Huwa nakerwa sana na hii kauli 'Upelelezi haujakamilika'

mhuri25

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
2,667
3,454
Hello Wakuu ndani ya GT ni Jumapili moja maridhawa kabisa pengine ya mwisho kabisa kwa mwezi huu August...

Wakuu awali ya yote Mimi sio mwanasheria sisomi sheria na wala sina interest na sijawahi kuwa na interest za kusoma sheria....Kutokana na akili hizi za MEMKWA nilizonazo pengine ndio maana sielewi na pia najikuta nakasirika kila Mara ninaposikia kauli hii Wakili wa upande wa mashitaka kaomba kesi ihairishwe kwa sababu upelelezi haujakamilika, Au kesi flani imehairishwa na Hakimu flani maana upelelezi bado haujakamilika.....

Sasa Mimi hoja yangu ni hii utampelekaje mtu Polisi baadae mahakamani Afu anarudi magereza mtu anakaa zaidi ya mwaka magereza huku kila Leo akipanda kizimbani anaambiwa upelelezi bado haujakamilika!!! Aseeh huwa siipendi sana hii kauli Wakuu ila basi tu!!!

Mtu kaacha familia ndugu jamaa na marafiki wakati mwingine labda kaajiri kabisa watu na wanamtegemea anakaa magereza Muda mrefu tu... Kila Leo kesi haisikilizwi wala hakuna hukumu kisa upelelezi haujakamilika.... Kama huna ushahidi wa kutosha si umuache tu huyo mtuhumiwa....

Halafu mbaya zaidi mwisho wa siku huyo mtuhumiwa anashinda kesi....Daah miaka mi3 upo jela tu!!! Hicho kipindi si sawa na kifungo kabisa Wakuu!??

Hivi kwa kipindi chote hicho hauruhusiwi kisheria kufungua kesi mahakamani kuwa wamekupotezea muda Wakuu!!?? Kwa saabubu ya kauli moja tu inayokera kuwa UPELELEZI BADO HAUJAKAMILIKA!!!!
 
Hello Wakuu ndani ya GT ni Jumapili moja maridhawa kabisa pengine ya mwisho kabisa kwa mwezi huu August...

Wakuu awali ya yote Mimi sio mwanasheria sisomi sheria na wala sina interest na sijawahi kuwa na interest za kusoma sheria.... Kutokana na akili hizi za ki-MEMKWA nilizo nazo pengine ndio maana sielewi na pia najikuta nakasirika kila Mara ninaposikia kauli hii Wakili wa upande wa mashitaka kaomba kesi ihairishwe kwa sababu upelelezi haujakamilika, Au kesi flani imehairishwa na Hakimu flani maana upelelezi bado haujakamilika.....

Sasa Mimi hoja yangu ni hii utampelekaje mtu Polisi baadae mahakamani Afu anarudi magereza mtu anakaa zaidi ya mwaka magereza huku kila Leo akipanda kizimbani anaambiwa upelelezi bado haujakamilika!!! Aseeh huwa siipendi sana hii kauli Wakuu ila basi tu!!!

Mtu kaacha familia ndugu jamaa na marafiki wakati mwingine labda kaajiri kabisa watu na wanamtegemea anakaa magereza Muda mrefu tu... Kila Leo kesi haisikilizwi wala hakuna hukumu kisa upelelezi haujakamilika.... Kama huna ushahidi wa kutosha si umuache tu huyo mtuhumiwa....

Afu mbaya zaidi mwisho wa siku huyo mtuhumiwa anashinda kesi....Daah miaka mi3 upo jela tu!!! Hicho kipindi si sawa na kifungo kabisa Wakuu!??

Afu hivi kwa kipindi chote hicho hauruhusiwi kisheria kufungua kesi mahakamani kuwa wamekupotezea muda Wakuu!!?? Kwa saabubu ya kauli moja tu inayokera kuwa UPELELEZI BADO HAUJAKAMILIKA!!!!

Ai kotoni ende mai kondisheni...
Saabubu,, Duh heheh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kauli nyingine inaudhi "Hata hivyo watuhumiwa wameambiwa wasijibu chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina nguvu kisheria kusikiliza kesi kama hiyo" (In Reinfred masako's voice)

Sasa kama hamna nguvu kisheria si mngeipeleka kesi kwenye Mahakama husika? Yanini kupoteza mda kusoma tu kesi tena hata Mara nne ila haitakiwi Kujibu chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom