Jana majira ya saa 10 jioni nikiwa Igunga gari yenye namba za usajiri KUB ikiwa na bendera ya taifa ilitupita ikielekea shinyanga jamani huo sio mwendo, ni hatari kama sio balaa, sasa unakimbilia wapi? trafik nao wakiona bendera wanakimbilia vichakani, wakamateni hata kama ni msafara wa JPM kama uko katika mwendo hatarishi wakamateni, hii tutaokoa maisha ya watu na rasilimali za taifa. Leo tena nimesikia gari ya mkubwa umeparamia gari ndogo. Viongozi na watumishi wa umma na wabunge wawe mstari wa mbele kutii sheria za barabarani jamani.

