Nadhani maneno ya Prof ni sahihi. Mimi juzi nilukwa nimekaa na Mama yangu mzazi, ambaye ni Kiongozi wa chama fulani pale tunapoishi, tukawatunamsikiliza DR Slaa alipokuwa anahojiwa na ITV ikiongozwa na Masako, Mama yangu alisema, huyu Baba ni hatari, yaani anaweza kutushawishi tumpigie kura. Mie nikamwambia, mama, kura ni siri, kama unaona mambo aliyoongea Dr ni mazuri, basi mpigie kura tarehe 31 hakuna atakaye jua kuwa umefanya hivyo. tuliishia wote kucheka na kumpigia makofi Dr. Prof alikuwa sahihi kabisa..