Huyu fundi wa hizi sarakasi ni nani?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,643
698,112
Baada ya rais mstaafu Jakaya Kikwete kurudi tena madarakani kwa mara ya pili alifanya jambo ambalo lilishutumiwa sana. Alikusanya watendaji wa serikali karibia wote na kwenda kufanya semina elekezi kwenye hotel ya kifahari ya Ngurdoto mkoani Arusha.

Kiuhalisia maudhui ya semina naweza kusema kwamba hayakupewa kipaumbele zaidi ya watu kula bata kwa raha zao. Hakika usemi wa kazi na bata ulipata umaarufu sana kipindi kile.

Ukiachana na mapungufu ya ile semina lakini watendaji wale walitoka pale na kitu kikubwa sana! Kule kuwakutanisha nje ya taratibu zao za kawaida za majukumu ya kila siku kulisaidia sana kuwajenga na kuwaleta pamoja na kuwafanya kuwa kitu kimoja.

Semina elekezi hizi ziliendelea kila wakati kwa kipindi chote cha utawala wa JK. Hawa watendaji walipata nafasi ya ku relax, kupunguza uchovu, kutoa stress kufahamiana kwa karibu nje ya taratibu za kazi.

Baada ya Kikwete kumaliza muda wake alimkabidhi kijiti marehenu hayati Magufuli. Huyu alifuta kila kitu, si semina elekezi wala makongamano makazini. Maono yake hayakuwa ya JK! Watendaji lile bata la JK likakoma na kuanza kutimiza majukumu yao kwa pressure kubwa na hata kama kulikuwa na semina au kongamano kukawa tena hakuna bajeti za vyakula na kumbi za kukodi.

Mambo yaliishia idarani tena kwa maji na biskuti ikawa sasa sio KAZI NA BATA tena bali HAPA KAZI TU.

Haya mambo ya sasa ya watendaji kupishana kauli ama kila mmoja kuongea lake ni matokeo ya kauli mbiu ya hapa kazi tuu. Na wala hayakuanza sasa. Huu ni mwendelezo tuu toka enzi za mwendazake.

Huu mgongano wa kauli na kulifungia gazeti la chama kwa siku saba ni matokeo yaleyale ya kukosekana mawasiliano, umoja na kujitambua kwamba nani anapaswa kufanya nini kusema nini na wapi!

Nikikumbuka matamko ya watendaji wakati wa Magufuli nabaki tu kucheka.

Hakuna aliyekubali kuwa chini ya mwingine bali kila mmoja alijitahidi kutoa tamko kali kuliko mwenzake ili kumfurahisha bwana Mkubwa.

Sakata la mchungaji Gwajima aliyeichokonoa serikali vilivyo limechukua sura mpya baada ya serikali kupitia waziri wa afya kutoa amri/agizo la kukamatwa Gwajima mchungaji na jeshi la polisi ambalo ni organ ya serikali.

Mkuu wa jeshi la polisi bila fikra na tafakuri alipoulizwa kuhusu kukamatwa Gwajima alisema hajapata wito rasmi wa maandishi toka serikalini, lakini hata hivyo akaenda mbali na kutoa ushauri na maelekezo.

Kwamba hata akipokea oda ya kumkamata Gwajima mchungaji basi wataangalia kama kuna jinai na kama basi ipo jeshi la polisi litashauri wamalizane kwa njia ya mazungumzo!

Kwanza mzee Sirro ajue kwamba hili si suala la ndugu wawili mtu na shemeji yake hata atoe ushauri 'wamalizane wenyewe' hili ni la kiserikali.

Pili mzee Sirro alikuwa kwenye nafasi nzuri kabisa kujibu kuwa wanafanga mawasiliano na wizara au na waziri! Full stop! Mengine yote aliyoongea hayakuwa mahali pake! Je, wakati wa kayafa angefanya hivi?

Mawasiliano ya watendaji yanafanyika mitandaoni na bila kuwasiliana kwanza, yaani ni kama kuna kuoneshana ubabe na ujuaji.

LAKINI ukiachana na hayo yote kuna tatizo kubwa huko ndani, waziri ni mdomo wa rais, akisema waziri ni agizo la serikali lenye ridhaa ya rais na organs za serikali zinachotakiwa kufanya ni KUTEKELEZA KWANZA!

Kuna dharau juu ya wanawake inajitanabaisha hapa na kuna kikundi ndani ya mamlaka hakikubali kuongozwa na wanawake! Je, Gwajima na Sirro ni sehemu yao?
 
Weee Mzee inji hii ukiiwaza sana utachanganyikiwa, kuna kitu kinaitwa agenda denie hiyo walifaulu sana mataifa ya kijamaa, na kitu hii inafanya kazi sehemu nyingi hasa kwetu na siku wananchi wakistuka utaona moto wake, ndio maana inaitwa bandika bandua na ujue wako well calculated maaana tozo chali, katiba chali, mbowe atapewa dhamana na kuachiwa kisela maana marekani wamewavua nguo, maisha yanaendelea na hii ndio bongo ambayo kabla ya kuingia lazima upite maili moja
 
Sometimes huwa nawaza hii nchi bora Taleban waje wawatie bakora watu akili zikae sawa...sina uhakika kama ukamatwaji wa viongozi na wanachama wa CHADEMA kunakuwaga na discussion ndefu namna hii
 
Kwamba jembe linahitaji kuwezeshwa kwa kuchomekwa mpini,

NB.
Mpini unachomekwa sio kuwekwa.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
Kwamba jembe lina tobo...! Na bila tobo wala mpini wa kuchomeka si lolote si chochote?
Kwamba mpini mpini una faida nyingi kwa maana ya matumizi bila jembe!?
TFKbPPc3c806ZwSzI7UO.jpg
 
Back
Top Bottom