Huyu bwana kaumia sana mimi kuolewaa

Huyu bwana kaumia sana mimi kuolewaa

Mamboz?
Jamn kuna watu hata sijui niwaweke kwenye kundi gani,sawa aliwahi kuwa wangu wa "moyo" ila ghafla akabadilika.Mawasiliano akakata na baada ya muda akanitangazia anaoa,basi kwa uhakika akanitumia mipicha ya harusi yake mpk memory ikajaa.ukweli niliumia ila Mungu si Jf namimi nikabarikiwa mume .

Miez miwil iliyopita ndio nilifunga ndoa takatifu, ukweli sikumjulisha coz sikuona sababu ya kufanya hvyo.Ila dunia haina siri taarifa ikamfikia akanipigia cm kunipa hongera basi, kuolewa ni baraka jmn nikawa najikuta tu napost picha na video za harus yngu kwenye status yangu wasap nikimshukuru Mungu. Sasa tangu huyu bwana kajua nimeolewa imekua kero kutwa ananipigia cm eti ananipenda,ooo mara harus yako ilinoga sana ,we mzuri aisee huyu mke niliemuoa hatuendan ,natamn turudiane na uchafu mwingi mwingi.
Sasa juzi kapost Instagram video yngu fupi niliyokua nikimuimbia mume wangu nyimbo ya Ed sheeran "perfect duet" half chini akaandika " I was d only one deserve this n not that ass" . kaniudh saaaana ,nmfanyej?? Nimwambie my lovely haya makaraha au ninyamaze tu??
Nyie wote bado mnapendana
 
Duuh! Tunatofautiana sana yaani mambo ya ndoa yangu sijawahi kuyapost kwenye mtandao wowote! Baada ya kuoa sikuthubutu kuweka picha yangu au ya mke wangu mtandaoni.


Nilipopata mke mitandao haikujua, nilipopata watoto mitandao haikujua, na mengineyo ya kifamilia mitandao haikujua wala haitajua.


Nikwambie kitu wewe ni tatizo tena kubwa maana bado una akili ya uwaruwaru, hujajua ndoa inasitiriwaje, hujajua kuwa hata mmeo atakuwa anakusoma kimya kimya utajikuta anaanza kutokukuamini taratibu. Acha kujianika mitandaoni maana inaonekana unapenda kujionyesha onyesha mitandaoni ili kuwakomoa adui zako.


Badili mtazamo wako wa kidemudemu uwe na mtazamo wa mke wa mtu, mblock huyo jamaa ikishindikana badili namba za simu, tumia jina lingine mtandaoni, tulia acha uwaruwaru.
Asante sokoro waito kwa kitchen party bila vyombo
 
Sasa kama umemtumia video ataachaje kujiwekea kwenye status? Kata mawasiliano kuanzia utakaposoma hii message.
 
Mtumie video ukiwa unamkiss mume wako...


Seriously, achana na drama zake, tena mpige biti kali sana aachane na maisha yako.

Ingekuwa kama mlipotezana ukaolewa bila ridhaa yake hapo ningekulaumu.....

Ila kulingana na scenario hiyo ilivyo ni kwamba yeye alishakutupa kwenye shimo la umauti kwa kuamua kuoa mtu mwingine..... Sioni tusi kubwa kama kuamua kuoa au kuolewa na mtu kwa maamuzi yako na unajua yupo anayekupenda na mlikuwa na malengo then mambo yakushinde urejee....huo ni utaahira wa karne tena huyu ukamchukulie "restraining order" ya polisi kabisa maana ana kichaa cha akili kabisa.....mkalie mbali.....
 
Najielewa zaidi hata ya neno jenyewe.
Ila kweli, na wewe hebu uache kuwasiliana nae......huo muda unatumia kusoma meseji zake fanyia mambo mengine......achana nae mawasiliano yaaani usije ukathubutu hata kumuota
 
"Dancing on the dark
with you between my arms
barefoot on the grass
listening to our favorite song"
Ed sheraan _perfect(my favorite song.)
Madam songa mbele na mmeo achana na huyo mbangua korosho.
Darling just hold my hand,
Be my man I ll be ur woman,
I see my future in ur eyes....
 
Ukichekacheka na mbwa kuna siku utaingia naye msikitini...
Nyie ndo mliofosi ndoa ili kulipiza mapigo....
Uyo atakukula siku
 
Jf post za kwanza zikiponda umekwisha kila mmoja atakuwa Angel
Na sifa zikianza post za mwanzo wanatiririka kusifia
Kwa hili leo mimi simo nimesoma tu
 
Jf post za kwanza zikiponda umekwisha kila mmoja atakuwa Angel
Na sifa zikianza post za mwanzo wanatiririka kusifia
Kwa hili leo mimi simo nimesoma tu
Ngoja nifanye Hii research mda wa Ziadi nkiwa Sina Kazi ya Kufanya naanza na
Sample size uzi 5000
Wenye reply zaidi ya 100
 
Mtafute huyo bwege kisha mwambie kinaga ubaga asikufatilie tena, na km akiendelea basi kinukishe kwa shemela ili akomeshwe ki_amberruty

Hilo la Amber rutty noma!
Wengine anaweza akajamtia kichaa!
Kwanini utake Mtu afanyiwe ushenzi wa kiasi hicho ?!
 
Hebu acha ujinga wewe khaaah!! Bwana wa zamani kinachikukereketa akituma maujumbe ni nini? Yaani kama vile na wewe unamkera mke wake. Block whatsapp, Instagram, facebook, Twitter and stop following or replying any text and call from him.
'Mwanamke mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe' am sorry for being bitter people like you can't change in soft approach.
Nakuunga mkono na miguu nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom