Huwezi kuuficha uchafu kwa muda mrefu utajulikana tu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,044
2,000
Njia ya mwongo siku zote si ndefu, inaweza kuchukua muda kidogo lakini itajulikana tu na utabaki na fedheha.

Kuna kijana alipata kazi ya utaarishi katika ofisi ya ma Expatriates mjini miaka ya 90. Cha ajabu yule bwana alikuwa na pesa sana mtaani. Alimudu kununua gari na kuishi maisha ya gharama.

Kumbe aligundua kule ofisini wale maboss ni wageni nchini. Akiwa kama taarishi alitumwa kununua vitu vidogovidogo kama stationery na kupost barua. Kwa kila alichonunua aliongeza 0 moja.

Pale ofisini kulikuwa na utaratibu wa kuuza likizo na unalipwa mshahara wa mwezi kwa likizo yako. Huyu bwana aliuza likizo kwa miaka mitatu. Mwaka wa nne Managing Director alimwambia ni lazima aende likizo si vizuri kwa afya ya mwili na akili kutokuchukua likizo kwa miaka minne mfululizo.

Katibu muhtasi wa MD aliyasikia haya. Alimleta haraka mtoto wa kaka yake aliyekuwa likizo ya chuo na kuomba ashike ile nafasi kwa mwezi mmoja ili apate pesa ya kumsaidia chuoni.

Kijana mwanafunzi hakujua mchezo wa kuongeza 0. Alifanya kazi kwa uaminifu. Tofauti ya gharama iliwashangaza ma boss. Yule bwana high life alipoteza ajira baada ya likizo na aliondoka kwa fedheha kubwa.
 
Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
3,347
2,000
Kuna watu walikuwa wafanyakazi waaaminifu watiifu waandamizi ila maisha wanayoishi baada ya kustaafu ni shetani tu ndiye anayejua...kwanza unakua muaminifu kwa nani na kwa nini na kwa muda gani na wapi
Sijawahi kuona muaminifu akidhalilika. Huwa nawaona waliokua sio waaminifu wakiteswa na kisukari na dialysis mara 3 kwa wiki.
Mfano mzuri angalie polisi waliokua dhulmat waliostaafu. Halafu angalia waalimu wengi waliostaafu.
 
Jang-Bogo

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
2,510
2,000
Kuna watu walikuwa wafanyakazi waaaminifu watiifu waandamizi ila maisha wanayoishi baada ya kustaafu ni shetani tu ndiye anayejua...kwanza unakua muaminifu kwa nani na kwa nini na kwa muda gani na wapi
Kabisa mkuu. Ukishajiuliza huyo mtu wa kumfanyia huo uamnifu jinsi anavyokubana na kukupunja aisee unakosa kabisaa nguvu ya kuwa mstaarabu.
NB:
Hii michezo usiicheze kijinga tumia akil sana.Kama mm tu
 
hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
36,482
2,000
Kuna watu walikuwa wafanyakazi waaaminifu watiifu waandamizi ila maisha wanayoishi baada ya kustaafu ni shetani tu ndiye anayejua...kwanza unakua muaminifu kwa nani na kwa nini na kwa muda gani na wapi
Aisee imagine !!!!
 
Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
5,009

Naunga mkono hoja!
Uwe mwaminifu kwa wezi?
 
Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
5,009
2,000
Sijawahi kuona muaminifu akidhalilika. Huwa nawaona waliokua sio waaminifu wakiteswa na kisukari na dialysis mara 3 kwa wiki.
Mfano mzuri angalie polisi waliokua dhulmat waliostaafu. Halafu angalia waalimu wengi waliostaafu.
Kwani walimu sio waaminifu?

Kwa zama hizi... .. uaminifu ni cheo!
 
Top Bottom