Huyu baba mkwe simwelewi anataka Nini?

Kulingana na maelezo ya Uzi wako, bila kukuficha ni kwamba umeonyesha tamaa ya mali za Jamaa na unalazimisha kuwa legal ili uwe sehemu ya mali hizo.

Unaonekana unalazimisha kufunga ndoa uli uwe sehemu ya umiliki Wa mali hizo. Utu uzima ni dawa Mzee kashakusoma kuwa unatumia nguvu nyingi kulazimisha ndoa, ula huyo zumbukuku wako hajatambua coz umemuweka kwapani.

Na kwa jinsi unavyoandika kwa baba mkwe inaonekana una matatizo sana ya kinidhamu ila ujitambui. Ova ova ovaa gonga like wadau twende zetu asituchoshe huyu gold digger.
 
Anataka ajue kama ilichezea usichana wako na huzai ndiyo basi tena atasamehe ata mahari.. [emoji23][emoji23]
 
Ukisikia shangazi anakwambia huyu mtoto Masikio hayafanani na familia kama mwanaume unahitaji jiongeza....KUNA KITU HUWI MWAZI NA BABA MKWE HATAKI MPOTEZA MWANAYE...ukweli mchungu
 
Ili Jambo wote tumejadili kwa pamoja Wala sio Mimi nalalamika hata mwenzangu sababu nimwajiliwa ivyo Kuna vingi anakosa ,, mfano hata hela ya likizo anapewa kidogo vitu ni vingi istoshe sio Mimi ninaemkazinia mkuu
Yaani uoe kwa sababu ya hela za likizo?samahani naungana na huyo Mzee,kuna kitu tumekiona ila huyo jamaa yako bado amepofushwa na mapenzi
 
Wenzako wana mwaka wa 16 na watoto 3 hawajafunga ndoa na maisha yanasonga wewe unalalamikia vimiaka viwili? Fikiria maisha sio ndoa, huenda hapo upo katka usahili na huenda ukafeli kwa unavyoonekana mlalamishi mlalamishi wa vitu vidogo vinavyofaa kuvutiwa subira.
 
Mahali umeshatolewa?,hebu nijibu hili tuendelee kushauriana vizuri
 
Hapo either baba mkwe hampendi mwali kwasababu zake mwenyewe au mwali hana sifa za kuwa mke lakini mzee hataki kufunguka.
Hii lugha sio nzuri kwa baba mkwe wako....

Samahani ila kuna tatizo mahali.
 
Yawezekana kabisa huyo baba mkwe amegundua mambo au vijitabia fulani Fulani ambavyo hapendezwi navyo, kwa hiyo anakuchunguza zaidi ili kujiridhisha na kuona kama umebadilika au hapana. Kitu cha msingi ni wewe mwanamke kwanza kujitathmini una kasoro au mapungufu gani ambayo yanamtia hofu/wasiwasi baba mkwe? Msiwe na papara wala jazba ktk kumshawishi baba mkwe ili akubaliane na uamuzi wenu, muwe na busara ktk kumshawishi, akiridhika moyoni mwake anaweza akabadili msimamo wake.

Pia kumbuka, ndoa siyo cheti bali ni upendo wa dhati kabisa kutoka moyoni mwa wanandoa, pamoja na kuwepo kwa mahusiano mema baina ya wanandoa wenyewe pamoja na ndugu zao wa karibu wa pande zote mbili za wanandoa, wazazi wakiwa wa kwanza.
 
Katika pitapita zangu zote, sijawahi kukutana na dhahma ya aina hii zaidi ya kinyume chake. Na nikienkuwaza zaidi nitajikuta nakutukania mkweo hata unione sina adabu, na nikiruhusu kufikiria zaidi nitajikuta nina kutukania mkeo na baba yake kwa neno ambalo litakuwa ni kukuudhi zaidi.
 
Ulikosea kukubali kuishi na huyo mwanaume bila ndoa.
 
Makosa ya wengine hayawezi kufanya kosa hilo lisiwe kosa.
 
Ilitakiwa aandikeje?
Hilo kwake analiona pungufu kwa baba mkwe wake kitu ambacho ni kweli kwa wengi hilo ni pungufu.

Ila kuna namna ya kuliwasilisha hata kwa watu wasiokujua. Sitaki kuongeza neno mwishowe nionekane nami sina heshima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…