Huwezi Kumsema JK, Ukamwacha Mwl.Nyerere!

Huwezi Kumsema JK, Ukamwacha Mwl.Nyerere!


Nitatoa mf. watu wanasema Raisi Kikwete ni omba omba na anatembeza bakuli, mambo ya kutembeza bakuli sio ya JK bali ni Sera za CCM ambazo zilianzishwa na Mwl.Nyerere na wenzake, Mlm.Nyerere na wenzake waliamini ktk Misaada na wakafanya kuwa ndio sera za nchi na ndio maana kila kitu ktk nchi yetu tunategemea Wahisani, Shule zetu tote zimekuwa zikisaidiwa na Wazungu au Wahisani kuanzia Maabara mpaka Vitabu, mimi watati niko Sekondari tulikuwa tunajua Mashirika yoote ya Nchi wahisani kwa majina kama CIDA, DANIDA, JICA n.k kwa nini?
Hivi takwimu za watanzania wanaofanya kazi private sector kwa sasa zikoje na wengi wameajiriwa na wazawa au makampuni ya kigeni. Chukulia makampuni ya simu, mabenki ya kigeni (yanayotoa mikopo ya biashara na faida zake kiuchumi), wawekezaji kwenye mahoteli ya kigeni na sasa kwenye maliasili wasingekuwepo ni watanzania wangapi leo wangekuwa jobless au wangeathirika kwa upungufu wa hizi services.

Au nitajie mtanzania mmoja tu unae mjua wewe anaetoa ajira zaidi ya 2000 (minus Bakhresa) yeye peke yake na kampuni yake kwa sasa, impact ya hiyo kampuni katika sector zingine za uchumi na faida kwa jamii. Vinginevyo tushukuru wawekezaji ama sivyo leo ujambazi na utapeli ungekuwa zaidi ya tatizo tulilonalo na umaskini wetu. Embu tujifunze kushukuru ata kidogo sio kulalama tu kila kukicha na mambo ya hadithi za vijiweni, bila ya kuzingatia uhalisia wa mambo kama vile dunia inazunguka siku miatatu na sitini na nne na robo siku, na kingine: mbetta.

Ni sawa kupinga terms of uwekezaji lakini si kujidanganya vingine, kwa nchi maskini.
 
Watu wengi wanamsema Raisi Kikwete lkn wanamtetea Mwl.Nyerere, wasichokijua ni kwamba kila kitu ambacho Raisi Kikwete anakifanya kimeidhinishwa na Chama chake au ni Sera za CCM ambazo ziliasisiwa na Mwl.Nyerere na watu wake.

Nitatoa mf. watu wanasema Raisi Kikwete ni omba omba na anatembeza bakuli, mambo ya kutembeza bakuli sio ya JK bali ni Sera za CCM ambazo zilianzishwa na Mwl.Nyerere na wenzake, Mlm.Nyerere na wenzake waliamini ktk Misaada na wakafanya kuwa ndio sera za nchi na ndio maana kila kitu ktk nchi yetu tunategemea Wahisani, Shule zetu tote zimekuwa zikisaidiwa na Wazungu au Wahisani kuanzia Maabara mpaka Vitabu, mimi watati niko Sekondari tulikuwa tunajua Mashirika yoote ya Nchi wahisani kwa majina kama CIDA, DANIDA, JICA n.k kwa nini? Ni kwa sababu walikuwa ndio wanakarabati Shule zetu, wanatuletea Walimu, wanaleta Vitabu n.k, hata hili la juzi la JK kuomba msaada wa Walimu ktk Jamaika ni muendelezo tu wa hizo Sera, zamani walikuwa wanatuletea walimu ktk Cuba, Trinidad na Tobago n.k

Kwa kifupi ni kwamba raisi yoyote yule maadamu atatoka CCM lazima atakuwa mtembeza Bakuli kwa maana ndio Sera za Chama na Nchi kwa Ujumla...


1. Mwl Nyerere aliitumiaje hiyo misaada?

2. Elimu wakati wa mwl ilikuwaje (hasa katika shule za serikali)?

3. Mashirika ya umma na viwanda kama TAZARA, TIPPER, TRC, UDA, TANGANYIKA PARKERS n.k. yalikuwaje?

4. Mwl na familia yake walimiliki mali kiasi gani?

5. Mwl alisafiri kwenda nje mara ngapi?

6. Maliasili zilitumikaje wakati wa mwl?

7. Viongozi wabadhirifu walifanywa nini na mwl?

Ukishindwa kuyajibu haya, muulize mzazi wako, inawezekana ulikuwa hujazaliwa bado.
 
1. Mwl Nyerere aliitumiaje hiyo misaada?

2. Elimu wakati wa mwl ilikuwaje (hasa katika shule za serikali)?

3. Mashirika ya umma na viwanda kama TAZARA, TIPPER, TRC, UDA, TANGANYIKA PARKERS n.k. yalikuwaje?

4. Mwl na familia yake walimiliki mali kiasi gani?

5. Mwl alisafiri kwenda nje mara ngapi?

6. Maliasili zilitumikaje wakati wa mwl?

7. Viongozi wabadhirifu walifanywa nini na mwl?

Ukishindwa kuyajibu haya, muulize mzazi wako, inawezekana ulikuwa hujazaliwa bado.

1. Misaada ilipelekwa kule kwenye Wakatoliki wengi na sehemu zingine hususan za Waislaam wengi kama vile, Dar., Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani, Kigoma, Tabora. kusahauliwa kabisa.

2. Elimu ilianza kufa mara tu baada ya Nyerere kuanzisha Azimio La Arusha, ikawa hakuna kusoma tena isipokuwa muda mrefu wanafunzi waliutumia, kufagia madarasa na viwanja vya shule, kulima bustani na mashamba, kuuza maandazi na vitumbua vya walimu. Waliosoma na kusomeshwa ni wale waliokuwa shule za Kikatoliki tu.

3. Tanganyika Packers (si parkers kama ulivyoandika) hii ilikuwa si ya Serikali, Serikali waliitafisha kutoka kwa akina Bathawab, ilikuwa ni kiwanda binafsi na mara baada ya Nyerere kukichukuwa kikaanza kufa kidogo kidogo mpaka kikafa kabisa wakati wake. Hizo zingine zote zilikufa kabla Nyerere kufa na zilizobaki basi ni jina tu, ziko hohe hahe.

4. Mwalimu na familia yake wanamiliki kijiji cha kifahari kinaitwa Mwitongo huko Butiama, kaburi lake ni kama nyumba ya kuishi mtu mwenye uwezo leo hii Tanzania licha ya utajiri mwingine uliopo Mwitongo. Pia wanamiliki Ardhi, Jumba na viwanja vikubwa kando kando ya bahari Msasani Dar. Wanamiliki Ardhi kubwa huko Geza Ulole Dar.

Licha ya hayo, bajeti ya kuendesha majumba yao ya Msasani na kuendesha Mwitongo, yote inatoka Serikalini.

5. Mwalimu hakuweza kusafiri sana kwenda nje kwani alikuwa kajitafutia matatizo lukuki humuhumu ndani ya nchi. Na alikuwa hamuamini mtu, kwani alikoswa-koswa kupinduliwa mara chungu nzima (rekodi ya kutaka kupinduliwa mara nyingi kwa Marais wa Tanzania anaishikilia Nyerere).

6. Maliasili zilianza kuibiwa kwa wingi wakati wa Nyerere, magendo ya meno ya tembo ndipo yalipoanzia ikabidi mpaka jeshi litumike (haikusaidia sana). Burundi ilikuwa wanauza meno ya tembo nje nje na hawana tembo hata mmoja, wakaibuka huko watu maarufu na matajiri (kutokea Tanzania) mpaka wakawa karibu na Michombero hususan aliyejulikana kwa jina la Sharifu wa Mabamba, mikoa ya kati wakaibuka akina Mohamed Mabruki, akijulikana wazi ni muuaji wa tembo na alikuwa akitembea na fedha kwenye buti la gari, akishikwa siku moja ya pili yuko nje.

Huyu unaemsikia anajiita "Born City" maarufu Dar, ndipo utajiri wake ulipoanzia, kuuza meno ya tembo wakati wa Nyerere, mpaka leo anadunda. Mpaka kuna Mgiriki mmoja alijisahau akadai kuwa Serikali ya Nyerere yote iko mfukoni mwake (Nyerere alikasirika sana) huyu alijihusisha sana na "mawe", wakati huo Watanzania wengi walikuwa wajinga sana na mawe ya thamani hawakuyajuwa yalikuwa yakitoroshwa kama njugu. Hasira zake akamfunga huyo mzungu bila kumpeleka mahakamani (udikteta). Lakini wazungu kama ujuavyo walikuwa ndio kiboko ya Nyerere, akatumwa mtu wa kanisa, na Nyerere anavyoliogopa kanisa, akamwachia.

7. Hakuna kiongozi mbadhirifu aliyefanywa chochote na Mwalimu, waliuwa viwanda alivyotaifisha Nyerere, waliuwa viwanda alivyoanzisha Nyerere, waliuwa mabenki aliyotaifisha Nyerere, waliuwa mashamba aliyotaifisha Nyerere na hawakufanywa chochote kwani wengi wao walikuwa watu wake wa karibu kama si kikabila basi kiimani.

Kwa kifupi, Nyerere aliiuwa nchi akaiwacha masikini hohe hahe, siasa yake ya ujamaa ikashindwa, uchumi ukashindwa, tukawa masikini wa mwisho duniani, elimu ikawa duni kuliko nchi yoyote ya Afrika Mashariki, kila umuonae taabani kuliko mwenzake. Udikteta ukazidi. Njaa mtindo mmoja, chakula kwa foleni, kilimo kimeshuka mpaka Wamerekani wakatuletea msaada unga tusioujuwa huku kwetu wa rangi ya manjano, ukapewa jina unga wa Yanga.

Eeh kijana usitukumbushe taabu, dhiki na madhila tuliyokumbana nayo wakati wa Nyerere.

Leo mshukuru mna neema kubwa sana, mnachaguwa mle mchele wa wapi Nzega, Mbeya , Kyela, china, Pakistan au Pemba? hayo tulikuwa nayo kabla ya Nyerere kutawala, alivyoingia madarakani yeye tu baada ya muda mfupi yakatoweka, tukaishi kwa taabu sana mpaka alipong'atuka, kushika tu Mwinyi, neema zikaanza kurudi.
 
Faiza fox unamjua vizuri sana JKN umemaliza kila kitu labda umuulize ndugu Nyerere alikuta Tanganyika ina barabara za lami km ngapi na aliondoko kivukoni alipo ishi kwa Robo karne aliongeza km ngapi halkadhalika shule za aina zote hospitali za aina zote achilia mbali sekta binafsi na sekta zisizo rasmi.
 
Back
Top Bottom