Huyu baba mkwe simwelewi anataka Nini?

Hajui mlango wa kanisa wala msikiti. Inshort hana dini.
Sioni tatizo, ukizingatia anawakosea bila kuwa wazi. Muda ni mali.
Hilo kwake analiona pungufu kwa baba mkwe wake kitu ambacho ni kweli kwa wengi hilo ni pungufu.

Ila kuna namna ya kuliwasilisha hata kwa watu wasiokujua. Sitaki kuongeza neno mwishowe nionekane nami sina heshima.
 
Subiri mwakani
Si uko ndani !! Tatizo lako nini mummy???
[emoji23][emoji23][emoji23] Mnamponza mwenzenu... Jamaa ndoa kwake sio kitu cha muhimu kama kwa binti sasa hapa binti mawenge anahisi kana anataka achezewe mchezo maana mzee mpaka anapewa hela hataki Wafunge ndoa duuh mzee nae changamoto...!
 
Tulia dada huenda baba mkwe ameshaona kuna kitu upande wako hakiko sawa. Kumbuka wazee wanaona mengi,
Maana Hata inavoonyesha na hiyo pressure ya kutaka kufunga ndoa huyo mumeo unamchochea wewe.
We subiri mwaka kesho ufike,
 
Hapo baba mkwe anajaribu kupeleka muda mbele ili tuu kuhakikisha kama kweli hiyo ndoa haitakuja kuwa ndoano,anaogopa mwanae asije kupata stress za ndani ya ndoa huku ambapo itakuwa si kazi ndogo kutoka.
 
Wanga nao ni mzigo japo kuna wanga mwingine una manufaa. Lazima kuna vitu ambavyo hajavitimiza huko kilingeni huyo mkweo bibie. Lipelekeni mbele za Mungu.
Ila upande wa pili jitazame na wewe na utathmini mwenendo wako halafu ingia kwenye viatu vya mzazi kama wewe ungekuwa mzazi ungeruhusu mtu wa mwenendo kama wako aoe/aolewe na mwanao? Kama jibu ni yes tatizo lilopo sirini kwa mkweo si dogo.
 
Me naona msikurupuke kufunga hiyo ndoa coz mtakua mnajisumbua tu, msikilizeni mzee pengine kunakitu anakichunguza na pia nikushauri ujaribu kuperereza historia ya huyo mzee hapo kijiini kwao anaishi vipi nawanakijiji wengine ila kwa swala la kufunga ndoa msithubutu kabisa.
 
Kumbuka mzee anaakili na busara kuliko wewe, jitulize tu ukichachamaa utaharibu yawezekana hili nalo ni jaribu ambalo mzee anakupitisha kuhakikisha mwanaye haowi mtu asiyefaa. Be careful
 
Linalo wezekana leo lisingoje kesho
ndoa ni baraka sana watu wengi hatujui
 
Tafuteni wasimamizi wa harusi na wazee hapa Mjini kama mna ndugu mfunge ndoa achana na huyo mzee mungu atabariki ndoa yanu msiogope
 
Huu ndio ukweli aisee.
Kama ameshaanza naye maisha na wanakula,wanalala wote na kuamka wote kila siku wasiwasi wake ni nini sasa?
Hana lolote ni mpigaji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…