Huwa ninakosea wapi kwenye oral interview?

Huwa ninakosea wapi kwenye oral interview?

[QUO TE="Shark, post: 18980919, member: 21139"]Eti labda afe halafu azaliwe upya[/QUOTE]
Hahahahahaha!!!
 
Mi nakupa technique hatari ambayo utanikumbuka daima .Jenga ujamaa/undugu na paneli ya washili. Take them as a one family wth u
Hii imenifanikisha mara nyingi, inafika kipindi unapata majibu ya maswali hapo hapo kutoka kwao
 
mimi nilidanganywa konyagi nikinywa ntaongea kingereza safi kbsa tena kwa kujiamini .nikaamka asubuhi nikanywa.kwenye interview nilijibu ata ambayo sikuulizwa dah
hahaha mkuu ulipata kazi lakini?
 
Mimi nakumbuka enzi hizo nimeenda kwa muhindi kupiga interview...muhindi sasa English yake mbovu sijapata kuona...kauliza uliza maswali uchwara nimemjibu yote fresh...kakagua vyeti ananiuliza mbona umefaulu sana ...nikamjibu... swali nililochoka ni kwa nini sijavaa tie ... akasema kazi hanipi kwa sababu nimefaulu sana so ntamkimbia na pili sijavaa tie
 
Nyingine jamaa anauliza enhee unampango wakuendelea kusoma nikajibu ndio, mana nna diploma, akauliza kwanini hujajiendeleza mpk sasa nikamwambia sijapata ada mzee akasema kwaio unataka tukuajiri hapa uje utuibie upate pesa ya ada,toka hatuna nafasi hapa, nliishiwa nguvu aiseee i hate oral interviews
hahahahaha mkuu..ujue umenichekesha sana leo
 
Mkuu kwenye Oral epuka sana neno "sijui",nilikosa kazi kampuni moja hapo moroco kwa sababu ya hilo jibu.
nikarudia tena hilo jibu hivi karibun sema wazungu hawana taabu akaniambia usiseme kamwe hujui kwenye oral just speak out your idea. Mungu yu pamoja nawe,siku yako pia bado haijafika ikifika hakuna wa kuizuia just believe that
 
Aiseee oral nomaaa
Nakumbuka niliulizwa unafanya kazi gani kwa sasa nikajibu sina kazi yyte,kwanini huna kazi yoyote unaiba au pesa za vocha unapata wapi nikajibu ninakibiashara kidogo jamaa akasema nenda kaendeleze biashara yako hapa hatutoi mitaji
Ungeendelea kukomaa kama vile unapinga kutoka lakini wakikazia toka mzee.
 
wakuu,nikisema kuwa huwa siitwi kwenye usaili nitakua namkosea mungu wangu bure.
kuanzia mwaka juzi nilipomaliza chuo nimehudhuria saili 15 kati ya hizo 6 zilikua ni oral interview ambazo kwa mtazamo wangu niliona kama nimefanya vizuri tu.kwa mfano kuna NGO moja ya kimarekani ina ofisi zao pale mikocheni waliwahi kutuita watu123 kwenye usail ambapo walikua wanataka watu wawili pekee,tulianza interview kwa kwa kupewa mtihani wa kuandika ambapo tulichujwa mpaka tukabaki watu 16 ambapo tukachujwa tena tukabaki watu 6 ambao tuliingia kwenye oral ya kwanza ambapo tukachujwa tena na tukabaki watu watatu ambao tuliingia final interview,lakini baadae me nikakosa kazi.
so wakuu kwenye oral huwa wannangalia nini ili na mie niboreshe niweze kupata kazi?
Uwe demu mweupe au black beauty mwenye shape.
 
1 jua hadi unafika hapo kuna wenzio wamefikishwa hapo maana kila sehemu kuna ndugu wanaotaka ndugu zao wapate kazi. Mshukuru mungu omba mungu utakuja kupata,
 
Kuna sehemu nikituma maombi mkoa na ni serikalini tulitakiwa 2 tulioenda 53 tuliobaki kwenye oral 16 kwamimi Nilikua nasifa zote ila sikuitwa alikua kupewa mtoto wa mtawala na mwingine hata barua hakuandika simu tuu ilipigwa but yule ambae hakuandika barua alifanya mwezi tuu na kuomba kuacha kazi sababu hawezi Fanya kazi mkoani hivyo nikaitwa mie hadi Leo mwaka wa 4 tena serikalini
 
Kuna sehemu nikituma maombi mkoa na ni serikalini tulitakiwa 2 tulioenda 53 tuliobaki kwenye oral 16 kwamimi Nilikua nasifa zote ila sikuitwa alikua kupewa mtoto wa mtawala na mwingine hata barua hakuandika simu tuu ilipigwa but yule ambae hakuandika barua alifanya mwezi tuu na kuomba kuacha kazi sababu hawezi Fanya kazi mkoani hivyo nikaitwa mie hadi Leo mwaka wa 4 tena serikalini
Kwani mkuu ukifanya kazi serikalini kuna uspecial gani?
 
Back
Top Bottom