Huwa ninakosea wapi kwenye oral interview?

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
6,568
12,669
wakuu,nikisema kuwa huwa siitwi kwenye usaili nitakua namkosea mungu wangu bure.
kuanzia mwaka juzi nilipomaliza chuo nimehudhuria saili 15 kati ya hizo 6 zilikua ni oral interview ambazo kwa mtazamo wangu niliona kama nimefanya vizuri tu.kwa mfano kuna NGO moja ya kimarekani ina ofisi zao pale mikocheni waliwahi kutuita watu123 kwenye usail ambapo walikua wanataka watu wawili pekee,tulianza interview kwa kwa kupewa mtihani wa kuandika ambapo tulichujwa mpaka tukabaki watu 16 ambapo tukachujwa tena tukabaki watu 6 ambao tuliingia kwenye oral ya kwanza ambapo tukachujwa tena na tukabaki watu watatu ambao tuliingia final interview,lakini baadae me nikakosa kazi.
so wakuu kwenye oral huwa wannangalia nini ili na mie niboreshe niweze kupata kazi?
 
Shukuru Mungu umefikia hiyo level
 
Fungu lako lipo mkuu. Usikate tamaa mambo kazi siku hizi wengine wanacheza foul mimi ipo taasisi Nimefanya interview Mara mbili na ninafikia hatua tunabaki wawili ila nakosa. Mara ya mwisho niliposikia kwa nini sikuchaguliwa nilisikitika nkasema sitaomba tena kazi kwenye taasisi Hiyo disemba hii wametoa ila sijaapply. Kwenye kazi na interview mara nyingi hawachukia aliyestahili
 
Waajili wanataka mtu ambaye wanaa uhakika ataweza kufanya kazi watakayo mpatia.hivyo lazima kuwashawishi kwamba unauwezo wa kufanya hiyo kazi wanayo kufanyia interview

hivyo kama ulikosa bas ujue uliyeshindana naye aliweza kumshawishi mwajili kwamba naweza zaidi yako

lakini unaonekana una uwezo .maana unafikia mpka dkk za mwisho.wabovu wote huwa hawapii round yoyote
 
Aiseee oral nomaaa
Nakumbuka niliulizwa unafanya kazi gani kwa sasa nikajibu sina kazi yyte,kwanini huna kazi yoyote unaiba au pesa za vocha unapata wapi nikajibu ninakibiashara kidogo jamaa akasema nenda kaendeleze biashara yako hapa hatutoi mitaji
 
Nyingine jamaa anauliza enhee unampango wakuendelea kusoma nikajibu ndio, mana nna diploma, akauliza kwanini hujajiendeleza mpk sasa nikamwambia sijapata ada mzee akasema kwaio unataka tukuajiri hapa uje utuibie upate pesa ya ada,toka hatuna nafasi hapa, nliishiwa nguvu aiseee i hate oral interviews
 
Ongeza bidii kidogo.. Hata mie mwaka juzi niliikosa nafasi ya kuwa Zonal Manager, interview ulikuwa arusha na kampuni hukohuko....yaani tulibaki watatu na walikuwa wanahitajika wawili, Mimi kwa mtizamo wangu nikajua wale wenzangu hawaniwezi lazima nipite.. . yaani majibu tulipewa siku iliyofuata maana walituambia msiondike hadi mjue majibu yenu... Mm nilikosa ila wakaniita ofisini wakanieleza sàbabu zilizosababisha, moja kuu ni kwamba hawaajuri madereva hivyo unatakiwa ujue na uwe na licence, nikaelezwa wenzako wana licence wewe hakuna ndio maana panel ikaamua kama ulivyoamua....nikarudi home kurekebisha mambo kujifunza na kupata licence, tangu siku hiyo nikihudhuria huwa nabahatika ila nazuiliwa kuendesha napewa dereva....nawewe jichunguze udhaifu wako then ufanyie maboresha na muombe Mungu maana yote yanawezekana. Kukosa pia ni jibu ila mkumbushe Mungu kwamba siihitaji fedheha. Tupo pamoja kiongozi
 
Aiseee oral nomaaa
Nakumbuka niliulizwa unafanya kazi gani kwa sasa nikajibu sina kazi yyte,kwanini huna kazi yoyote unaiba au pesa za vocha unapata wapi nikajibu ninakibiashara kidogo jamaa akasema nenda kaendeleze biashara yako hapa hatutoi mitaji
ila inauma aiseee
 
wakuu,nikisema kuwa huwa siitwi kwenye usaili nitakua namkosea mungu wangu bure.
kuanzia mwaka juzi nilipomaliza chuo nimehudhuria saili 15 kati ya hizo 6 zilikua ni oral interview ambazo kwa mtazamo wangu niliona kama nimefanya vizuri tu.kwa mfano kuna NGO moja ya kimarekani ina ofisi zao pale mikocheni waliwahi kutuita watu123 kwenye usail ambapo walikua wanataka watu wawili pekee,tulianza interview kwa kwa kupewa mtihani wa kuandika ambapo tulichujwa mpaka tukabaki watu 16 ambapo tukachujwa tena tukabaki watu 6 ambao tuliingia kwenye oral ya kwanza ambapo tukachujwa tena na tukabaki watu watatu ambao tuliingia final interview,lakini baadae me nikakosa kazi.
so wakuu kwenye oral huwa wannangalia nini ili na mie niboreshe niweze kupata kazi?
Mlibaki watatu,wanaotakiwa ni wawili,hapo hata kama mngefungana kwa marks mia kwa mia ni lazima wawiwili tu ndio wachaguliwe.Sifa za ziada ni 'PERSONALITY'.
 
Mkuu ulikuwepo na wewe kwenye ile interview waliofanyia TC...House waliobahatika walipata kiongozi...mimi mwaka huu nimefanya interview 6, 2 nilipata 4 nilikosa..chamsingi jifunze kutokana na ulipokosea tu..
 
Katika usaili kuna mambo mengi sana na hawaishii kuangalia namna unavyojibu maana Unaweza kuwa ulisha google maswali ukayakariri yote, Unaweza kuwa unakosa kazi kwa sababu ya muonekano wa umbile lako, namna unavyoongea au pengine unavaa miwani ambayo hukufanya uonekane kama ni mtu mwenye majivuno.
Cha msingi jitafakari kuanzia muonekano, uongeaji na mpaka mavazi.
NB: inawezekana pia wengine wanatumia pesa
 
Sio maswali magumu hivyo ila mengine ni very tricky inataka practice at least siku moja kabla.
 
Back
Top Bottom