Hivi utumishi wanatumia utaratibu gani kwenye oral interview

kante mp2025

JF-Expert Member
Nov 11, 2022
630
1,193
Habarini wakuu wa kazi naombeni kujuzwa utumishi (sekretarieti ya ajira wanatumia utaratibu gani kumpata mshindi wa baada ya oral interview?

Kuna post moja ya kazi ilitangazwa waombaji waliofanya kwa usahili wa kuandika walikuwa kama 128 hivi baada ya mchujo wa kuandika wakabaki wasahili wa kwenda oral kama 12 hivi kumbuka hiyo nafasi ya kazi ilikuwa ni post ya mtu mmoja.

Swali langu ni je nafasi hiyo moja inagombewa na watu 12 wote au? na kama jibu ni ndio kulikuwa na haja gani ya kuwaita watu wote hao 12 kwa hiyo nafasi moja kwanini wasingewachukua walau hata watu wanne tu wenye top marks ili kurahisisha mchakato

Au huwa wanakuwa na nafasi zingine za siri nje na tangazo lao la nafasi hiyo moja.

Nauliza hivo nikiwa kama mmoja wa watu hao 12 tulioingia hiyo oral nikiwa na marks za mwisho kabisa yaani nikiwa mtu wa 12 katika hao 12 hapa naiwaza nauli niliyokopa kutoka mkoani kagera kwa nafasi moja watu 12

Mwenye uelewa zaidi anifafanunulie kwanini ile nafasi moja isingegombaniwa na walau hao vipanga at least wangewachukua wale top five ili sisi wagonga ulimbo tusiwe tumechezea nauli

Asanteni.
 
Mkuu ww ndo hauna nauli wao wanazo na wanaamini wote mna maisha kama ya kwao. KWahyo sio shida zao
Daah inaumiza kaka angu maana sikuona haja ya kuita watu wote 12 kwa post moja wangewachukua walau top five ili sisi wngine tungenunulia mbolea hiyo hela, unless kama wana nafasi za siri nje na na tangazo la ajira
 
Hufai kuwa kiongoz wa familia Kwa uoga ulio nao,, kama umepata nafas ya kuitwa jiamin na ujiandae kufanya interview na jisemee kua utapasua
 
Habarini wakuu wa kazi naombeni kujuzwa utumishi (sekretarieti ya ajira wanatumia utaratibu gani kumpata mshindi wa baada ya oral interview?

Kuna post moja ya kazi ilitangazwa waombaji waliofanya kwa usahili wa kuandika walikuwa kama 128 hivi baada ya mchujo wa kuandika wakabaki wasahili wa kwenda oral kama 12 hivi kumbuka hiyo nafasi ya kazi ilikuwa ni post ya mtu mmoja.

Swali langu ni je nafasi hiyo moja inagombewa na watu 12 wote au? na kama jibu ni ndio kulikuwa na haja gani ya kuwaita watu wote hao 12 kwa hiyo nafasi moja kwanini wasingewachukua walau hata watu wanne tu wenye top marks ili kurahisisha mchakato

Au huwa wanakuwa na nafasi zingine za siri nje na tangazo lao la nafasi hiyo moja.

Nauliza hivo nikiwa kama mmoja wa watu hao 12 tulioingia hiyo oral nikiwa na marks za mwisho kabisa yaani nikiwa mtu wa 12 katika hao 12 hapa naiwaza nauli niliyokopa kutoka mkoani kagera kwa nafasi moja watu 12

Mwenye uelewa zaidi anifafanunulie kwanini ile nafasi moja isingegombaniwa na walau hao vipanga at least wangewachukua wale top five ili sisi wagonga ulimbo tusiwe tumechezea nauli

Asanteni.
Je wakiitwa wachache na wasipofaulu itakuwaje? Acha kukurupuka mkuu hiyo ni taaluma watu wanakaa darasani miaka ya kutosha kusomea human resources . Hata kama wakifaulu wote 12 wengine watawekwa kwenye kanzi data
 
Daah inaumiza kaka angu maana sikuona haja ya kuita watu wote 12 kwa post moja wangewachukua walau top five ili sisi wngine tungenunulia mbolea hiyo hela, unless kama wana nafasi za siri nje na na tangazo la ajira
Huwa kuna wengine wanaitwa kazini kutokana na orodha kama hizo. Naskia wanawekwa kwenye kanzu data.
 
Je wakiitwa wachache na wasipofaulu itakuwaje? Acha kukurupuka mkuu hiyo ni taaluma watu wanakaa darasani miaka ya kutosha kusomea human resources . Hata kama wakifaulu wote 12 wengine watawekwa kwenye kanzi data
Ok nimekupata mkuu, hivi hr wa taasisi fulani anayo nguvu ya kumchagua mtu anayeona anafaa kwa taasisi yao kwenye panel ya oral interview (anao ushawishi wowote ule) hata kama interview zinaendeshwa na sekretarieti ya ajira
 
Back
Top Bottom