Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,891
HUWEZI KUWA TAJIRI KWENYE NCHI MASIKINI
Na, Robert Heriel
Nianze kwa kuwaomba radhi wale wote mnaofuatilia makala zangu kutokana na kukaa kimya kwa muda kidogo, mpaka kufikia watu wengi kunipigia simu na kuniuliza kulikoni mbona sitoi makala. Wengine wamekuja ofisini kwangu kunisabahi, wote nawashukuru sana. Nilikuwa kimya kidogo, kuna mambo ya kitaifa nilikuwa nafuatilia. Sasa nimerudi, nimeona nianze na hili la Mhe, Kigwangala ambaye ni Waziri wa Utalii hapa nchini.
Mhe. Kigwangala amejaribu kushauri vijana wa taifa hili wafute fikara na mtazamo wa kuajiriwa badala yake wajiajiri wao wenyewe. Ni wazo zuri mno lakini sio halisi kwa jamii yetu katika zama hizi. Hakuna asiyependa kujiajiri. Watu wengi hupenda kujisimamia kwa kila kitu ikiwemo masuala ya kazi. Lakini jambo hilo haliwezekani.
Moja ya falsafa zangu katika masuala ya kiuchumi ni kuwa; Mtu hawezi kuwa tajiri katika nchi masikini hata siku moja. Iwe ni umasikini wa kiuchumi, kifikra au umasikini wa aina yoyote ule. Hata katika muktadha wa kifikra, mtu hawezi kuwa na akili katika jamii za watu wajinga. Siku zote jamii jinga huzalisha watu wajinga, na kama atatokea mwenye kuonekana anaakili basi hizo ni akili kwa waliowajinga ambazo sio akili zenyewe bali ujinga uliorembwa.
Kuwaambia watu watafute utajiri kwenye jamii zao, ikiwa jamii hizo ni masikini, huko ni kuruhusu dhuluma na unyonyaji. Huko ni kuruhusu watu hao wanyonyana na kudhulumiana. Na yule mwenye nguvu na ujanja kidogo basi huyo ndio ataibuka tajiri kwa masikini wenzake.
Hakuna tajiri katika nchi au jamii masikini, bali kuna wanyonyaji na wanaodhulumu wengine na kujilimbikizia mali nyingi mno. Matajiri wote waliopo katika jamii zetu ambazo ni masikini, wote ni wanyonyaji, wezi na watu wenye dhuluma kwa masikini wenzao.
Wengine ni wasaliti, na matapeli wanaonyang'anya mali za wenzao kwa nguvu zote.
Mara kadhaa nimekuwa nikiongea na baadhi ya viongozi wa nchi hii, nikiwasisitiza kuhusu namna ya kuinua nchi hii lakini bado wamekuwa wagumu kunielewa. Sijajua ugumu wao upo kwa manufaa yao au ni kweli hawanielewi. Lakini bado ninatumaini ipo siku watanielewa.
Nchi yetu ni masikini kwa sababu inaundwa na jamii masikini. Serikali inapokuwa masikini ni wazi haiwezi kuunda taifa tajiri kwa kutegemea wananchi masikini, hilo katu haliwezekani, lazima likandamize na kunyonya wananchi wake Ili walau liweze kujiendesha.
Sishangai kwa nini watu wanalalamika mishahara ni midogo isiyotosha kitu. Huko serikalini watumishi wengi wa umma wanalia kwa ufinyu wa malipo. Waalimu wanalia na kufia katika umasikini usioelezeka, Mapolisi nao halikadhalika, hata hao wauguzi na matabibu kutwa kucha kulalamika. Mishahara ni midogo haiendani na kazi zao na hali ngumu ya maisha.
Wakandarasi na wahandisi kutwa kusubiri pesa zao. Serikali haina uwezo wa kuwalipa mishahara mikubwa kutokana na umasikini wake.
Nchi ni masikini kamwe haiwezi toa serikali yenye kufanya watu wawe matajiri bila kuruhusu watu kunyonyana na kudhulumiana.
Sishangai kuona wanasiasa wakilipana mapesa mengi, posho zisizoisha, wabunge na mawaziri hutembelea matako na magari ya bei ghali ambayo mafuta yake kwa mwezi ni mishahara ya wafanyakazi wengine.
Kwa bahati nzuri nimezunguka kidogo katika nchi hii. Viwandani nimejionea vijana wakisulubika kwa kazi zaidi ya masaa 12, tena kazi ya shifti za mchana na usiku. Imenilazimu nitaje mshahara japo sikutaka kufanya hivyo kutokana na uchungu wa dhuluma na unyonyaji wa wazi kabisa. Mtu analipwa laki na ishirini kwa mwezi ati huyo siku moja anampango wa kuwa tajiri thubutu yake.
Matajiri wote kwenye nchi masikini huko viwandani huwalipa wafanyakazi wake mishahara ya aibu, mishahara ya kitumwa, hao ndio huitwa matajiri ambao kimsingi sio matajiri isipokuwa jina sahihi ni wanyonyaji au wenye dhuluma.
Sekta ya sanaa katika fani ya uigizaji na muziki napo unyonyaji ndani nje. Wasanii wengi wamebaki kuwa wacheza sinema za kitoto kama wehu. Wamevurugwa na kuchanganyikiwa kutokana na malipo kidunchu wayapatayo. Kazi wanayoifanya ni kubwa, pesa wanayozalisha ni ndefu lakini wao hulipwa pesa ya kitumwa. Wengine imefikia hatua wanajiingiza katika dili chafu na hatari kwa usalama wao na usalama wa jamii, wapo waliojiingiza kwenye madawa ya kulevya kama vichaa. Ati wanaondoa stress za maisha, sonono na ufukara uliosababishwa na dhuluma walizofanyiwa.
Wengine ni makahaba wanaodanga kutwa kucha. Mpaka imefikia kuonyesha nyuchi zao ambazo ni aibu kwao na kwa kizazi chao. Huo wote ni umasikini. Mtu tajiri hawezi kukaa uchi au kujiuza na kujidhalilisha isipokuwa mwehu na aliyechanganyikiwa au mwenye laana.
Wafanyakazi wa ndani nao kilio, mishahara kama pesa ya matumizi ya mwanafunzi wa shule ya msingi, ati huo mabosi ndio wanauita mshahara, imefikia kipindi baadhi yao huwanyanyasa kabisa. Huwezi mlipa mtoto wa watu 50,000 hata kama anakula na kunya kwako. Huo ni unyonyaji.
Kutafuta utajiri kwenye jamii masikini ni kutafuta ugomvi na sheria za Mungu. Ni kujiingiza katika kudhulumu masikini na jamii yako mwenyewe.
Sijawahi kuona wala kusikia mtu aliyekuwa tajiri akitokea jamii masikini bila kunyonya wenzake au kuwadhuru kwa namna yoyote ile. Kama sio kuwauzia madawa ya kulevya, basi ni kuwaibia pesa zao za kodi, kama sio uganga wa kienyeji, badi ni pesa za utapeli za hawa wachungaji wahuni wa zama hizi.
Mhe. Kigwangala, kama ulikuwa hujui ni kuwa matajiri wote unaowaona, au wote wenye pesa waliopo nchi masikini basi jua hao ni wanyonyaji na wanaodhulumu wengine, ukiwemo na wewe. Huwezi kuwa na kipato cha zaidi milioni 10 kwa mwezi katika nchi kama hii bado usiitwe mnyonyaji. Watanzania wengi kipato chao kwa mwezi hakifiki laki moja wewe unapataje milioni na ushee katika nchi ya namna hiyo. Wewe lazima uwe nyonyaji.
Kuwa na ndoto ya utajiri kwenye nchi masikini ni sawa na kuwa na ndoto ya kuwa mdhulumati na nyonyaji lisilojali utu wala haki za binadamu.
Kitu pekee ambacho niliwahi kukisema siku za nyuma ni kuwa; lazima tutafute mahali pa kuufukuzia umasikini uliopo katika nchi yetu. Kama hatutaufukuza basi tutafanyana kuwa masikini sisi kwa sisi. Kama taifa, hatuna budi sisi viongozi kutafuta namna bora za kuzitawala nchi nyingine, nchi hizo ndizo tuzifanye shimo letu la taka, nchi hizo ndizo tuzigeuze makaburi ya kuzikia adui masikini, ujinga na maradhi. Nchi hizo ndizo tutafutie utajiri huko.
Serikali iunde mkakati kabambe uliosukwa kikamilifu bila ya kushukiwa na adui zetu.
Hakuna mtu makini anayeweza kujisifu kwenye nchi yetu kuwa yeye ni tajiri na anamaisha mazuri ikiwa asilimia 89 ya watanzania ni masikini. Mtu huyo labda awe mwehu, Nilimsikia Mo Dewji akikebehi mtu kukosa elfu kumi mfukoni, nikagundua anamatatizo makubwa ya kufikiri. Na ni kwa vile nchi yetu wajinga wengi, ila ingekuwa na watu wenye akili Mo asingethubutu kunyanyua mdomo wake kuongea pumba kama ile.
Wazungu wao wameamua kutuletea matatizo yao, ujinga wao wametuletea, dini zao za kipuuzi wametuletea, teknolojia yao ni nzuri lakini hawatufundishi namna ya kuitengeneza zaidi ya kuitumia nayo wametuletea, umasikini na maradhi wametuletea, sanaa na mitindo karibu yote ya nguo wametuletea, kwa nini wasiwe matajiri.
Utajiri ni kumfanya mwingine awe masikini, hiyo ni kanuni. Uhai ni kufanya mwingine afe, akili ni kumfanya mwingine awe mjinga, Uungu ni kumfanya mwingine awe kiumbe.
Sasa sisi tunatafuta utajiri humu humu, sisi kwa sisi ilhali sisi ni masikini. Lazima wengine wakione chamoto ili wengine wale bata.
Mwisho: Niombe Serikali ijadli namna bora ya kuliinua taifa hili kwa kuzitawala nchi zingine kusudi kupunguza umasikini kwa taifa letu.
Nafurahi kuona wenzetu wa Rwanda na Uganda wakihangaika huko Kongo. Kwa kweli mimi nawapongeza hata kama wenye ufinyu wa fikara wataona ninatabia ya uvamizi. Lakini ni heri tuvamie nchi zingine kuliko kuvamiana sisi kwa sisi.
Nipumzike sasa, Taikon wa Fasihi kwa sasa Nipo Morogoro.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300