Kadiri siku zinvyokwenda usaliti wa ndoa unazidi kuwa jambo la kawaida sana. Dhamira za wengi wetu hazipo hai tena, hata roho haziumi tunavyofanya vitu vya kiovu namna hii kwa ndoa zetu, bila aibu tunaomba na ushauri kabisa namna ya kumiliki nyumba ndogo vizuri.
Mwili si wa kuuamini sana mahitaji yake na tamaa zake. lazima tujifunze ku-argue na tamaa za miili yetu. Wengi wetu tumekuwa shuleni kwa miaka takribani 20 tukinoa bongo zetu, nini faida yake kama tunatekwa na tamaa za miili teyu kirahisi rahisi? tumekua watumwa sana wa miili yetu, akili tumepewa za nini? kufikiri tumepewa kwa nini?
Usipokuwa mwaminifu kwa KIAPO cha ndoa yako, utawezaje kuwa mwaminfu kwa mengine?