Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 10,622
- 18,279
Watu wengi wanamsema Raisi Kikwete lkn wanamtetea Mwl.Nyerere, wasichokijua ni kwamba kila kitu ambacho Raisi Kikwete anakifanya kimeidhinishwa na Chama chake au ni Sera za CCM ambazo ziliasisiwa na Mwl.Nyerere na watu wake.
Nitatoa mf. watu wanasema Raisi Kikwete ni omba omba na anatembeza bakuli, mambo ya kutembeza bakuli sio ya JK bali ni Sera za CCM ambazo zilianzishwa na Mwl.Nyerere na wenzake, Mlm.Nyerere na wenzake waliamini ktk Misaada na wakafanya kuwa ndio sera za nchi na ndio maana kila kitu ktk nchi yetu tunategemea Wahisani, Shule zetu tote zimekuwa zikisaidiwa na Wazungu au Wahisani kuanzia Maabara mpaka Vitabu, mimi watati niko Sekondari tulikuwa tunajua Mashirika yoote ya Nchi wahisani kwa majina kama CIDA, DANIDA, JICA n.k kwa nini? Ni kwa sababu walikuwa ndio wanakarabati Shule zetu, wanatuletea Walimu, wanaleta Vitabu n.k, hata hili la juzi la JK kuomba msaada wa Walimu ktk Jamaika ni muendelezo tu wa hizo Sera, zamani walikuwa wanatuletea walimu ktk Cuba, Trinidad na Tobago n.k
Kwa kifupi ni kwamba raisi yoyote yule maadamu atatoka CCM lazima atakuwa mtembeza Bakuli kwa maana ndio Sera za Chama na Nchi kwa Ujumla...