Huwezi kuamini mambo haya yapo dar!!!!

Huwezi kuamini mambo haya yapo dar!!!!

Dar ni jiji lililokuwa na watu chini ya laki tano miaka ya 70. Wakuja mmekuja kujazana sasa mnalalamika nini?

Kwa mara ya kwanza tunaona miradi mikubwa ya maji Dar ikianzishwa na Kikwete toka kabla ya Uhuru. Kuna mradi unaendelea sasa wa kufikisha maji Dar kwa kiwango cha juu kutoka Ruvu. Na pia kuna miradi mingine miwili inaendelea ya kuchimba visima virefu na vikubwa 40 huko Kimbiji vitavyoweza kuinywesha Dar kwa miaka 100 ijayo.

Ahsante Kikwete. Sijui Mirais iliyotawala kabla yake ilikuwa inafanya nini. Haikufikiria kabisa wala haijawahi kuchukuwa hatua zozote za kuipatia maji na umeme wa kutosha nchi hii.

Leo Kikwete ndio anaetekeleza miradi ya maji ya uhakika nchi nzima na umeme ndio usiseme maana kila mahala nchini kuna mradi wa umeme na maji wa aina moja au nyingine.

wanalalamika mji unakuwa majengo na idadi ya watu na sio miundombinu.au wewe ulitegemea Dar itakuwa na watu laki tano forever???
 
Back
Top Bottom