Huyu demu amekua Mkuruzinza

Huyu demu amekua Mkuruzinza

bongompya

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2015
Posts
224
Reaction score
43
Siku moja nikiwa kwenye matembezi ya jioni Mala nikakutana na dada mmoja mrembo kwelikweli,Kama kawaida ya mwanaume kumuacha mrembo yeyote apite kihasara ni kosa la jinai.Basi nikamsimamisha na kuanza kuchezanae(Kumtokea).Baada ya kuongeanae kirefu nikamuuliza kama ana mchumba au kama alishakwisha olewa akanijibu sio(hana mchumba na wala hajaolewa),Na akanihaidi kuwa atanipa jibu kwa ombi langu.

Baada ya kuachana nikafanya utafiti wangu na kugundua ana mahusiano na baba mmoja ambaye alishaoa na ana familia yake,na kwa sasa huyu baba kampangia Huyo mrembo vyumba viwili na sebule.Basi ilipopita siku zipatazo kama tatu hivi nikabahatika kukutana na nikaongea nae kwa mala ya pili juu ya kile nilichomueleza siku ile.
Basi mrembo akanijibu kuwa ombi langu limekubaliwa na yupo tayari kuanza mahusiano na Mimi.

Basi tukaendelea kuzungumza na nikamuulize kulikoni aliweza kunidanganya siku ile kwamba hana mchumba wakati ana baba ambaye amempangia chumba na anakucha avyotaka?
.Demu kakataa katakata kwamba hana mtu yeyote na wala hajaolewa.Basi kama ujuavyo za Mwizi arobaini,ilipopita kama wiki mbili hivi,nikawa nimetengeneza nae appointment kwenye grosali moja ili kutae na tuongee kuhusu mambo yetu, kabla hatujaingia kwenye hiyo grosali tukiwa bado mlangoni demu akakataa kuingia kwa kigezo kuwa amemuona baba yake mzazi yupo pale ndani ,tukabishana sana baadae akakataa katakata na kudai kuwa anarudi nyumbani kichwa kinamuuma sana.

Basi nikamuacha aende zake.Baada ya kufanya uchunguzi mwingine nikagundua kuwa pale kwenye ile grosali ,palikua na yule baba aliyempangia chumba anapoishi ndo maana alikataa kuingia siku ile.

Basi nikafanikisha kukutana nae kwa siku nyingine na kumdadisi kwa nini siku ile alinifanyia vile alikataa sana lakini baadae aliweza kunieleza ukweli kwamba pale ndani palikua na mtu anayemfahamu na akutaka ajue kinachoendelea kati yake na mimi.

Nilisikitika sana kwa sababu alishindwa kuwa muwazi kwangu na kuamua kunidanganya kwa mala nyingine.

Toka siku hiyo niliamua kuachanane na sikuweza kumtafuta tena,Juzi juzi alinipigia simu na kuomba tukae tuzungumze na tumalize tofauti zetu,na sasa amekua msumbufu mpaka najuta kwanini nilimpa mawasiliano yangu,Hivi kwa nini wadada wengi sikuhizi wanapenda kutembea na baba zao,pia kwanini warembo wengi wanakua sio wawazi na sio waaminifu kwa wapenzi wao?
 
Kumbe hiki ni kipindi cha likizo shule zimeanza kufungwa.

Huyu mwanafunzi amesahau kuweka hata aya.
 
Ulipokutana nae baada ya wiki mbili ina maana ni siku 14 na sio 40
 
unaandika kama gazeti mkuu fupisha ,,pia ulichoandika ni pumba tupu na uongo ndiyo tatizo la tuvulana badala ya kwenda tituion kipind hiki.mmrfunga ,,umekuja humu
 
huyo kidosho amekwambia huyo ni baba yake.....?. ukute mwenzio anaitwa baby uzee mwisho chalinze mjini kila mtu baby
unanikumbusha professor mmoja UDSM aliitwa mzee, alikataa akasema wazee wapo manzese mie ni prof
 
Back
Top Bottom