga simu
hujajitambulisha wewe nani na unapiga kutoka wapi halafu on top
unajifanya una haraka wakati hiyo mojawapo ya kazi yako.
Ni aibu kwa taasisi kubwa kama hii kutokuwa na mtu competent wa kuweza
kupiga simu akaongea kwa kueleweka tena kwenye lugha ya nyumbani.
Nadhani next time watu kama hawa wakikupigia wao wakiongea Kiswahili
dawa yao kuwajibu kwa kizungu . Kizungu huwafanya watanzania waende
kwenye point moja kwa moja :happy:.