Huyu Chura wa EATV

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
538
Jamani naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza Channel 5 kwa kuzidi kutuletea ubunifu mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine inatufanya tuburudike,

Hiki kichura ambacho mara nyingi huonyeshwa wakati wa kipindi cha kusaka waigizaji wa kipindi cha ze comedy, mara nyingi huwa kinanivunja mbavu kinoma.

Hongera sana aliyebuni hicho kitu pamoja na timu nzima ya EATV, together tunawakilisha.
 
ZionTZ I support u, tuko pamoja. Kila ninapousikia wimbo unaoambatana na miondoko ya chura huyo, namkumbuka na kuachia tabasamu. Mind you - tabasamu, kucheka, kunaongeza maisha ya mwanadamu. So, big up EATV!
 
Picha yake please kama kuna mtu anayo...i love that chura....kwa kweli..tena anaonekana hajawahi kujua duniani huwa kuna maji ya moto.
 
tuwekeeni basi na kale ka picha tuendelee kuburudika
aramba aramba aamm aaaamm
 
na hawa
Jumpingfrog.gif


DancerFrog.gif


Dancer2frog.gif
 
tuwekeeni basi na kale ka picha tuendelee kuburudika
aramba aramba aamm aaaamm

hahahhahahha firstlady umenikumbusha mbali hahahhhah, yani kweli haka kachura ni soo yani nilivyosoma tu hii coment yako nimecheka mwenyewe.....thts gud unajua, yani nikitokaga kwenye mishemishe af ghafla nikakaona kale kachura nakua kama nimeflash ubongo wangu.......full happy....af umeona ile mpya ya piipii kama hujaona angalia TV i think watakaonyesha kakicheza ile ngoma ya marlaw
 
kweli ni burudani ndani ya roho

WEWE FIRSTLADY NAONA UNATUZINGUA..... yani hawa chura wako micharuko namna hiyo unawalinganisha na yule wa eatv??? hahhahhahhahhah

kwanza hawanati na biti, yule full kunata na biti....angalia alivyocheza ule wimbo wa michael jackson, angalia ule wa pii pii af na huo unaoupenda wa taarab kwa stail hii watacheza vipi,,,,,
 
wengi twampenda wasiwasi wangu ni jinsi binti yangu mdogo anavyokata kama chura huyo
 
Yule chura ni kiboko anafurahisha sanaaaa, watoto wa jirani yangu wanalia ikitokea mtu akachange channel while watching that chura.
 
Ladyyyy hao chura wako hawana lolote, wanrukaruka tu hebu wafunze kukata mauno kama yule wa EATV bwana, huyo mmoja ni mmasai nini mbona hivyo?
 
Ladyyyy hao chura wako hawana lolote, wanrukaruka tu hebu wafunze kukata mauno kama yule wa EATV bwana, huyo mmoja ni mmasai nini mbona hivyo?
Sasa umkute yule wa EATV anacheza arambaaaa arambaaaa aaaaaamu aaaamu............ utachoka
 
Back
Top Bottom