Huyu dada anatafutwa na ndugu zake

Huyu dada anatafutwa na ndugu zake

Kigoma sio kanda ya ziwa,rudi darasani ukajifunze vizuri Gepgraphy.
 
Anatafutwa.

Tafadhali sambaza ujumbe huu, na Mungu akubariki.

Jina:Sweet Martin.

Jinsi: Mwanamke.

Umri: miaka kati ya 29 hadi 33.

Alizaliwa Kanda ya Ziwa, inasemekana ni Mkoani Kigoma, wakati baba yake, Martin M. Mmassy, alikuwa anafanya kazi railway, Kigoma.

Baba yake ni mwenyeji wa Moshi.

Mama yake ni mtu wa Kanda ya Ziwa, na baada ya baba kuhamishwa kikazi, Sweet alibaki na mama yake.

Sweet inasemekana amewahi kusoma Uganda.

Amewahi kuwa na mawasiliano na shangazi yake, Justina M. Mmassy, ila toka shangazi afariki, mwaka 2010, mawasiliano kati ya Sweet na upande wa baba yake yalipotea.

Wadogo zake, Joseph Martin Mmassy, Simon Martin Mmassy, Jackline Martin Mmassy, wanahitaji kuwasiliana naye ili kujua alipo huyu ndugu yao, na kufahamiana.

Mawasiliano: +255 713 35 0489

Email: josephmmassy@gmail.com.

Tafadhali sambaza ujumbe huu. Mwenyezi Mungu akubariki sana.

Kafanya nini?report ya polisi weka hapo
 
Mungu akutangulie ktk juhudi zako za kuungana na member wa familia yenu.
Dah I wish ningekuwa namjua ningerusha mawasiliano.
 
Mungu akutangulie ktk juhudi zako za kuungana na member wa familia yenu.
Dah I wish ningekuwa namjua ningerusha mawasiliano.





Ninashukuru. Pia, kama unaweza kukopi na kusambaza Whatsapp, facebook, nk. ,fanya hivyo. Asante
 
Itakuwaje kama kweli ni ndugu yenu hata umri wake msiufahamu? Badala yake unaandika 29 - 33!!!!
 
Kigoma sio kanda ya ziwa,rudi darasani ukajifunze vizuri Gepgraphy.

Mkuu, inawezekana kijiografia hajakosea sana. Kanda ya ziwa ipi? Victoria au Tanganyika?
Tumeshikilia kanda ya ziwa Victoria. Kumbuka kuna nchi zinaitwa za maziwa makuu na Lake Tanganyika imo katika maziwa hayo!
 
Back
Top Bottom