Huwezi kumchunga mwanamke!

Huwezi kumchunga mwanamke!

M2mwembamba

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2014
Posts
2,491
Reaction score
1,097
Kiukweli mwanamke huwezi kumchunga bali yeye akiamua kujichunga mwenyewe na kukuheshimu Ilikuwa mwaka 2006 pale demu wangu tuliyependana sana aliponieleza kuwa amepata mwanaume wa kumuoa kipindi hicho naishi Bukoba,kwakuwa nilikuwa sijajipanga kuoa nilimuruhusu bila kinyongo ila aliniahidi kamwe penzi letu halitakufa siku moja nikawa na shida ya elfu 70 nikampigia simu na kumueleza,akasema usijali ngoja nifanye makeke,kwa mujibu wake kilichotokea ikawa hivi:

Alimdanganya mume wake kwa njia tofauti anavyojuwa yeye ampatie pesa ikashindikana,ikapita kama siku tatu hivi,ilipofika usiku kama saa tano hivi akachukua vicks dawa ya mafua akaipaka kwenye kope za macho afu akaanza kudai tumbo linamsokota,akajinyonganyonga weee huku macho yanatoa machozi kutokana na ile dawa (vicks).

Mume wake akaamua kumpeleka hospitali,hapo alikuwa na mimba changa,basi banah! kufika huko kumbuka mgonjwa ndiye anayeingia chumba cha dokta,alichofanya akampa dokta elfu tano na kumwambia yeye haumwi ila anataka kwenda kijijini so kwakuwa ana mimba changa ampe dawa za kuzugia pia amshauri mumewe kuwa ni vizuri akitumia pia dawa za kienyeji,dokta bila hiyana akafanya hivo.

Haooo! wakarudi home,kesho yake akamuandalia laki na nusu huyoo kijijini wilaya ya muleba kamachumum kesho yake akanitumia laki moja na kuniambia mimi ni mwanamke nina mbinu za kila aina kiukweli nilichoka kwa mbinu aliyoitumia,hadi leo nikikumbuka hata mke wangu huwa simwamini wanawake siyo watu wa mchezo.
 
Sasa kama anakupenda kwanini alienda kuolewa? Yani mi nitoe hela ya mume wangu nimpe mchepuko?? Mscheewwww.
Yani mimi nikuwa bado sijawa na maisha ya kusema niishi na mwanamke,alivyonieleza nikamuruhusu kiroho safi
 
Sasa kama anakupenda kwanini alienda kuolewa? Yani mi nitoe hela ya mume wangu nimpe mchepuko?? Mscheewwww.
Kwa kweli siwezi kumtukanisha matusi mume wangu kiasi hicho. Kama ndo anampenda sana huyo ex wake angemrudia tu waoane. Mambo mengine unajidharaulisha wewe mwenyewe afu bado unamfanya mumeo aonekane boya tu. Kukosa akili huko
 
Ukitaka kujua Tabia ya mtu MPE Uhuru!!, ukimnyima atakuficha.
 
Kwa kweli siwezi kumtukanisha matusi mume wangu kiasi hicho. Kama ndo anampenda sana huyo ex wake angemrudia tu waoane. Mambo mengine unajidharaulisha wewe mwenyewe afu bado unamfanya mumeo aonekane boya tu. Kukosa akili huko
Itakua jamaa ana hela halafu bibie akaona fursa ila moyo uko kwa ntu mwembamba.
 
Back
Top Bottom